Zambia na Congo zaanza kutafuta njia mbadala kusafirisha mizigo yao

Zambia na Congo zaanza kutafuta njia mbadala kusafirisha mizigo yao

Imeuzwaje?
Wasio na Bandari wanategemea nini? Kuna Land locked countries kibao zinaendesha uchumi vizuri ije kuwa Sisi tuna chetu? Yaani tuuze utu wetu Kwa kisingizio cha uwekezaji? Tangu lini Mtu akakodisha bandari akapewa na anga?
 
Umesoma mkataba na kuuelewa? Umesikiliza hoja za wansheria waliofungua kesi Mahakama kuu kanda ya Mbeya? Umezielewa hoja zao?
Upotoshaji katika nyakati hizi za smartphone ni kazi rahisi sana. Mkataba wa IGA umeandikwa huko Dubai kwa mwaka mzima, yaani miezi kumi na mbili ya majadiliano ya kina. Hakuna anayeweza kukosa uzalendo na kuuza nchi kijinga hivyo.

Hao wanasheria wanakwenda kushindwa huko huko mahakamani tena mapema asubuhi tu. Hii ni vita nzito ya kiuchumi, kumbuka wapinzani wa hiyo bandari ni wengi na faida zake wanazijua.

Leo hii wakiona inashusha meli kumi ndani ya wiki moja ni lazima mioyo iwaume na wivu uwatese. Watawatumia watu wao humu JF, watawatumia mpaka wanasiasa waandamizi ilimradi tu watimize lengo lao katika haya mapambano.

Rais Samia na wasaidizi wako, hakuna kurudi nyuma.
 
Wasio na Bandari wanategemea nini? Kuna Land locked countries kibao zinaendesha uchumi vizuri ije kuwa Sisi tuna chetu? Yaani tuuze utu wetu Kwa kisingizio cha uwekezaji? Tangu lini Mtu akakodisha bandari akapewa na anga?
Bullshit mkuu bila bila, hakuna kitu kama hicho.
 
Shida sio dp world , shida ni mkataba gani tumeingia na dp world. First class countries kutokana na uwazi na sera zao wana uwezo wa kufanya lobbying hata na mashetani na bado wakapata reasonable deals. Huku kwetu dp akishahonga group la watu anaweza kuandika chochote kwenye mkataba , rejea mikataba ya symbion power projects.
Huku kwetu tunasikiliza wapotoshaji na kuwaamini bila ya kujua kuwa tayari wameshalipwa na maadui tunaoshinda nao kibiashara. Habari za kutungwa zinasambaa upesi kuliko ukweli wa mambo.
 
Mkuu kwani Angola nao wamekodisha bandari yao kwa mwekezaji kwa muda usiojulikana?
Hata Tz tunapenda sana wawekezaji. Shida yetu ni kwamba vifungu vya mkataba na DP world ndo haviko sawa kimaslai ya Taifa letu .Tukikubali tumeigawa bure bandari, mwekezaji akae kwa muda usiojulikana.

Alafu, Tz iwepo au isiwepo, mkataba wa DP World hauvunjiki. Kwani ni KISIKI???
Hakuna kifungu kisichosawa katika huu mkataba. Zaidi ya upotoshaji ambao baadhi yetu tumeamua kwa makusudi kabisa kuwa wapinzani wa mipango yetu wenyewe, so sad.
 
Southampton walipowapa DP World inamaanisha hakuna mwingereza anayejua kuendesha?

Kuwa na akili ya namna hiyo tu unamaanisha umejaza ujinga kichwani
Tanzania unailinganisha na uingereza? Huu mkumbo utaliangamiza taifa. Ndio walewale mnaosema hata marekani umeme unakatika.
 
These guys are confused! Yaani bandari iliyopo Atlantic Ocean ndio shortest route kwa mizigo yao itokayo Asia na china ? [emoji85]
Tuna shida mahala sisi waafrica pamoja na viongozi wetu .
Atlantic ocean haiwezi kuwa suluhisho la mkongo na mzambia kwa mizigo yao ya kwenda na kutoka asia na china. Hiyo lobito ya angola haina tofauti kabisa na beira port ambayo mzambia na mkongo inamshinda kwa gharama na language barrier. Mzambia na mkongo kwa mizigo ya asia ana option mbili tu viable, dar na mombasa port .
 
Ninachoamini wafanya biashara ndio wataamua watumie bandari ipi kutokana na mizigo inapokwenda

Bandari ya Dar ipo kwenye strategic position na hyo SGR ikikamilika ndio kabisaa itakua unbeatable
Geographic location ya bandari ya dar ni hot cake kwa karibu nchi 5 zinazotuzunguka . Dar pia ni cheapest destination of them all ports. Uganda peke yake ndiye at least anaweza kuamua kutumia mombasa port badala ya dar . Lakini si burundi ,rwanda, congo au zambia .
 
bandari ya Dar , haikimbiliki kirahisi hivo , inakila urahisi wa kifikika na nchi za ukanda wa kusini , Angola kwanza ni distance ya kutosha . watarudi tu hao ,
Angola picha la kwanza watakutana na lugha ya kireno !! Ndio kilichomkimbiza mzambia na mkongo bandari ya beira msumbiji
Pili huo mzigo utoke asia ukashuke lobito si bora hata waushushe durban kupunguza gharama? Mfanyabiashara gani atafanya expensive logistics kama hizo
 
Hacha kuuliza swali la kijinga umeona huo mkataba na kuusoma na unasemaje,ukilinganisha huo mkataba unaona unafanana kabsa na kutumika kwenye nchi iliyopata uhuru?
Wewe sema hivyo vifungu unavyodai vina shida?
 
Mimi Mkenya hapa, hili suala la bandari yenu nafuatilia kimya kimya ila nakosa kupata kuelewa nini haswa, maana kila mmoja ana hoja zake, au kasoma mkataba na kuelewa kivyake, mara bandari inauzwa, mara inakodishwa, mara ni ubia, mbona msiwe na lugha moja ambayo hata mama nitilie mtaani ataielewa?

Mnatupiana maneno hadi basi, utadhani ubishi wa Simba/Yanga wakati ni raslimali muhimu sana ya taifa......
 
Kwa maneno hayo. Nikisema wewe ni mjinga kuna watu watanibishia
Kama ambavyo na wewe unaweza kuwa mjinga kwake maana umeamini kuwa ufanisi wa bandari unaletwa na DPW tu..kwani duniani kote bandari zipo chini ya DPW tu!? Tukiogelea wala haipotei na tutakapopata exposure tutaacha kuogelea tutawekeza wenyewe.
 
Mimi Mkenya hapa, hili suala la bandari yenu nafuatilia kimya kimya ila nakosa kupata kuelewa nini haswa, maana kila mmoja ana hoja zake, au kasoma mkataba na kuelewa kivyake, mara bandari inauzwa, mara inakodishwa, mara ni ubia, mbona msiwe na lugha moja ambayo hata mama nitilie mtaani ataielewa?

Mnatupiana maneno hadi basi, utadhani ubishi wa Simba/Yanga wakati ni raslimali muhimu sana ya taifa......
Afadhali mkuu, The Big Nyang'au, hebu njoo tusaidie , tunauzwa huku!
 
Wakati wajinga fulani nchini Tanzania wakipigana kufa na kupona kuzuia jitihada za Serikali kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa na ufanisi ili kukamata soko la Afrika Mashariki na Kati huku Serikali ikiendelea kupata shida kutokana na wajinga hao kuendelea kusisitiza ujinga wao, mataifa yaliyokuwa yanategemea Bandari ya Dar es Salaam sasa yameanza kuchukua hatua za kuondokana na Bandari hiyo ambayo imekuwa ikisifika kwa kutokuwa na ufanisi na kuchelewesha mizigo.

Jana Marais wa Zambia na Congo wamekubaliana kutumia Bandari ya Lobito ya nchini Angola huku wakitengeneza corridor mpya ya usafirishaji ijulikanayo kama corridor ya Lobito!

Tukisema watanzania tafuteni exposure muondokane na ujinga mtuelewege jamani! Sasa endeleeni na tantalia zenu kukataa uwekezaji wa kufanya mabadiliko ya kweli bandarini huku wale wateja mliokuwa mnawategemea wakizidi kuwakimbia
View attachment 2678928
Mtu yupo Kinshasha atumie bandari ya Dar es salaam iliyopo bandari ya Hindi badala ya kutumia bandari ya Atlantic iliyo karibu zaidi atakuwa ana mtindio wa ubongo. Labda watu wa mashariki ya Congo ndiyo sahihi kutumia ya Dsm.
 
Labda tuweke sheria kwamba atakaepatikana anapiga madili bandarini ni risasi hadharani, kwani ni kikwazo katika maendeleo ya taifa. Ufanisi utakuwepo na majirani wataendekea kutumia bandari.
 
Back
Top Bottom