Zambia na Congo zaanza kutafuta njia mbadala kusafirisha mizigo yao

We mpemba hii nchi inaendeshwa kwa kodi zinazokusanywa kwa mwanainchi mmoja mmoja haitegemei bandari.
 
Kama huelewi Baki hivyo hivyo na ujinga wako..

Mara imekodishwa milele mara imeuzwa which is which?

Kukodishwa milele Kuna shida gani kama pesa nazo zinaongezeka milele hivyo hivyo?
 
wee mshenzi usituone mapumba , bandari ya lobito nayo pia ni ya DP world au ?
mbona angola wanamiliki bandari yao vizuri tu bila waarabu kuwepo .
mjinga n ww tu ulipo kudhan wanasiasa wana nia njema nasi
 
Muwe mnaelewa hoja! Hakuna anayepinga uwekezaji wala uboreshaji wa Bandari ili kuleta ufanisi!

Hiyo haihalalishi kugawa Bandari zetu na kuingia ktk mikataba ya Kimangungo!
Bandari zenu na nani? mbona lugha inatumiaka hapa kama kundi moja ndio wamiliki. Kama ni yetu sote basi hatuwezi kubaliana 100% ndio linakuja mwenye majority anaamua. Serikali itafanya kosa kubwa sana kusikiliza kelele za mitandandaoni huwezi kufanya maamuzi ya nyumba yako kwa kelele za majirani, utapoteza credibility. Hujaridhika subiri 2025 fanya maamuzi simple. Ondoa kauli ya zetu, zetu na nani. Tanzania hii kuna mali ya urithi yetu na mali yako hakuna kitu zetu. grow up usikariri maisha. Jenga achia urithi wanao usiwaaminishe wanamiliki bandari...
 
Shida ilikuwa vita vya Angola, umbali bado ni rahisi kwa zambia kutumia Lobito
 
Mkuu denning umeniwahi, nilikuwa niipandishe hii habari asubuhi hii hii. Nchi hii ina wapumbavu wengi sana na kwa kweli ni ya kuiombea kwa Mungu ipate nafuu.

Kuna watu Baba zao wameishi kwa kodi ya serikali tangu wao wanapata akili, wanakuja kuwa watu wazima wanaanza kutumia nguvu kubwa kupinga hizi biashara.

Hayati Rais Magufuli alifanya kikao cha pamoja kati yake, Kakoko na Hamza Johari pamoja na viongozi wa Zambia kuhusu mzigo wao kupitia bandari ya Dar na hayati akawahakikishia kuja kufanya hiyo biashara siku moja.

Leo wanatuona wajinga namna tunavyopoteza muda kwenye siasa za majibizano tena ya kijinga wakati biashara pana ya kusafirisha mzigo wao tukiiacha itupite.

Kutoa mzigo kutoka China na kuuleta Dar ni gharama ndogo kuliko kuutoa huko na kuupitishia bandari ya Lobito Angola na meli inabidi izunguke kule chini Durban halafu ipande juu kwenda bandarini.

Kina Mwabukusi na wanasiasa wengine wanaendelea kuwajaza watu ujinga wakati huo Angola ambaye alikuwa ni chaguo la pili la Zambia kusafirishia mizigo yake anakuja kufaidika na upumbavu wetu wa kupenda siasa za majibishano tena mengi ni upotoshaji wa watu wenye uelewa mdogo sana wa kitu wanachokiongelea.
 
Kama huelewi Baki hivyo hivyo na ujinga wako..

Mara imekodishwa milele mara imeuzwa which is which?

Kukodishwa milele Kuna shida gani kama pesa nazo zinaongezeka milele hivyo hivyo?
Kuna mijitu nchi hii yanahitaji maombi, Mimi nyumba yangu natafuta mpangaji wa milele sio wale kila miezi 6 wamehama natafuta wa milele muhimu kodo naweka mimi...
 
Mjinga ni wewe unayetetea waarabu kumilikishwa Bandari yetu milele
Wewe unayeamini kuwa waarabu wanamilikishwa bandari yetu milele sio mjinga?.

Wewe unayeelimishwa kila kukicha tena na wataalam mbalimbali wa sekta husika na bado unaamua kutokuelewa unachoelimishwa, kweli sio mjinga?.
 
Wakati mjadala huu ukiendelea bandari inafanya kazi labda mtuambie imesimamisha shughuli zake.
 
Mimi nilikuwa na biashara yangu nimeibiwa mpaka nimesema basi unakuja mwezi naona niko kama break even hakuna kitu nimepangisha mwaka wa 4 naingiza kodi tena nalipwa kwa mwaka advance wala siumizi kichwa wala kugombana na mtu, ndio serikali inaenda huko wamechoka na mambo ya Bandari kila awamu imekuja ule mfupa mgumu umewashinda. Sababu kubwa watu hawajali kuiba wala kuogopa kufukuzwa muhimu anaiba anajenga. Leo hii tukienda kufanya audit kwa kila mfanyakazi wa bandari na kuuliza mali hizi umezipata wapi kwa kipato gani tunaweza kupata mshtuko wa moyo.
 
Hata wasipokuja, bandari yetu tutaitumia kwa kuogelea!
Duh!
Umenikumbusha kina baba zangu walipokuwa wanazozana wasiuze nyumba za bibi (mama yao) pale Tambaza.
Wapo waliokuwa na mawazo kama yako eti hatuuzi hii ninnyumba ya urithi, ht ikibidi tutafugia mbuzi lkn haiuzwi
 
Wakati mjadala huu ukiendelea shughuli za bandari zimesimama? haifanyi kazi?.
Bandari kuwa na faida ni wingi wa mzigo unaopitishwa hapo.

Zambia anapoamua kutumia option ya pili ya Angola na akaiacha Tanzania ni aibu kwa waasisi wa nchi hii waliotumia nguvu kubwa kuijenga bandari. Ni aibu kwa waliojenga reli ya TAZARA huko walipolala makaburini.
 
Kabla ya huu mjadala serikali ya ccm ilishindwa kuiendesha bandari nini tatizo.
 
Mnapigia kelele eti Serikali isimpe private operator na hasa Waarabu Sasa sijui mnamaanisha nini..

Mwisho nawakumbusha tuu bila Zambia na DR Congo ,Dar Port ni tembo mweupe la sivyo tukuze sana uchumi wa ndani.
Sio port na SGR tuifanye makumbusho. Hatuna uzalishaji wowote mahindi tunauziana humuhumu ndani bidhaa zingine zinakuja kwa matukio tu soko likipatikana tu lazima tuchakachue tunakimbiwa.
 
kumbe hata wewe hujui lolote ni mbumbu kabisa.kama umeshindwa kutafsiri kiingereza rahisi kama hicho ni bora hungeandika huo uchafu wako.the shortest route but not slow performing harbour.
 
Kabla ya huu mjadala serikali ya ccm ilishindwa kuiendesha bandari nini tatizo.
TICTS wamekuwa pale kwa miaka 22, CCM hawajashindwa kuiendesha bandari.

Inakodishwa na sio vinginevyo. Zinakuja tafsiri nyingi za upotoshaji zenye malengo ya kisiasa.

Mwisho wa haya yote huwa malalamiko ya mbona bandari yetu haina tija kwenye uchumi mkuu?, Hili swali linakuwa katika mfumo wa lawama.

Ni wakati huu wa kufanya maamuzi yenye lengo la kuimarisha hali ya uchumi kwa kutumia bandari kama chanzo cha mapato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…