Ok, kumbuka pia tunayemzungumzia sio mtu binafsi bali kiongozi wachama, chama ambacho ni taasisi yenye wings tofauti tofauti, wing ya masuala ya usalama na wing ya mambo ya nje...Hizo wings zimechukua hatua gani kuishinikiza Serikali?.... juu ya haki ya mhusika?..
Nasisitiza tumia akili vizuri unapojadili mambo haya.
Lisu ni mwanachama lakini pia nimuajiriwa wa CHADEMA.
CHADEMA au CCM au chama chochote hakina wajibu wa kulinda usalama wa wanachama wake,
Jukumu hilo linabebwa na Serikali kupitia vyombo vyake vya Dola Kama Polisi.
Polisi ambao ni chombo cha serikali moja ya majukumu yake ni kulinda usalama wa Raia na Mali zao. Polisi wanalipwa mishahara Kwa kazi hiyo, na serikali inachukua Kodi Kwa Raia Kwa ajili ya kuweza kuwalinda na kuwapa Huduma zinginezo.
Lisu ni Raia wa Tanzania Kama ulivyo wewe na Mimi.
Serikali ilishindwa kumlinda akapigwa RISASI licha ya kuripoti mara kadhaa kuhusu vitisho vya kudhuriwa,
Nikiwatetea Polisi na serikali, ni ngumu Kwa serikali au polisi kulinda mtu mmoja mmoja huenda ndio maana Uhalifu unaweza kumtokea yeyote.
Sawa, Uhalifu umeshatokea, Lisu kapigwa RISASI,
Mwenye jukumu la kufanya uchunguzi na upelelezi ni serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama.
Kumbuka ni jukumu na wajibu wa serikali, sio mpaka mtu aende kuomba, uchunguzi ufanyike na waliofanya wakamatwe sheria ifuate Mkondo wake.
Sasa wewe unaleta mambo ya CHADEMA sijui viongozi, sijui blah! Blah! Hujui hata wajibu wa serikali na hii inamaanisha hujui hata wajibu wako