Zanzibar kuna Muafaka ulishafanyika pamoja na kwamba CCM miaka yote imekua ikishindwa lakini wapinzani wao wanakubali kutulia .
Zanzibar kuna katiba iliyoka wazi kuwa Tume inapaswa kuwa huru na kushirikisha vyama vyote.
Je,hayo yanafanyika ?
Zanzibar Mshindi wa pili anakua makamu . Maalim Seif alikubali na akawa makamu, je ,ni kwa nini CCM wao hawataki na wanafanya mambo ya uhalifu kwa wazi kabisa kila unafika uchaguzi.?
Je wanataka muafaka tena baada ya kuua watu wakati huko tulishatoka?
Wazanzibar na watu waliopo kwenye nchi yao na wanastahili kupewa Uhuru wa kuwachagua viongozi wao kwa mujibu wa sheria .
Tunaposema kuwa CCM ibadilike tunamanisha wakubali kuwa kile ni chama tu kama vyama vingine ndio maana ASP na TANU iliondolewa na hakuna mtu aliyepoteza maisha mana ni Jina tu kwenye usajili. Watu wanapaswa kuzingatia sheria kwa haki. Mtu akishinda atangazwe ili akishindwa kuleta matumaini aliyowaaminisha watu naye atoke kwa kura .Ndio ustarabu wa binadamu aliyestaarabika . CCM wanatufanya tuishi kama manyani huko porini bila ustarabu ,watu wanagombania mpaka kuapishana ! Mawakala tu wanavurugwa na kunyanyaswa kama watumwa !! Hapo unaona CCM wanatenda haki hivyo! ? Nani wa kuteswa na binadamu mwenzake kila siku?
Nani wa kuwakemea watesaji na wanyanyasaji kama marais Shein na JPM wamekaa kimya kuona hayo yanatendeka ?
Ni bora CCM ishindwe ili hao walioko nyuma ya pazia wanaowashauri vibaya marais wetu wakose nguvu ya kulivuruga taifa letu na sheria zake.