Tanzania ni nchi moja ya JMT, ambapo Zanzibar ni sehemu ya JMT, SMZ na Mzanzibari yoyote yuko huru kumiliki Ardhi huku kwasababu kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki Ardhi.
Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.
Mkataba huo unaitwa The Zanzibar Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Helingoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.
P