Zanzibar inachangia nini kwenye Serikali ya Muungano? Isije ikawa wanatumia Kodi za Bara

Au warudie jina lao la Tanganyika
 
huyu mama nchi itamshinda mapema kama ataendelea na huu ujinga aloanza nao
Mama ameanza vituko mapema sana.

Baada ya kauli yake nimejiuliza..awali wakati sherehe zinafanyika, ina maana upande wa Zanzibar sherehe zilikuwa zinagharamiwa na bara!?
 
Mkuu Zanzibar inachangia Jina maana hebu piga picha tu Tungeendelea kuitwa "Tanganyika" jina lenyewe linahuzunisha kabisa.
Dah mawazo mengine, inachangia jina? kwani tungeitwa Tanganyika tungepungukiwa na nini.
 
1. Kwani aliyeua tanganyika ni nani?
2. Kwani aliyeunganisha nani?
3. Kwani aliyetaka Zanzibar iendelee na mamlaka yake nani?
4. Kwani aliyekuwa kiongozi kipindi hicho nan?
Ndio maana wanasema tanganyika imevaa koti la muungano kwa maana ukiongelea Tanzania unaigusa moja kwa bara, kwasababu Tanganyika haionekani lakini Zanzibar bado inaonekana.
Rasimu ya katiba (Mzee Warioba) iliyowekwa kapuni ilikuja na mchakato wote wa kuwa na serikali 3. Lakini kwa nini ilitupwa?
 
Mtoto akililia wembe mpe hakuna haja ya kupiga ramli
 

Aliyeitupa ni yule anayedai kuwa katiba si kipaumbele chake.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Ni lazima upite kwene serikali ya muungano haya mambo akina nyerere walikuwa very technical...ila kiuhalisia sisi upande wa bara tunawanyonya zaidi wale wavisiwani
 
Ni lazima upite kwene serikali ya muungano haya mambo akina nyerere walikuwa very technical...ila kiuhalisia sisi upande wa bara tunawanyonya zaidi wale wavisiwani

Hayo ni maoni yako mkuu. Wengine sisi tunaona bara tunanyonywa sana mkuu kwenye huu utaratibu wa Muungano.
 
Wakimaliza kutawala wote wanabaki bara, no one goes back! Muungno no waste of resources.ilikuwa uroho wa madaraka
 
Wazanzibar wamebakia kwenye huu muungano kwa sababu wao ndio wanufahikaji wakuu

Leo hii muungano ukivunjika, Zanzibar hawana cha kupoteza

Wana kila kitu ila Tanganyika hatuna cha kujivunia tutaanza mwanzo kabisa kama nchi inayozaliwa upya

Tanganyika haina
-jeshi
-serikali
-mahakama
-wimbo wa taifa
-bunge
-bendera ya taifa
Zanzibar hayo mambo yote wanayo huku Tanganyika ikibaki IPO chini ya muungano

Wabara tutabaki chini ya hiki kivuli cha hili jina la TANZANIA hata kama muungano huu utafika tamati kama ilivyokuwa tangu muungano huu umeasisiwa

Hatutarudi nyuma kwenye majonzi tena ya kufanya tulichoshindwa kufanya huko nyuma
 
acha upotoshaji hakuna pato lolote linalokusanywa zanzibar halafu likaja kutumika tanganyika ...zanzibar wanakusanya mapato yao na kuyatumia wao tu

wazanzibar hawako tayari kitu chao kikawa cha muungano hata kimoja refer upatikanaji wa mafuta kwao

kusema na ukweli hili la mapato ya bara kugawanywa kwenda zanzibar limeshangaza wengi na geni kabisa halafu basi ingekuwa hata ktk mlinganyo unaolekea na uhalisia yaani zanzibar inakula 50 nzima kweli hii imekaa sawa !!!

kuna mikoa mingapi bara jamani!!! je kila mkoa ukidai pato lake lirejeshwe kwa ajili ya matumizi yake watakuwa wanakosea?!!!

yaani zanzibar anakula pato la arusha,mwanza,mbeya,kigoma n.k pato ambalo hakulichangia chochote kile !???...je hiyo mikoa ina mahitaji mangapi imejinyima ili kuchangia pato la taifa leo pato lao linagawanywa kwa mtu ambaye hana uhalali nalo !!!

hii haiko sawa hata kidogo uhalali wa zanzibar kugawiwa ungekuwepo kama anachangia 50 ya pato la muungano hata mgawanyo wake ungepaswa kuwa 50 /50 basi hata mgawanyo utakuwa 50 - 50 siyo achangie 2 then aje apewe 50 basi kila mkoa uombe mgao wake uliosawa kama ulivyochangia

hii tabia ya kubebana kwa nguvu za jasho la wengine iishie hili tu lisjirudie tena eti kwa kigezo cha koti la muungano ni bora ungepewa mkoa wowote asilimia 50 ya pato lote la taifa maana watakuwa na uhalali kwa sababu wanachangia hilo pato
 
unapotosha sana... ukweli ni kwamba zanzibar wataomba jambo lao wanalolitaka kupitia tanzania na linaporudi zanzibar si kweli kuwa tanganyika italimega kwanza then ndio liende kwa wazanzibar la hasha isipokuwa jina tu la zanzibar au tanganyika ndio yenye shida kimataifa lakini kila mmoja ataomba jambo lake kwa jina la tanzania na alichokiomba atakitumia yeye mwenyewe na si wote

kuna mwingine pia ametia chumvi kwamba mapato ya utalii zanzibar yanakusanywa na tra tanganyika na kuingizwa kwenye mapato ya bara si kweli hata kidogo
zanzibar wanakusanya kila kitu wao na kukitumia wao wenyewe kama nchi hii ni kutaka kuhalalisha hiki walichokifanya cha kugawanya mapato 50/50
 
Ni vema aseme kila upande urejeshewe kiasi cha fedha ulichochangia 🎃patamu hapooo 🎒
 
Kama hakuna TRA zanzibar inayokusanya kodi kwa ajili ya Tanganyika basi yale majengo yenu yaliyo na mabango TANZANI REVENUE AUTHORITY yaondoeni., yapo kila kona zanzibar unguja na pemba kote kila mahali mpaka bandarini na kila sehemu.
 
Wabara mpaka urojo mwaujua. Kariakoo kuna wachaga wanapika urojo
 
Tulimwona Mtikila ni kichaa wakati akiipambania Tanganyika.
Kwa kweli tunaumizwa sisi tuliopoteza nchi yetu.
Hii ni ndoa ngumu na ya upande mmoja.
Sawa na kijana ameoa amebeba jukumu la kutunza ukweni na familia yake ilhali wakwe hawana mchango kwa familia.
Muungano unaendeshwa na Tanzania huku ukihudumia Zanzibar wenye makusanyo yao na hawachangii lolote.
Muungano huu hauna faida kwa watanganyika. Unawafaidisha wazanzibari tu.

Anayebisha anyooshe mkono juu, au hata afanye kama anajikuna. Halafu alete faida moja tu ambayo mtanganyika anaipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…