DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mkuu umesomeka, unajua wabongo wengi huwa fikra zinaenda likizo mpaka matatizo yatokee ndio wanakurupuka wakati huo gharama zimeshakua kubwa!
 
mwanakijiji ahsante kwa porojo. Naamini lengo halikuwa Daraja la TZ Zanzibar ila kuonyesha uthubutu, uamuzi na kusimamia maamuzi, kutekeleza na Kufanikiwa kwa maamuzi yanayoleta maendeleo tena kwa muda mfupi. Jambo ambalo kwa maghamba limepotea. Tunahitaji serikali nyingine inayoweza tekeleza haya na sio daraja bali huduma bora na miundo mbinu ya kutosha , bila kusahau upangaji wa miji ambalo sidhani nalo linahitaji hela
 
 
For curious minds google" a potential fixed link to vancouver" for an excellent primer on the technical,socio-economic ,enviromental challenges of building such a link(ie zanzibar mainland bridge) and possible solutions.
 
$ 1.5 billion zikiwekwa kwenye fixed account with intrest rate of 12 % ni sawa na faida $ 493150 kwa siku.Daraja inabidi lizalishe kwa uchache kiwango kisichopungua $ 493150 kila siku.
Mfano gari elfu moja zikivuka kila siku kila gari itabidi kutozwa $ 493.Kazi ipo.
 
usiende mbali hivyo tunahitaji maji ya bomba kwenye vyoo vya shule za kata au zahanati za kata . Ambazo plant za kusupply kaya 190 maji safi yawe ya ziwa, mto au ya kuchimba ni usd 2,000 tu. Waulize kwa nini hawafanyi hivyo kurahisisha maisha ya wanakijiji ehhh mzee mwanakijiji
 
Daraja la kwenda wapi ndugu yangu kuna nini zanzibar cha kusafirisha kwenye daraja la matrilioni ya shilingi wakati wazanzibar wanakufa kwa malaria kwa kukosa dozi ya shilingi 1500!
 
Daraja la kwenda wapi ndugu yangu kuna nini zanzibar cha kusafirisha kwenye daraja la matrilioni ya shilingi wakati wazanzibar wanakufa kwa malaria kwa kukosa dozi ya shilingi 1500!

Kuna watu, the biggest and superior development resource in the world, kuna deep sea opportunity, kuna mafuta (Energy), kuna karafuu na kilimo, kuna utalii, Biashara kubwa na ndogo ndogo yapo mengi sana swali lako nadhani lina wakilisha kile kilichosema tupo vipofu hatuoni chochote!

La msingi ni kama hilo daraja ni muhimu wakati watoto wanakaa chini darasani na Polisi wanaishi kwa Rushwa kwasababu mishahara haiwatoshi na wanaishi kwenye mabanda na serikali haioni yote hayo.
 
Tatizo watu wanafikiria nimependekeza tuache mambo mengine yote na tujenge daraja au kabda tusiwekeze kwenye maeneo mengine ya miundo mbinu. Ninachosema bi kuwa tunaweza kabisa kujenga daraja hilo na la kigamboni na bado tukaweza kumudu mambo mengine. Kumbuka tatizo siyo fedha hata kidogo bali mipango, uongozi, na matumizi na usimamizi bora wa fedha zetu.
 

Mkuu,

Fikra za kitanzania tunafanya maamuzi kisiasa zaidi kuliko kiutawala na hilo ndio Lowassa juzi alikuwa akilikemea na kwakweli namuunga mkono. Ujenzi wa daraja linaweza kuwa moja ya development projects na linaweza kufanyika sambamba na miradi mikubwa mengine. Kila kitu kimekuwa siasa nchini hadi ufanisi unapotea.
 


yakhe! ulisikia wapi watanganyika wanalilia serikali ya mkoloni mzungu irudi atutawale , shekh weye piga kelele tu ... muarabu harudi pale mapinduzi yalikuwa ni ya kuondoa utawala wa muarabu .. mtaedelea kujiita wa oman .. wengine wa yemen , waarabu walikuja pale wakawakuta wenyeji na wakafukuzwa kuwaacha wenyeji , kwa kukusaidia tu mwisho wa siku znz haitosimama peke yake kama nchi bila tanganyika... mpo ughaibuni mnapiga kelele.. rudini znz basi muanze hizo harakati za mapinduzi ..
 
Nyie acheni kuwatafutia watu ulaji. Chai na maharage inawashinda mnafikiria maziwa na keki. kama hizo pesa zipo/zilikuwepo basi tuzipeleke kwenye elimu tuelimike daraja tujenge wenyewe sio mnazidi kuwatajirisha wageni kwa 10%. Wachina wanafanya wenyewe kwa mikono yao kwa sababu waliwekeza kwenye elimu siriaz sio kama hizi za st Kayumba!
 
MMJ ndoto nzuri, hii itaweza tokea may be karne ijayo (Mwaka 2111) sisi bye then tutakuwa tumeshakufa. Daraja la kigamboni tu limechukua miaka zaidi ya 15 linajadiliwa kwenye vikao, ndiyo juzi NSSF wanatuambia wataanza mwezi Dec.

kwa sasa watu wanafikiri kuleta mi project ya ulaji hasa kwenye uwekezaji uchwara ili watengeneze mi-hela as if wataishi duniani milele, binadamu tuna mioyo ya ajabu sana sometimes.
 
nimeipenda hiyo. hii yote kwa sababu ya tamaa ya mali kila mwenye madaraka anafikiria awe bilionea na si kuwahudumia bora wafe wote tuanze upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…