Zanzibar kupo ovyo sana. Kweli au nahitaji kueleweshwa?

Zanzibar kupo ovyo sana. Kweli au nahitaji kueleweshwa?

Zanzibar iko kwenye miji inayotambulika kuwa urithi wa Dunia, Historia ya miaka ya 1700-1800 inaakisiwa na majengo yake mengi makuu kuu. Kuwa kwenye orodha ya urithi ni wazi kuwa magofu yote yatakuwa na thamani pale hivyo, hakuna ruksa ya kuingiza usasa pale.... Labda ujengwe mji mpya seheme nyingine kama ilivyo kwa miji mingi mikongwe ya nchi za bara ulaya.
Sawa sawa... Hata ujenzi wa nyumba umegawanyika kutokana na jinsi wageni walivyokuwa wakiingia kisiwani humo.

Zanzibar ni tropical town na ujenzi wake umeendana na hali hiyo. Kwa Wazungu wa mwanzo walipenda kukaa eneo la Vuga na kujenga hapo.

Wagoa (The Goans) wao walijenga nyumba zao karibu na Kanisa Katoriki(R.C. Cathedral) Kama kawaida yao ya kutopenda kujichanganya eneo hilo lilijulika kama Goan village.

Waarabu wao walijenga majumba mengi kwa kutumia coralline limestone. Kuta za majengo yao zilikuwa ni pana, aidha nyumba hizo kuwa na giza hivi ambalo hupungua kadiri unavyoingia ndani, kwani nyumba hizo zilikuwa zina uwazi kwa ndani. Kutokana na kuwepo na nafasi chache wengi walipendelea kujenga nyumba za ghorofa.

Wahindi(The Indiani) hawa walipenda kulundikana, unaweza kukuta watu kati ya tano hadi sita wakiishi kwenye chumba kimoja kidogo na kisichokuwa na madirisha wala mwanga wa kutosha. Kutokana na tabia hii pamoja na uchafu, walijikuta wakitolewa maeneo ya Mji Mkongwe na kupelekwa Ng’ambo.

Waswahli, nyumba zao ziijengwa kwa fito pamoja na chokaa zikiwa na paa la makuti. Tatizo kubwa la nyumba hizi zilishindwa kuunganishwa na drainage system ya wakati huo. Hivyo vyoo vyao vilikuwa ni vya shimo. Hata hivyo nyumba zao zilijengwa kufuata mpango mzuri wa ukaazi, huku Mwembeladu ikiwa ni mfano kwa ujenzi wa nyumba za Waswahili wa miaka hiyo. Baadhi ya nyumba hizo walipenda kuweka bustani ndogo nyuma ya nyumba.
 
We ulishawahi kuona wapi watu wanaopenda ubaguzi, choyo roho mbaya na kulalamikalalamika bila kufanya kaz wakawa na maendeleo
 
Hivi zanzibar si moja ya mikoa ya tanganyika [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwa maoni yangu mimi binafsi, Unguja ni kisiwa kizuri sana na kinavutia. Wauache mji mkongwe ila kuwe na mji mpya mbali kidogo na mji mkongwe pawe na ofisi za serikali na majengo ya kibiashara ya watu binafsi.

Tatizo ni mji mkongwe na surrounding areas ambao ni mji mdogo sana, kutumiwa kiserikali na biashara za kibinafsi . Majengo yale, kwa kuwa ni UNESCO heritage site yangeachwa yapumue na serikali ikajenge mji wake nje kidogo ya mji mkongwe angalau 10 miles away. Wafanyabiashara nao watawafuata.

Malalmiko mengi ni neighbourhoods za Zanzibar, zipo very unplanned kama Dar ilivyo ila tofauti Zanzibar wakazi wake inaonyeesha wazi aidha hawana kipato cha kutosha au basi hawana ile nia ya kuishi mahali palipojengeka vizuri, ingawa ni watu wasfi sana. Nyumba zao ndani ni safi sana na ni watu wanaojiweka kiusafi kwa ndani. Ila nje unaweza ukaona kama kuna uchafu mwingi umezagaa kutokana na kutokuwa na tabia kama za kuwa na makaro, utaona maji ya kuparia samaki yanatupwa tu kwenye mchanga na kufyonzwa.

Kingine kilichonishangaza (Na nimefika Zanzibar mara nyingi naijua tangu 1986) ni upungufu a misikiti mikubwa yenye shule kubwa za kiislam. Yaani, Dar es salaam ina misikiti mingi mikubwa kulinganisha na miji mingi ya kiislam ukanda wa Pwani ya AFRIKA MASHARIKI. Nashangaa sana kila nikiangalia miji ya kiislam ukanda wa East Africa, hukuti misikiti mikubwa au taasisi kubwa za kiislam mijini au vitongojini kama ulivyo mji wa Dar es salaam.

Mfano mzuri wilaya ya Temeke, ingawa haipo mjini lakini ina misikiti mikubwa na taasisi kubwa za kiislam zilizojengwa na watu tu wa kawaida. Zanzibar vitongojini misikiti yake ni midogo na taasisi za kiislam hazijapenya sana vitongojini. Hilo wazanzibari mpende msipende ni jambo la kufanyia kazi ukilinganisha na wingi wa waumini Zanzibar.

Mwisho, wazanzibari wengi wapo diaspora na hupenda kujilipua, hata kurudi hawataki na hii nadhani inatokana na kutokuwa na imani na serikali ya Mapinduzi hasa kwa vijana. Serikali ya Mapinduzi sidhani kama historia yake kwa vizazi vya muda huu ni nzuri. Ni kama kuna kutokupenda nyumbani kwa vijana hasa wa unguja. Labda Serikali ya Mapinduzi ijitahidi kuwashirikisha zaidi vijana kwenye maamuzi na kuwapa vyeo vya juu vya kimaamuzi vijana hasa wilayani.

Sikubaliani na mdau Emiir kuwa majengo mazuri siyo hulka au mambo ya kiislam kwa sababu kama kuna kitu ambacho uislam umeleta dunia hii ni majengo na kasri za kifahari. Angalia miji yote ya kiislam kuanzia Muscat, Riyadh, Mecca, Basra, Qoum, Cordoba, etc.. ni miji iliyojengeka haswa ukizingatia miaka hiyo ambapo New York ilikuwa ni kijiji tu.
 
Mtoa mada unamatatizo sio bure watu wenye wadhifa wao, utajiri na wafanyabiashara na mashuhuri wanaipenda Zanzibar ni sehemu moja iko kipekee kabisa kama una hela za kutumia nenda Zanzibar Tembelea stone town na uinjoy hotel za kifahari.

inasemekana Zanzibar ni sehemu pekee ukienda msikitini unaweza kuonana na waziri, wabunge , Rpc na ukapiga swaga nao bila shida yoyote ufahari, majivuno hawana wanaishi maisha yakawaida kabisa.
Sasa Zanzibar RPC atamringia Nani wakati mkoa mzima una watu elfu nne labda!?
Ila Kwa Dar tu pekee mwenyekiti wa Kijiji Sinza anamiliki watu zaidi ya elfu 100,000/=
Zanzibar nilishamuona Jaji anapanda daladala kwenda kazini? [emoji1787][emoji1787]
Zanzibar Kuna vituko nyie. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Aisee we mtu punguza fiksi kidogo basi... dah!
Sio sound mkuu... Nilikuwepo na nimeshuhudia mwenyewe hii ishu kwenye uzinduzi wa Zahanati ya Nungwi.

Unaweza kuhisi ni fundi ujenzi anapewa chakula na kibarua wake... Anaeleta chakula mchafu kuanzia mavazi Hadi ubebaji wake.
 
Huyu kafikia Jang'ombe [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji125][emoji125][emoji125][emoji377][emoji377][emoji377]
Sasa mvuta bangi si anapewa connection na wenzake pakufikia?
 
Nimetembelea huu mji, kwa kweli ni mji ambao bado watu wamelala, migahawa ya kumulika kwa tochi vyakula havieleweki, nimeenda hadi forodhani yaani nyama za pale bei juu alafu hazina mvuto yaani rafu rafu tu.

Barabara za lami kama wamemwaga zege yaani , mainjinia sijui wameajriwa kwa kazi gani, nimehisi nimerudi Dar es Salaam ya mwaka 2000 ,or ndio mji wa kitalii labda.

Labda nipewe chimbo huenda nimeenda sehem sio lakini kwaweli ni majanga sana hapa.
Mkuu Ahsante sana kwa kuliona hili, kwa kweli nchi yetu ya Zanzibar inaendeshwa kienyeji mno, mji wa Zanzibar ndio Aibu, barabara hazina lami, mavumbi kila pahala, ujanja ujanja tu. Yaani kuendesha chombo mjini ni sawa sawa na kuendesha safina katika gharika.

Mji upo ovyo utasema hakuna serekali. Hapo Malindi kwenye mataaa kuna barabara ya bwawani ni mbovu hatari, ajabu barabara hii inatumiwa sana na Shirika la bandari lakini wameshindwa kuiboresha. Pia kuna jengo la Benki ya PBZ la ghorofa moja tu lakini tunaambiwa limetumia billion 4 , pia na wao wameshindwa kutoa milioni 200 kutengeneza hii njia ya bwawani.

Kwa ujumla mji wa Zanzibar upo ovyo kwa kweli. Decision making zinafanywa na watu incompetent ambao wanajali matumbo yao tu
 
Siyo hawapend kujionyesha tatitizo hawajielewi, ndiyo maana huwezi kumtofautisha mkuu wa mkoa, katibu mkuu wa wizara na wauza nazi sokoni, mkurugenzi wa Zec Zanzibar ana panda boti ya elfu 25000, kwenda kwenye kikao, Una zani mkurugenzi wa NEC utampandisha boat ya elfu 25000 kwenda kwenye kikao Zanzibar, kwa kifupi wa Zanzibar hawajui kutumia hela
Kwa akili hizi wabara wanashida ndio maana matumizi ya serikali ni makubwa sana na maendeleo ni sifuri
 
Mkuu Ahsante sana kwa kuliona hili, kwa kweli nchi yetu ya Zanzibar inaendeshwa kienyeji mno, mji wa Zanzibar ndio Aibu, barabara hazina lami, mavumbi kila pahala, ujanja ujanja tu. Yaani kuendesha chombo mjini ni sawa sawa na kuendesha safina katika gharika.

Mji upo ovyo utasema hakuna serekali. Hapo Malindi kwenye mataaa kuna barabara ya bwawani ni mbovu hatari, ajabu barabara hii inatumiwa sana na Shirika la bandari lakini wameshindwa kuiboresha. Pia kuna jengo la Benki ya PBZ la ghorofa moja tu lakini tunaambiwa limetumia billion 4 , pia na wao wameshindwa kutoa milioni 200 kutengeneza hii njia ya bwawani.

Kwa ujumla mji wa Zanzibar upo ovyo kwa kweli. Decision making zinafanywa na watu incompetent ambao wanajali matumbo yao tu
Tatizo wanapenda kufuga majini kila nyumba kuna fugwa jini, kingine wanahamin Sana ushirikina utakuta Mume hajaonekana nyumban siku mbili mke anaenda Kwa mganga ili amsaidie, baadala aende kutoa taarifa polisi na kwenda hospital kumtafuta , chakushangaza wanaenda kwa waganga.
 
Unaongea kama kichwani kwako kumefungwa nati badala ya ubongo. Umeshafika maeneo ya Mbweni, Mwambasa, Mazizini, ukajionea hayo maeneo yaliyopangika au hapo ulipofika ndio unaona umefika?

Kuhusu five star hotel nenda maeneo ya shamba huko Matemwe, Kiwengwa, Pwani Mchangani, Nungwi Jambiani, Paje kisha uje na mrejesho hapa.

Anayoyaongea ni ya kweli, penye ukweli tunatakiwa tuukubali.
 
Unaongea kama kichwani kwako kumefungwa nati badala ya ubongo. Umeshafika maeneo ya Mbweni, Mwambasa, Mazizini, ukajionea hayo maeneo yaliyopangika au hapo ulipofika ndio unaona umefika?

Kuhusu five star hotel nenda maeneo ya shamba huko Matemwe, Kiwengwa, Pwani Mchangani, Nungwi Jambiani, Paje kisha uje na mrejesho hapa.

Watu hawaelewi Zanzibar mji wa kihistoria. Kuna maeneo inabidi yabaki vile vile yalivyo kuendelea kuwa vivutio vya utalii.

Aende Melia, Lagema, Kendwa, Mnemba, arudi Chukwani, Mbweni Kisauni tuone kama hajabadili thread au kuifuta kabisa.

Zanzibar inategemea unataka kitu gani.
 
Wenyewe mnakili mnawanyonya Watanganyika leo mnataka kodi ya uzalendo!.

Umeme bei chee kuliko bara, aya sukari nyengine yatoka bara lakini bei hapo Unguja 1900kg.

Kina mamalishe wa darajani waliokiwa wanatuokoa mabachera menu ya jioni mmewafukuza kisa uchumi wa bluu 😂!.

Nyie watu Allah anawaona asee!.

Uchumi wa Blue my foot, Mwinyi tayari ni failure. CCM wote ni wale wale
 
Back
Top Bottom