Unayohaki kubwa juu ya kile unachochagua kuamini. Mimi kwangu moja sio muumini wa maendeleo yasiyo rafiki. Unafanya kulingana na uwezo.
Kwa hali ya uchumi wetu usafiri wa ndege ulikuwa ni dhana ngeni.. Ulipaswa kujengewa utamaduni kwanza. Pili hata kama tunayahitaji sana maendeleo hatuwezi kuyataka Leo kwa mgongo wa uhakika wa kesho ya watanzania Wa kizazi kijacho.
Unaimani kubwa kiasi gani kuwa watu milioni 55wa tanzania wanahitaji madege makubwa Leo ili waende wapi?! Hao watalii wanaokuja tanzania tunahakika kiasi gani watachagua kutumia ndege zetu kuja tanzania kisa tu zinamilikiwa na serikali?!
Kama nilivyoanza Siamini kabisa na hii dhana tukope..tuwadeprive watanzania na investment zinaweza kuongeza Tija zaidi kama kuwaongezea kipato, elimu bora na afya.. Tulete ndege kubwa kubeba watalii.. Kwa nn zisiwe ndogo ziwabebe watanzania?!
Maendeleo endelevu sio kuwa na Nyumba ya Ghorofa na mkopo wa milioni mia mbili bank.. Just because a friend will praise you.. Tutaendelea kweli kama tutaweza kuwa na kauli zetu, kujiamini hata kama hatuna hiyo International company.. Kikubwa hatuna madeni ya hovyo hovyo.. Kwa vitu ambavyo vipo bound to fail right from the start.
Lazima tuheshimu rasilimali..na mojawapo ni kuzitumia for greater good kwa kizazi hiki na kijacho. Sio kwa sifa ya kizazi hiki. SISI NI MASIKINI tukubali na tuanzie hapo.. Tutauza hii nchi kwa maamuzi mabovu ya Leo.
NB; I wud careless ..what any body else says, as long as we are respected and we are content. Bila kuwaibia wajukuu na vitukuu. Kwa ujumla tunamtazamo mmoja ila ni wapi/kipi kianze kwanza ndio tunatofautiana.