Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Tanganyika ina

1.Tanganyika inachangia kiasi gani ?
Nielimishe kwa ushahidi
2.nini maana ya neno TanZania?
3. TRA ni nini?
4.Tanganyika bado ipo?
Naomba kujuzwa
 
Usiwadanganye eti wakitaka watoke!. It's very unfortunately zile artcles of Union sio contract ni aggreement, tumeungana for life, hakuna kipengele cha kuvunja Muungano, hivyo huu muungano wetu adhimu, tutaulinda kwa gharama yoyote!.
P
Sio sahihi
Bunge likipata 2/3 ya bara na Zanzibar muungano unavunjika Tizama vizuri katiba ya sasa.
Hata kura ya maoni ya wazanzibar inaweza vunja muungano tizama katiba ya Zanzibar.

Kama mtaulinda kwa gharama yoyote hata kwa kumwaga damu huo si Muungano ni ukoloni are u proud to be colonial power ?mnapenda historia iwaandike hivyo nyinyi waafika kuwa mlitawala kimabavu nchi nyengine ya kiafrika.
 

Wasiwasi wako tu wala visingezama. Ingesaidia zaidi kuunganisha na kuwa na Muungano wa kweli.

Nothern Ireland ina watu1.8M, Wales 3M, Scotland 5M, England 55M.

Muungano wao unaendelee na hizi nchi zenye ardhi ndogo wala hazilalamiki kuhusu ardhi. Infact they encourage people to move to these countries.

Hawana ubaguzi kwenye ajira, elimu, dini zingine, ndoa etc.
 

Sheria za Vatican ambazo zinakuongoza wewe ni zile kidini (Canon and Ecclesiastical Laws), tena kwenye mambo machache kama ndoa, talaka na ubatizo wa watoto. Ukienda Vatican ndiyo utabanwa na sheria za huko.
.,....................

Hapa umekubaliana na mimi kwamba sheria za Vatican zinaniongoza.


Sasa hivyo vigezo vya dola ambavyo umeniwekea hapa, navyo umevichanganya sana. Vimetolewa na mkataba wa monte-video (The Monte-Video Convention of 1933) ambao ulitoa vigezo vya taifa au dola ambavyo ni: Permanent Population, Government, Defined Territory and Sovereignty.
..,...........
Sijajua hapa unapinga nini zaidi naona umetoa reference ya nilichosema


Sasa The Vatican haina idadi ya watu ya kudumu (Permanent Population) watu wa pale huja na kuondoka baada ya kumaliza utumishi wao na kurudi nchini kwao. Ndiyo maana nakwambia hivi, kukosekana kwa kigezo kimoja haimaanishi kwamba dola siyo huru.

.,.....,.....

Rejea case ya Machano na Wenzake iliyoamuliwa na Mahakama ya Rufaa. Vigezo vyote vinne ni sharti vitimie. Na Zanzibar ilikosa kimoja, sovereignty, na hivyo kuamuliwa siyo dola na hivyo basi Serikali ya Zanzibar haiwezi kufanyiwa uhaini.

Holly Chair/Vatican ina watu. Hakuna sheria inasema watu wawe permanent. Ni hivi, popote alipo Mkatoliki basi utawala wa Pope upo. Yaani, utawala wa Papa hauna territory maalum. Na hiyo ni exception kwenye general rule ya defined territory.


Kama kigezo ni SOVEREIGNTY, kuna nchi kama The Sovereign Military Order of Malta (SMOM) ambayo haina Sovereignty lakini bado inatambulika kama nchi na ina ushawishi mkubwa sana kimataifa.

..........😀

Sasa unasemaje Malta haina sovereignty huku unasema inatambulika kama huru?

Kutambulika kama huru ndiyo sovereignty yenyeweee
 
Northern Ireland imechanganyika, kuna wenye asili ya Britain na kuna wenye asili ya Ireland. Northern Ireland siyo taifa hilo. Taifa ni Ireland na taifa ni Britain. Scotland ni taifa na sitoshangaa kama ikipata uhuru siku zijazo. Walipiga kura ya maoni 2014 matokeo yakawa 55.3% walipinga, 44.7% walitaka.


Tanzania hata kuuzungumzia huo mnaouita muungano unaonekana kama adui sembuse kupiga kura ya maoni kuuliza je bado pande zote mbili wanautaka? Usilinganishe muungano wa UK na hili vamizi la Zanzibar alilofanya Nyerere.

Tanganyika ni artificial state huwezi kupinga. Kwa mfano Mmasai wa Tanzania na Mmasai wa Kenya ni watu wale wale ila Uingereza ilichora mstari kwenye ramani ikawatenganisha. Huwezi kusema Mmasai wa Kenya na Mmasai wa Tanzania wana tofauti lakini Mmasai wa Tanzania na Msukuma wana utamaduni mmoja.

Artificial states huwa ni rahisi kusambaratika. Angalia nchi kama Syria, angalia Iraq, hata Marekani ilikuwa karibu kusambaratika, walishapigana vita ya wenyewe kwa wenyewe wakauwana watu zaidi ya milioni 1


Wewe binafsi uko tayari Zanzibar ijitoe kwenye huo unaouita muungano lakini CCM haikubali na wapo tayari kuulinda kwa gharama yoyote. Wako tayari kumwaga damu, kufunga watu, kufilisika ili kuulinda huo unaouita muungano. Sera hiyo haiwezi kuendelea siku zote.
 
Historia ya Tanganyika ni kuanza kuwa koloni la Uingereza 1922, kupata uhuru 1961, na kuuliwa na mwaka 1964. Nje ya hapo hakuna Tanganyika wala haina historia. Ni sehemu tuu Mwingereza alichora mstari kwenye ramani akapaita Tanganyika. Siyo taifa hilo.
 

Nimesema Zanzibar ni taifa. Zanzibar is a nation. Sijachanganya chochote na maana ya taifa/nation nimeshaiweka. Zanzibar ilipovamiwa na Nyerere ilipoteza sovereignity, ilipoteza uhuru ila haijapoteza utaifa.

Tanganyika huwezi kuita taifa. Haikuwa na hadhi hiyo ukifuata maana ya utaifa. Ilikuwa ni nchi bandia (artificial state) iliyoundwa na Uingereza na ikavunjwa au kuuliwa na Nyerere. Huwezi kulinganisha Zanzibar na Tanganyika hata siku moja.
 
Hii siyo kweli. Zanzibar haiwezi kwenda kinyume na katiba ya JMT. Mfano mzuri ni Nyerere kupinga Zanzibar kujiunga na
Organisation of Islamic Cooperation (OIC). Haya ni makubaliano ya kimataifa ambayo Wazanzibari walitegemea yatasaidia kuinua uchumi. Sasa sovereignity gani hiyo?
 
Mkuu Bepari2020, kwenye mijadala ya kuhusu maslahi ya Taifa kama hoja hii, ni vema tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu kwa kwanza kuukubali ukweli uliopo hata kama hatukubaliani nao .
Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar uliounda Tanzania, ni kitu ambacho kipo na kina exist, hivyo huwezi kuita "huo mnaouita Muungano" as if ni kitu ambacho hakipo ila kinaitwa tuu!. Hakuna huo mnaouita Muungano, hatuuiti Muungano, bali Muungano upo una exist.

Pili waasisi wa Muungano, Nyerere na Karume, waheshimiwe, usianze kumyooshea kidole mmoja na kumuita kwa majina mabaya kama "hili vamizi la Zanzibar alilofanya Nyerere".

Muungano wetu adhimu sio vamizi!. The Initiator wa Muungano ni Karume ndio alikuja bara kumuomba Nyerere ulinzi wa kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, dhidi ya manowari za Uingereza zilizokuwa zimetia nanga Mombasa tayari kwa kuja kuivamia Zanzibar, kuigomboa na kumrejesha Sultan aliyepinduliwa.

Ndipo Nyerere akapendekeza tuungane, Karume akakubali pale pale "tuungane, wewe rais, mimi Makamo". Usimtwishe Nyerere uzushi wa uvamizi!. Zile story za Kipumbwi ni hadithi tuu za uongo na ukweli.

Tuujadili Muungano in good faith kuwa una kero ambazo zimeendelea kutatuliwa na mwisho wa siku kero zote zitaondoshwa, tutakuwa na Muungano shwari bila kero ila pia kama ilivyo kwenye penzi, mahasidi hawakosekani hivyo tunaiendeleza nadhiri zote mbili, kwa Zanzibar "Naapa na naahidi, Mbele ya Mungu, Mapinduzi nitakulinda mpaka kifo". Na kwa JMT, "Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote".
P
 
Kwani kilichoungana na Tanganyika ni 'dola la Zanzibar', 'nchi ya Zanzibar' , 'serikali ya Zanzibar' au 'taifa la Zanzibar'?
 
😀 Nimeshangazwa na aya👆 yako ya mwisho.

Naona unaandika unachotaka kusikia na siyo kilichopo.

Katika Muunguno, Jamhuri ya Muunguno wa Tanzania ndiyo the only sovereign State (dola huru) linalosaini mikataba ya Kimataifa.

Zanzibar siyo sovereign State since 1964. Haina sovereignty.

NB:Ninasisitiza google na usome Kesi ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania baina ya Machano Hamis and Others v. Republic, ambapo Wahe. Majaji walifanya utafiti wa kina kirefu, na kuelezea kwa undani kuhusu dhana nzima ya uraia, dola huru na uhaini.

Hivi vitu vipo kisheria, na ukitoa hoja bila rejea ya sheria na principles ni kosa. You're actually not with me(us).
 
1.Tanganyika inachangia kiasi gani ?
Nielimishe kwa ushahidi
2.nini maana ya neno TanZania?
3. TRA ni nini?
4.Tanganyika bado ipo?
Naomba kujuzwa
Bandiko lililotangulia nimesisitiza hili jambo tulijadili kwa kuwa wakweli na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa.
1. Kwanza Tanganyika haipo, kilichopo ni Tanzania Bara na Tanzania Visiwani. Mpaka sasa gharama zote za kuendesha Muungano zinagharimiwa na upande mmoja tuu wa Muungano, na hii ni kero inayoendelea kushughulikiwa, Tume ya pamoja ya fedha imeishaundwa, kinachoendelea ni Establishment ya gharama za Muungano, zikiisha patikana , Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar zinachangia kwa uwiano ule ule, wa 95.5%/4.5%.
maswali No. 2, 3 siyajibu. Swali la 4, nimeisha lijibu.
P
 
Kwani Zanzibar inayo history ipi zaidi ya ukoloni huo wa mwarabu ? Mataifa yetu haya ya Africa kwa sehemu kubwa , waliishi jamii za watu waliokuepo kipindi hicho wakizungumza lugha zao na tamaduni zao, Zanzibarikiwemo .

Ramani zao, na serikali zao zimechorwa na wakoloni. Zanzibar ni visiwa pembezoni mwa Tanganyika huwezi kwepa hilo. Kikubwa mna haki ya kujiendeshea mambo yenu kama ilivyo Comoros, Seashells, Madagascar nk. Hili la muungano wa kinyonyaji hapana. Tanganyika iacheni na uwema wake wa kimshumaa
 
Unajikweza mno na Zanzibar yako. Ambayo hata asili ya jina lake ni wakoloni wenu wa ki Arabs . Huu utaifa unayoipa zanzibar kuinyima Tanganyika umeitoa wapi ?!. Bila Tanganyika, Zanzibar is nothing. Bahati mbaya kwa Tanganyika na nzuri Zanzibar ni kukuta viongozi wa Tanganyika wasiojielewa . Wenye mapenzi na jina Tanzania kuliko nchi yao
 
Mkuu Bepari2020, naomba nikurejeshe kwenye historia kwa kifupi
1. Naanza na Physical Geography da Formation ya Visiwa vyote vya bahari ya Hindi vilikuwa sehemu ya nchi kavu, vikamegeka, vikazungukwa na maji. Hivyo Zanzibar, Pemba Mafia ilikuwa ni sehemu ya Bara. Uthibitisho wa hoja hii ni mchoro huu
2. Visiwa vya Zanzibar vilikuwa ni sehemu ya bara miaka milioni nyuma!, vikamegeka na eneo la kati likasombwa na mmomonyoko!,
3. Baada ya miaka mingi watu wa bara ndio wakaazi asili wa visiwa vya Zanzibar na Pemba, simulizi za kale za Fumo Liongo Karne 8 na Ibin Batuta karne ya 12 zilieleza. Kiongozi wao aliitwa Mwinyi Mkuu.
4. Karne ya 15, Mreno Vasco Da Gama alipopita ndipo akapeleka Ureno sifa ya visiwa vya Zanzibar na Pemba.
5. Karne ya 16, Ureno ikaivamia Zanzibar, ndipo mtawala wa asili wa Zanzibar, MwinyiMkuu kuwaomba Waarabu wa Oman wamsaidie kuwatimua Wareno.
6. Baada ya kazi ya kuwatimua Wareno kukamimika, Karne ya 17, hakuna anayekijua kilichomkuta Mwinyimkuu maana hakijaandikwa popote, ila mara ghafla mwaka 1734, Sultan Sayyed Said, akaihamisha Sultanet yake kutoka Oman na kuihamishia Zanzibar kwa
kuvivamia visiwa hivyo na kuvitwaa as if havina wenyewe, wakakulia, wakazaliana, wakalowea na sasa baadhi yao wameanza kujisahau kwa kudhania visiwa hivyo ni mali yao ilhali wao ni watu wa kuja tuu!.
7. Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884, ukamtambua rasmi Sultan wa Zanzibar kama mtawala na mmiliki halali wa visiwa vya Zanzibar na akapewa a 10 miles za costal stip ya Bara ilikuwa chini ya himaya ya Sultan wa Zanzibar.
8. Tanganyika ilikuwa koloni la Ujerumani, Kenya ilikuwa Koloni la Uingereza, nchi hizi zote mbili hazikuwa na access ya bahari kwasababu a 10 miles ya costal stipe ya pwani yote ya Africa Mashariki ilikuwa chini ya himaya ya Sultan, ila Zanzibar ilikuwa chini ya uangalizi wa Uingereza, ndipo mwaka 1890, Waingereza na Wajerumani
wakaingia mkataba, wa Hellingoland, (The Zanzibar Treaty) Sultan wa Zanzibar aziachie zile 10 miles kwa matumizi ya German East Africa.
9. Tarehe 10 Desemba, 1963, Uingereza ikatoa uhuru wa bandia kwa Zanzibar kuendelea kuwa chini Sultan na serikali kibaraka wa Sultan.
10. Ndipo tarehe 12 January 1964 wanaume wakaingia kazini wakafanya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya 1964, vilirudisha heshima ya visiwa hiyo iliyoporwa na madhalimu wale na muungano ukavirudisha visiwa hivyo kwa wenyewe halisi.

Mapinduzi Daima!
Muungano Udumishwe!
Mungu ibariki Tanzania.

P.
 
Watu waliofika Zanzibar 1734 kwa maneno yako Unawaita watu wa kuja tu Yaani ilipofika 1964 waliokua na miaka 230.
.tukiaza hivyo hata wewe usikute ni Mrundi au Mnubi wa central Africa
Kwa taarifa tu sultan Jamshid mama yake ni Mmanyema.
Alie kuwa waziri mkuu aliepinduliwa ni Mpemba wa asili.
Mgeni ni Okello alizaliwa kukulia Uganda 🇺🇬 na kuja zanzibar kuuwa wenyeji na kurudi kwao.
 



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…