Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Huyu ana nia mbaya na kuwachonganisha Wazanzibar tu, kauli zake zote ni za ovyo kwa wazanzibar sio za kuunganisha ni za kuwagawa ili aendelee kuwatawala.
That's right. Watu wanakamatwa kwa madai ya kuchonganisha wananchi na serikali yao. Okay.

Rais anawaambia watu Jecha apewe tuzo wakati 50% (let's just assume uchaguzi was a tie), 50% ya Wanzanzibari wanaamini Jecha hakuwatendea haki. Sasa hawa raia, nusu ya population, kulikuwa na haja gani kuwachoma vidole machoni kwa kuwakumbusha masuala ya Jecha eti apewe tuzo?

Hapo ni nani anachochea watu wamchukie Magufuli au waichukie Serikali, kama sio yeye Rais?
 
DUH!! LOWASA INABIDI AMSHUKURU MUNGU ANGEKIONA CHA MTEMA KUNI!
 
Hahaha wengi mtateseka lakini mtakuja kumbuka baadae aina hii ya uongozi. Ukitaka kujua vizuri uliza Rwanda walifikaje hapo ndani ya kipindi kifupi. walihangaika kwa kipindi fulani kwa shida lakini nadhani wako sasa kwenye mteremko sasa. Tusipoangalia watatupita wakati sisi ni wakongwe kupita nchi zote hizi zinazotuzunguka. Ni aibuuuu

Anateseka magufuli sio mimi atasimama kila jukwaa kuongea fyoko fyoko huku uchumi unaporomoka akijistukia miaka 5 hiyo over kwa hiyo rwanda ndo rol model wa tz? Kagame nae alidili na wapinzani kujakustuka miaka inakwenda mwisho wa siku anajiongezea miaka ya utawala kwa kuipindua katiba na kujiweka rais wa milele kwa kuwa muda wa ahad aliotoa kwa raia ulikwisha
 
Nik

Nikupe mfano mmoja tu aliwahi kusema nini kuhusu meya wa Dar pale CCM walipotaka kufanya yao?
Huo siyo mfano maana hakukuwa na njia ya kupenya kwani hesabu hazidanganyi na hata huo uchaguzi wangeenda kuufanyia marekani lazima ukawa wangeshinda yaani ni sawa na kutabiri mvua kunyesha kipindi cha masika
 
Ok,shein kafundwa na kufundika
Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshangaa Rais wa Zanzibar kuwa anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekuwa rahisi hivyo.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.
 
"Kupatwa kwa jua ni ishara ya Mungu kuukubali uongozi huu" - Mzee wa kimila Mbeya.
 
Huo siyo mfano maana hakukuwa na njia ya kupenya kwani hesabu hazidanganyi na hata huo uchaguzi wangeenda kuufanyia marekani lazima ukawa wangeshinda yaani ni sawa na kutabiri mvua kunyesha kipindi cha masika
Ni kweli mkuu aliona wanapoteza muda tu, ndio maana alisema wakubali kushindwa.
 
Nimesikiliza hotuba ya Rais ya JPM akimshangaa Rais wa Zanzibar kuwa anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekuwa rahisi hivyo.

Nimejiuliza maswali mengi sana lakini mojawapo likawa ni Je stahiki za Maalim Seif ni za hisani ya rais aliyeko madarakani au ni matakwa ya kisheria/kikatiba?

Na je kama ni matakwa ya kikatiba; JPM anamanisha kwamba Shein avunje katiba kwa kutosaini stahiki hizo? Ama kweli safari ndo imeanza.

Anayevunja maagizo ya mwenyezi mungu anayetuagiza tusalimiane na kuheshimu mamlaka humshangai unakimbilia kumshangaa anayevunja katiba iliyotungwa na binadamu?
Kulikuwa na hekma kubwa sana mwenyezi mungu alipotuagiza tuheshimu mamlaka,kumbuka hapa mwenyezi mungu hakuweka condition kwamba mamlaka unayotakiwa kuiheshimu ni ile unayoikubali tu,ujumbe hapo ni mmoja tu,mpe heshima anayestahili kuheshimiwa hata kama hapendi na hata kama wewe hupendi,hiyo ni kwa faida yako wewe mwenyewe...ukijidai huamini hili laana zitakapoanza kukuandama usishangae na kuanza kusingizia katiba,kama yeye ni hodari wa katiba kwani katiba inaruhusu kumdhalilisha mkuu wa nchi?ukijidai mtu wa timing ujue watu wenye mipango ya kichwa wapo pia.
 
mzee wa visasi na kukomoa. kumbe in kweli alichepusha barabara kuwakomoa watu huko geita
 
Style ya kikoloni. "Wagawe uwatawale" No wonder Afrika hatuendelei viongozi wenyewe ndio kama hawa. Anajidai kuwambia wazanzibari waungane halafu anawachochea. Usanii.
 
Ninapatwa na mashaka mengi kuwa pengine kuna wakati bob anakuwa sio yeye yaani akili yake inapata intruders. .na hili linasemwasemwa

Hisije ikawa wanamloga wanamvuluga akili Ili waliopita waonekane bora, maghufuli anachemsha big time
 
Style ya kikoloni. "Wagawe uwatawale" No wonder Afrika hatuendelei viongozi wenyewe ndio kama hawa. Anajidai kuwambia wazanzibari waungane halafu anawachochea. Usanii.

Hii ni hatari kwa ustawi wa Taifa letu
 
kwa hili simuungi mkono rais kamwe. rais hapaswi kuwatendea tofauti wale wasiompenda. rais akumbuke yeye ni rais wa wote. pia yeye ni nembo ya taifa letu na anapaswa kutuunganisha wote....
 
Hisije ikawa wanamloga wanamvuluga akili Ili waliopita waonekane bora, maghufuli anachemsha big time
Pengine engine inahitaji overhaul kwakuwa nikiangalia radiator haina shida au pengine ni waterpump[emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom