Katika imani ya dini ya kiislam imekatazwa kabisa kulipiza ubaya kwa ubaya, Ni dhambi kulipiza kisasi kwa mtu ambaye unahisi kua hajakutendea jema.Katika kitabu kitukufu cha Quran inatamkwa kua ni mwiko kabisa kulipa kusasi.Sijui vitabu vingine vinasemaje katika hilo lakini naamini sio jambo njema na haviruhusu hali hiyo.
Inaruhusiwa kutompa mkono mtu ambaye unahisi amekiuka maamrisho ya Mwenyezi Mungu,na ni mtu ambaye amejiandaa kuitia mikono yako katika Shari! Si kosa kukataa kumpa mkono yeyote ambaye wewe unahisi anakula haramu huku akijua kua haramu ni kosa.
Ikumbukwe kua Suala la kumhudumia Maalim Seif sio la Dkt Shein wala Rais Magufuli bali ni utaratibu wa kikatiba. Seifu analazimika kukubali kuhudumiwa na kinachotokana na katiba ya wananchi wa Zanzibar, Dkt Shein naye analazimishwa na katiba kufanya hivyo maana pengine kwa nafsi yake asingekubali. Anayemtunza Maalim Seif kama waziri kiongozi na Makam wa Rais mustaafu ni Wananchi wa Zanzibar na sio Dkt Shein.
Kwahiyo kusikiliza maneno aliyoyasema Rais Magufuli tutapandikiziana mbegu za ubaguzi,Chuki na kuendelea kusababisha utengano katika jamii. Dkt Shein anatakiwa kuangalia imani yake inasemaje na sio misukumo ya kisiasa.Sisi sote ni ndugu, taifa ni moja tuepuke kauli za kutubagua.