Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Suala siyo imani ya Shein kutomruhusu kufanya anachotaka baba J, bali ni matakwa ya katiba na utaratibu wa utumishi. Hata kama Shein angekuwa hana imani wala siyo mfuasi wa dini yoyote bado anawajibika kutekeleza suala la malipo au mapato ya Self.
Utaratibu wa nchi katika hili suala ndiyo wenye uzito siyo imani ya Rais.
 
Lowassa alikupa mkono wa salamu kukufundisha kunyoosha moyo kwa maadui zako, Maalimu alimnyima mkono Shein kumfundisha kua unafiki ni dhambi kubwa katika uislamu.

Afya na uzima vinatoka kwa Mungu.

NB: uchochezi ni kumlipa Lowasa mafao yake kwa mujibu wa sheria na kuwataka nchi jirani wavunje sheria ili wamnyime Maalim stahiki zake.
 
mm nataka ccm itawale milele cion namna nyingine kwan hata CDM wakiingia (ILa haitatokea) watafanyanin
 
w
Katika imani ya dini ya kiislam imekatazwa kabisa kulipiza ubaya kwa ubaya, Ni dhambi kulipiza kisasi kwa mtu ambaye unahisi kua hajakutendea jema.Katika kitabu kitukufu cha Quran inatamkwa kua ni mwiko kabisa kulipa kusasi.Sijui vitabu vingine vinasemaje katika hilo lakini naamini sio jambo njema na haviruhusu hali hiyo.


Inaruhusiwa kutompa mkono mtu ambaye unahisi amekiuka maamrisho ya Mwenyezi Mungu,na ni mtu ambaye amejiandaa kuitia mikono yako katika Shari! Si kosa kukataa kumpa mkono yeyote ambaye wewe unahisi anakula haramu huku akijua kua haramu ni kosa.


Ikumbukwe kua Suala la kumhudumia Maalim Seif sio la Dkt Shein wala Rais Magufuli bali ni utaratibu wa kikatiba. Seifu analazimika kukubali kuhudumiwa na kinachotokana na katiba ya wananchi wa Zanzibar, Dkt Shein naye analazimishwa na katiba kufanya hivyo maana pengine kwa nafsi yake asingekubali.Anayemtunza Maalim Seif kama waziri kiongozi na Makam wa Rais mustaafu ni Wananchi wa Zanzibar na sio Dkt Shein.


Kwahiyo kusikiliza maneno aliyoyasema Rais Magufuli tutapandikiziana mbegu za ubaguzi,Chuki na kuendelea kusababisha utengano katika jamii. Dkt Shein anatakiwa kuangalia imani yake inasemaje na sio misukumo ya kisiasa.Sisi sote ni ndugu, taifa ni moja tuepuke kauli za kutubagua.


Kwa hiyo imani ya Seif Sharif inamtaka kukataa salam za muislam mwenzie?
 
Nakumbuka wosia wa baba wa Taifa, ni kweli nchi inaongozwa na watu na watu wanaongozwa na sheria ikiwemo katiba nchi.
Na ndiyo maana tuna muapisha kwa mujibu wa sheria na imani ya dini yake. Inasikitisha sana issue ya nchi inachukuliwa maamuzi kwa jinsi mtu anavyojisikia(utashi wake).
Kwa style hii mbona makosa yatakuwa kuwa kibao.
Swali la msingi hapa, hivi tunajenga nchi au tunaibomoa nchi?
 
Kauli zako zinaonekana zina harufu ya utovu wa maadili, hivyo judgement zako zina msukumo wa utukutu tu sio tafakar ya hekima. Kaa pemben
Ah nimeuliza tu. Kuna uhuiano gani kati ya kushikana mikono na uendeshaji wa nchi? Haki za Seif zipo kisheria au ni hisani tu kutoka kwa mtu?
Kuna sharia gani ya nchi inayosema Rais alazima ashikwe mkono kwa kusaliminiana?
 
Hiyo ni moja ya mikutano ya Siasa maana hapo wanejaaa CCM tu je waliweza kupata kibali mbona Chadema wanakataliwa??
 
Mhh i dont want to beleive this coming from our beloved president..
 
Sikuamini nilipoambiwa ila hii video clip imenithibitishia.
 
Halafu inakuja mijitu type ya kina mkijiji na kuanza kunanga upande wa pili. Unaanzaje kutetea hali kama hii?
 
Nyie mna matatizo sana. Yaani Maalim Seif afanye ujinga kisha aachwe tu kwa vile ana haki ya kupokea mafao?
Sawa na wewe unaona sawa sheria zivunjwe kirejareja hovyo!! Kwani Magu hana namna nyingine ya kushughulikia migogoro badala ya kutoka povu kama siye?!! Inamuharibia huo siyo urais
 
Tumuombee Mh.Rais kama anavyosisitiza tumuombee.Anatambua matatizo yake tumuombee.....
 
Tumuombee Mh.Rais kama anavyosisitiza tumuombee.Anatambua matatizo yake tumuombee.....
 
Tumuombee Mh.Rais kama anavyosisitiza tumuombee.Anatambua matatizo yake tumuombee.....
 
Tumuombee Mh.Rais kama anavyosisitiza tumuombee.Anatambua matatizo yake tumuombee.....
 
Back
Top Bottom