TANZIA Zanzibar: Salim Turky, Mwanasiasa Mkongwe na Mgombea Jimbo la Mpendae Zanzibar, afariki dunia

TANZIA Zanzibar: Salim Turky, Mwanasiasa Mkongwe na Mgombea Jimbo la Mpendae Zanzibar, afariki dunia

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2014
Posts
1,443
Reaction score
2,643
Mwanasiasa mkongwe na mfanyabiashara maarufu Turk wa Zanzibar afariki dunia.

===

Mheshimiwa Salim Hassan Abdullah Turky, afariki dunia usiku huu akiwa hospitali ya Tasakhta global chanzo cha kifo chake inadaiwa kuwa aliugua ghafla. Swala ya maiti itafanyika leo Alasiri September 15 katika msikiti wa Othman Maalim na baada ya hapo atazikwa Fumba, Zanzibar.


Salim Turky alikuwa mfanyabiashara maarufu Zanzibar na mbunge wa jimbo la Mpendae tangu 2010, alizaliwa February 11, 1963. Mpaka anafariki alikuwa mwenyekiti wa makampuni ya Turky ambapo chini yake yalikuwa makampuni 12 yanayoendesha biashara zake Tanzania Bara, Zanzibar na visiwa vya Comoro.

Baadhi ya makampuni hayo yanajumuisha hoteli ya Golden Tulip, hospitali kubwa ya Tasakhtaa Zanzibar, pia ilijihusisha na biashara ya cement, Nitak communications, vyakula na mafuta.

Turks Group iliazishwa mwaka 1978 kama duka la nguo na ndugu wa familia moja ambao ni Salim, Murtadha na marehemu Yunus pamoja na baba yao, Hassan Turky na miaka 40 baadae wakalibadilisha kuwa moja ya makampuni yanayoongoza Tanzania.

Mwaka 2017 Lissu aliposhambuliwa kwa risasi, Turky alitafuta ndege iliyompeleka Lissu Nairobi na kuwa mdhamana wa deni la kukodi ndege iliyokuwa inamilikiwa na FlyghtLink ambao ni jamaa zake katika biashara.

Zaidi, soma:

= > Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

= > Salim Hassan Turky: CHADEMA walilipia gharama za Ndege iliyomsafirisha Lissu



1600119044432.png
 
Mgombea wa ubunge wa jimbo la Mpendae kupitia CCM ndugu salim Turky afariki dunia.
_20200914_224716.JPG

Chanzo: Account ya Maulid Kitenge ya Instagram
 

Attachments

  • IMG_20200914_232032.jpg
    IMG_20200914_232032.jpg
    57.4 KB · Views: 4
Ndiye aliyewezesha kupatikana kwa Ndege iliyompeleka Lissu Nairobi Septemba 7, 2017 kwa sharti la mali kauli.

Alisema hivi wakati wa purukshani za kutafuta ndege
“Tusifanye tukio la Tundu Lissu kuwa la siasa. Mimi binafsi tukio zima la mbunge mwenzangu limenisikitisha sana limenisononesha sana. Nikiwa kama kamishna wa Bunge lakini pia ni binadamu kuna kuzaliwa na kufa,”amesema.
.


Mwenyezi Mungu amlipe malipo anayostahili na amsitiri katika makazi anayostahili!.
 
Back
Top Bottom