TANZIA Zanzibar: Salim Turky, Mwanasiasa Mkongwe na Mgombea Jimbo la Mpendae Zanzibar, afariki dunia

TANZIA Zanzibar: Salim Turky, Mwanasiasa Mkongwe na Mgombea Jimbo la Mpendae Zanzibar, afariki dunia

Mambo mengine mngewaelewa chadema mngewapiga mawe akina Mbowe. Wana CCM walitoa ndege kumuwahisha Lissu Nairobi, Mbowe na genge lake wakawa wanagombea kukaa Nairobi ili walipwe posho kukaa na mgonjwa Hadi Mke wa Lissu akakasirika.
Leo Turky kafariki Siri zinawekwa hadharani.

Wewe ndo unajua Leo kuhusu Turky kusaidia kupatikana kwa ndege ya kumpeleka Lissu Nairobi?

Sasa mnajifanya GT wa nini kumbe hata taarifa kama hizi hamna? Tafuta nyuzi humu JF kuhusu safari ya Lissu maana kipindi hicho wanaCCM wenzio kina YEHODAYA walileta uzushi kuwa CCM ndo wamelipia ndege hadi Mh. Turky akatoa ufafanuzi wa Ankara ya malipo iliyolipwa na CHADEMA.

Si wanaCCM wote waliofurahishwa na ushenzi uliofanywa na serikali yao kipindi cha shambulizi lile, hata humu Jingalao, Gentamycin na Johnthebapst walikemea kwa nguvu zote.

Hata Pasco kabla hajakabidhi busara kwa Polepole alikemea sana shambulizi lile kabla ya kuwa shabiki.
 
Innalillah...

Ni hivi Majuzi Pale Uwanjani Zenji Alikuwepo Na Uso Bashasha Kwenye Ufunguzi Wa Kampeni wa dokta Mwinyi...

Duniani si nyumbani kwetu...Tutendeni Wema Jama!!


Hapo hapo UWANJANI !!!!!!!?????
 
Lissu aliposhambuliwa Watanzania wengi (wakiwemo CCM, CDM, CUF, ACT, wasio na vyama ,nk, akina Ndugai, Tulia, Ummy, Turky, nk) wali-react naturally kibinadamu kama binadamu mwadilifu anavyo-react kwa matukio ya nmana hiyo: walisikitika na kila mmoja akitafuta jinsi gani ya kuokoa maisha ya mhanga huyo! Ilikuwa ni baada ya siku chache bosi wao alipoonesha bila kificho kuwa hakufurahia kunusurika kwa mtu huyo, ndipo walipoanza nao kulazimisha moyo wa kishetani (ili wasipoteze ulaji wao) hadi kufikia kumfanyia dhihaka na hatimaye kumvua ubunge wake. Kumbuka kuwa ni Bw. Nyalandu mwana CCM pekee aliyesema liwalo naliwe nitaendelea kuonesha kujali na kulaani udhalimu huu, na matokeo yake ilibidi aondoke CCM!! Duniani kuna binadamu wanyama, ambao kila Jumapili au Ijumaa hutaka public iwaone kuwa ni watu wa Mungu lakini ni wanyama, ni wanyama, ni wanyama. Huwa natamani Mungu awape adhabu wakiwa bado hapa hapa duniani.
Kweli kabisa mkuu, ni Magufuli aliyesababisha hadi Wabunge wakazuiwa kwenda Nairobi kumwona mgonjwa na wengine waliokwenda Kijenge kumuona Lema wakalazimika kujiuzulu uenyekiti wa Kamati za Bunge. Samia kipindi hicho alikuwa bado binadamu alikwenda Nairobi hospitali akiwa kwenye ziara ya kikazi, kabla ya siku hizi kuingiwa na Ushetani hadi kugeuka Izraili wa "Risasi 3".
 
Mkuu Unapenda Conspiracy theories eee?
Mzee Kolimba aliposhika kile kipaza sauti alikuwa akiishiwa nguvu mpaka...., tena ...mwisho wa siku ikabainika kwamba Mzee Mangula alilishwa sumu!! Nadhani hizo zote ni conspiracy theories shehe.

Wanaccm hawaachiani maji ya kunywa mezani - Kikwete
Na hawawapendi watu wakweli na ukweli wenyewe
 
RIP kiongozi. Naona waungwana wanashadidia kukodisha ndege ya kumpeleka Lissu Nairobi 2017, kama kazi kubwa aliyofanya wakati wa uhai wake.
Kama Mzee Mbowe Senior Aikaeli alivyo mpa nauli Kambarage kutuletea Uhuru UN hivyo na huyu ameleta ukombozi kupitia The great Lisu
 
Innalillah...

Ni hivi Majuzi Pale Uwanjani Zenji Alikuwepo Na Uso Bashasha Kwenye Ufunguzi Wa Kampeni wa dokta Mwinyi...

Duniani si nyumbani kwetu...Tutendeni Wema Jama!!
Kwa imani na matendo, wako wanaojidhani wataishi milele ama bila wao wengine hawawezi ishi. Allah amrehemu Salim Turky na wengineo wenye haki waliotutangulia.
 
Back
Top Bottom