Zanzibar: Simai Mohamed Said, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale ajiuzulu siku mbili baada ya kutangaza uhaba wa pombe kwenye hoteli na migahawa

Amechukua uamuzi wa haraka ushauri mtu huwezi kujiuzulu kisa watu wa nchi nyingine,mbona dubai unaambiwa ujisitiri??
 
Viongozi kujiuzulu zenji rahisi maana hawana makuu hawali mastarehe wao niwashika dini,wala urojo,gahawa na visheti. Huku bara mtu hajiuzulu ng'oo atakubalije kujiuzulu akose rushwa,pombe,mademu,makuku choma,malive band,mandinga,majumba hawawezi kujiuzulu kiboya
 
Habari aina uhusiano wowote na Zanzibar kuzuia pombe, wala imani yake kuhusu pombe kama sababu ya waziri kujiudhuru.
kadri siku zinavyokwenda mbele humu ndani ndio nazidi kujifunza ya kwamba watanzania bara walio wengi wanapenda kuchangia habari zinazohusu zanzibar bila ya uelewa wa jambo husika.

huyo Simai mwenyewe kwenye mgahawa wake anauza pombe halafu eti ajiuzulu kwa sababu dini yake inakataza biashara ya pombe.

ni ujinga
 
Huu ni ukweli mchungu,viongozi wengi ni hedonistic in nature,they may have positive change to accomplish but with time they're all consumed in fleeting stuff and forget what's it's all about.

Ila siwalaumu sana umaskini waliotokea ni trauma tosha kwao, so the only thing they know is to prove Kwa ndugu zao,mashangazi na marafiki wao kua they made it. And the only thing they should prove it is to accumulate as many resources as possible Ili wasichekwe na wananchi.

Nchi hii ukiwa mzalendo na hutaki makuu na una nafasi unachekwa kuanzia ndugu zako mpaka paka wako wanyumbani. Umaskini mbaya sana wazee
 
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Simai Mohamed Said ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo usiku...
Kwani Zanzibar hairuhusiwi kuuza pombe?

Mbona mimi niligonga Safari Lager hapo Stone Town halafu nikagonga Scotch Whisky restaurant Nungwi?
 
Itakumbukwa kuwa wiki iliyopita ilitoka habari kwamba kuna uhaba wa pombe katika hoteli za kitalii visiwani zanzibar. Sasa inasemekana jambo lile hakulipenda Mh. Rais wa zanzibar Dr. Hussein Ali Mwinyi kiasi kwamba mjadala ulizuka na kampuni za nje zikapewa kandarasi ya kuleta pombe visiwani.

Bodi ya vileo zanzibar haikua pamoja na Mh waziri ambae alipendelea kandarasi hiyo kupewa makampuni ya ndani ya nchi.kwahiyo kutokana na jambo hilo inasemakana Mh.waziri aliyejiuzulu ameona kuwa anaingiliwa katika utendaji kazi wake hivyo kuamua kumuandikia barua ya kujiuzulu Dr. Hussein Mwinyi.

Binafsi nampongeza Waziri simai mohamed saidi kwa kusimamia anachokiamini hata kama kuna watakao muona kakosea. Kiongozi asiyeweza kusimamia anachoamini hafai.
 
Waziri wa utalii Zanzibar ambaye ni rafiki yangu binafsi Mh Simai amejiuzulu. Inaelekea kuna mgogoro mdogo na hujuma za maslahi. Kuna viongozi wamewafukuza wasambaza vivyaji makusudi ili kuleta drama kwa watalii. Sasa haujulikani kama ni dini, rushwa au wanawania nafasi ya Simai. Naona mwana Ilboru mwenzetu yuko mbele sana na hapendi ujinga jinga
 

Attachments

  • IMG_6047.MOV
    19.7 MB
  • BE14D912-A1C0-4958-8DA6-EAEB665FE3FC.jpeg
    38.9 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…