Zanzibar: Tsh. 150M zilizookotwa zarudishwa. Biashara ya kununua jini yahusishwa

Zanzibar: Tsh. 150M zilizookotwa zarudishwa. Biashara ya kununua jini yahusishwa

Darmian

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
17,315
Reaction score
46,858
Nilikuwa nime-tunein to Clouds FM Amplifaya na Millard Muyenjwa Ayo nikasikia hii stori na imenishangaza kidogo.

Kuna bwana huko Zanzibar aliokota milioni 150 na akaona ni bora atangaze ili aliyezipoteza aje kufwata mzigo wake alikuwa anauliza tricky questions ili ampate aliyezipoteza kweli.

Kuna raia wa Oman alijibu maswali fresh na mzigo ikaonekana ni wake na kwenye maelezo ya aliyeokota hizo fedha anasema huyu bwana raia wa Oman ni mfanyabiashara na alikuwa ameenda Zanzibar kununua "jini" yes jini ili liwe linasimamia biashara zake ziende poa. So aliambiwa na muuza jini kuwa nenda sehemu fulani acha hizo fedha then jini atapita kuzichukua ila sijui jini hakutokea ndo jamaa akaziokota hizo fedha.

Nimeshangaa sana hili la kununua jini kwa 150M kumbe haya mambo yapo serious hivi, nilikuwa nadhani ni mambo mambo tu ya kiswahili Biashara +majini.

===

1613461929108.png

Msamaria mwema Mkazi wa Unguja, Zanzibar Suleiman Bakari Ramadhan Akida amefanikiwa kuzirejesha Tsh. MILIONI 150 kwa Mmiliki wake halali baada ya kuziokota zikiwa zimepotezwa

"Tulishirikiana katika swala zima la kusambaza tangazo la uokotwaji wa pesa katika kisiwa cha Unguja”

“Changamoto zilikua nyingi na nimepigiwa simu sana wengi wanasema wamepoteza lakini nimempata Mmiliki wake ambae ni Raia wa Oman baada ya kujibu maswali likiwemo la pesa zilipotea zikiwa kwenye mfuko wa aina gani, tayari nimeshamtumia kwenye account yake na nimelipia 170000 ya ziada ili tu azipate pesa zake zikiwa kamili MILIONI 150"

Chanzo cha habari ni Millardayo
 
Ananikubusha mzee mmoja Arusha yupo hadi sasa ni ndugu yangu, Yule Mzeee ana Bahati za Kipekee niseme, make kuokota pesa tu alisha okota sana na anarudisha, alishaa wahi ingiziwa kimakosa milion 700 kwenye account yake halafu ni acvount ambayo alikuwa haitumii na hakuna na ile huduma ya kupata sms kama kuna pesa imeingia au kutoka, siku amekuja kugundua ni muda,

Kuna Bahati Moja alipewa Gari Jipya kabisa hizi TATA New Model ila aliipata vipi ni story ndefu kidogo
 
Alienda kuwaambia benki kuhusu hizo millioni 700?
 
Hii story niliisikia toka last week ila kama imekaa kibiashara biashara.

Alieokota mzigo alijuaje kuwa huo mzigo wa pesa ilibidi jini ndio auchukue??? Hayo mambo yote alijulia wapi? Au ndio baada ya kumpata mwenye mzigo alimchana kuwa alienda kununua jini!!
 
Mwenye huo mzigo aliojiwa na aliyeziokota na akasema hayo yote, kwa jinsi habari inavyosema.
 
Zanzibar inajijua ilivyo, vitu vya kuokota okota ovyo na kutumia kule unakuwa msukule. Watu kule hela za kuokota wanaziogopa kama ukoma japo kwa jinsi nilivopigia hivi, ningekuwa jini tayari huko Oman [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] mana najua nisingezitangaza na ningezitumia tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787] yan ata jero nisitumie?
[emoji3][emoji3]Ungekuwa Oman huko mzee unalinda biashara za watu
 
Ila Zenji hutakiwi kuweka tamaa mbele unakuwa jini🤣🤣🤣 yaani ata shilingi mia hutakiwi kuiwekea tamaa eti uokote.
 
Back
Top Bottom