Zanzibar turudishe heshima yetu, tuige mfano mzuri wa Qatar, pombe ipigwe marufuku kabisa

Zanzibar turudishe heshima yetu, tuige mfano mzuri wa Qatar, pombe ipigwe marufuku kabisa

Nchi ya Qatar imenivutia sana kwa kuwa na msimamo mzuri dhidi ya uozo wa kimagharibi wa pombe, ngono, ushoga etc

Zanzibar ni nchi nzuri ya kistaarabu sana lakini naona kuna uozo unaongezeka kwa kasi kubwa.

Nyimbo na video za uchi, unywaji pombe, kuvaa vivazi vya nusu uchi hadharani n.k.

Ni muda sasa wa Zanzibar kuweka heshima ya ustaarabu wetu tupige marufuku bar zote na TV zinazopiga nyimbo za nusu uchi.
Unazuia pombe na watu wanatoa line mbili 😃 kuleni tu ngurue
 
Unajua maana ya neno USTA-ARABU na neno KUST-ARABIKA????Mdogo wangu????NA STONE AGE UNAZINGUMIZIA YA UPANDE UPI DUNIANI????MAANA DUNIA KUBWA MDOGO WANGU
Kwa hiyo turudi kutembea uchi basi kwa kuwa kuvaa nguo ni kuiga utamaduni wa kigeni
 
Nchi ya Qatar imenivutia sana kwa kuwa na msimamo mzuri dhidi ya uozo wa kimagharibi wa pombe, ngono, ushoga etc

Zanzibar ni nchi nzuri ya kistaarabu sana lakini naona kuna uozo unaongezeka kwa kasi kubwa.

Nyimbo na video za uchi, unywaji pombe, kuvaa vivazi vya nusu uchi hadharani n.k.

Ni muda sasa wa Zanzibar kuweka heshima ya ustaarabu wetu tupige marufuku bar zote na TV zinazopiga nyimbo za nusu uchi.
Tulikua Qatar kwenye world cup na kuna club kabisa zinauza pombe.. watu tulikuza henekene za kutosha!

Starehe za wenzio zisikutoe roho mbona wewe mwasherati na hatukusumbui?
 
Z'bar sio Islamic republic
Mnataka hayo,vunjeni muungano sasa
He, hii haihusiani na Uislamu, maadili mema ya kuvaa kwa stara na kuepuka ulevi mbona hata Wakristo wanasisitiza sana hayo?
 
Mkifanya hivyo, Zanzibar itakuwa kama Saudia.

Saudia sheria inazuia biashara ya pombe, lakini Saudia ndiyo inayoongoza Duniani kwa kununua mitambo ya kutengenezea pombe majumbani. Ukishuka tu kwenye ndege pale King Khalid International airport unafuatwa na watu, unaulizwa kama unataka pombe ili wakuletee hotelini. Yaani uwatajie hoteli utakayofikia halafu wakuletee pombe.

Masuala ya imani aachiwe mtu mwenyewe, isipokuwa yale yenye kuwaathiri na watu wengine, hayo ndiyo yapigwe marufuku au yatengewe maeneo maalum.

Pombe inamwathiri mtumiaji mwenyewe, lakini vitu kama sigara, hata usiyevuta unaathirika kama unakuwepo kwenye mazingira ya wavutaji.
Mbona sio swala la Uislamu, dini nyingi zinakataza pombe na uasherati, hata usipokuwa na dini tu, hutapenda mwanao awe anakunywa pombe au kuvaa bila stara
 
bahati mbaya kwako ni kuwa wanaotakiwa kupiga marufuku ndiyo walevi waliokubuhu zanzibar. wanajificha kw kuvaa kanzu na baraghashia ni hijabu na baibui
Inahitaji kiongozi mmoja jasiri tu,
 
Definition ya stara according na imani yako ndio unayotaka tuu, acha watu wajivalie wanavyotaka as long as wamefunika mbususu zao sio tatizo
Imani yangu unaijua? Ni imani gani inayotaka watu kutembea uchi?
 
Hayo mambo madogo sana,tatizo la kuwaza kwa kutumia dini,Ili kutatua matatizo ya kiuchumi,
Zenj vijana hawana ajira,uchumi ni tegemezi,Zenj haiwezi jiendesha bila kuwa kupe wa Tanganyika,sasa badala ya kuwaza kukuza uchumi,kupitia sekta za IT,utalii,kilimo,real estate,viwanda Ili Zenj iwe kama Hongkong au Taiwan,au Qatar !!mbulula anawaza pombe na kuvaa vimini,kwamba ndio tatizo kuu!!!
Akili za kiislam huwa zinashangaza sana.
Unakuta kijana kama (zuchu na Mond),hawafanyi matangazo ya pombe sababu wao ni "watoto wa kiislam"
Ila wanakulana nje ya ndoa,kadadaa kama piga pozi kama porn artist!!hapo "utoto wa kiislam haupo""
Unafiki balaaa
Utakuzaje uchumi na watu wasiokuwa na maadili? Yaani una mtu anakunywa pombe hovyo huyo mtu anaweza ku focus kwenye kazi? Mtu asiyekuwa hata na discipline ya kuvaa ndio aje afanye kazi kwa discipline?
 
Huwezi kupiga pombe marufuku bila ya kwanza kuwa Islamic republic, na Zanzibar siyo Islamic country ili seize kuwa Islamic 200 years a go, leo hii mfumo mzima wa Zanzibar ni Christian (western) hata Watalii inategemea kutoka Ulaya na USA na siyo Iran au Saudia, …
Marekani ilishawahi kupiga pombe marufuku na sio Islamic republic, nenda kasome.
 
Huna akili ,

Hizi ni picha za watu wakinywa pombe hapo Qatar.


Mlivyo wajinga huwa mnadhani wanaoharibu maadili ya Zanzibar ni wabara Tu Ila wale wazungu waotembea uchi na kunywa pombe hamuwaoni.
images (49).jpg
images (48).jpg
images (47).jpg
images (46).jpg
images (45).jpg


Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom