Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Hatishii. Anawatahadharidha wale wote wanaofikiria watachezea amani ya nchi hii. Unawakumbuka UKUTA? Waliweka mpira kwapani dakika za mwisho baada ya kumwelewa.
Wanatishia amani kivipi wanataka kulipuwa mabomu au maana bado sijaelewa wanatishiaje amani ya nchi.
 
Mzee anasema mtu akileta zake amnong'oneze,hivi anawajua wazanzibar vizuri kweli,au wanadhani wale ni wanyakyusa au wapare.
Kwa kutangaza kuwashughulika wapanzani wa kisiasa kwa nguvu zote Tz, tumepata Rais binadamu asiye na chembe ya ubinadamu
 
Hizi hotuba mimi sijawahi sikia mubashara,yanayoonekana kwenye uzi ni hotuba au uzushi wa JF?kumlisha rais maneno
 
Ngoja nisome maoni ya Watanzania wenzangu. Maana hapa giza na mbele giza.
 
Kwenye hili la Seif Sharif kuwadanganya CUF nakubaliana nae,,yaani jamaa kazunguuka huko hadi leo hana la maana
 
Nilitaka kuandika kitu ila ngoja nitulie
 
Hongera Mh. Rais kwa kudumisha Muungano kwa vitendo.
 
We ndiyo unaliona leo, mimi nilishaliona zamani kuwa ana matani/mizaha... ya matairi ya magari, elfu tano za polisi kubrush viatu, kufyatua etc. Ila nikashtuka aliposema hakuna mikutano, na akawa hatanii (nilidhani ni utani wake), hapo nikaanza kufikiri tena tofauti na mtazamo wa utani!
 
Najuuta najuta kumpa kura yangu huyu jamaa.natamani uchaguzi uitishwe hata kesho .ameniboa kuliko maelezo yani.
 
Huyu jamaa ananitia hasira sana haswa juu ya jecha,tumwogope mungu
 
Ukawa na wapinzani uchwara.. Wapinzani mara nyingi wanapenda kuongea kauli za uchochezi.. Kumbuka kipindi kile Mbowe Mwaka 2015 alikua anasema nchi itawaka Moto, uchaguzi usipofanyika October.. Lakini wapinzani wenzake hawakukosoa..

Au utasikia mara nyingi oooh wananchi wasipokua huru kukosoa itakua kama Libya, pamoja na kupewa kila Kitu..


Lakini kauli hizi zikitolewa na serikali kua... Amani ni muhimu, tusichezee amani yetu kama watu wa Libya.. Upinzani utasikia, serikali inatisha wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…