Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Magufuli asipoandikiwa hotuba na wenye busara, yuko mbioni kuliingiza taifa hili kwenye machafuko makubwa!

Hivi JECHA ni wa kumsifia?

Cha kushangaza huwa anasema tumuombee? Kweli utathubutu kwenda mbele za MUNGU kwa ajili ya MAGUFULI anayeona JECHA yuko sawa?

Taifa linaangamia!
 
Uuuuwii!!

Mbona jazba, maghadhabu, hasira.

Nini tatizo au hatutakiwi kuonekana Tz?
 
Mzee anasema mtu akileta zake amnong'oneze,hivi anawajua wazanzibar vizuri kweli,au wanadhani wale ni wanyakyusa au wapare.
Wasukusuku.

Yaani Mimi ndiyo nimeona aibu.
Hapana, Mimi si mtz for 4yrs to come.
 
Itakuwa 'kalazimika' kutumia hii ili kujibu hoja za Kitwanga... Si unajua zile Jet zinahitaji long runway ili ziweze kutua wakati hizi za mapanga boi zinahitaji kiwanja kifupi tuu...
Gharama zimelipwa kwa shirika?au ndio wanaanza kulihujumu shirika kwa matumizi yasiyo ya kibuashara?
 
naona kaenda na kidumu cha petrol kuzima moto kwa jirani, Elimu ni zaidi ya kukaa darasani
 
Hotuba ya Magufuli kwa Wazanzibar ilikua inachochea chuki kwa wazanzibari
 
Hii sampuli ya kupiga push up jukwaani tegemea vituko tu
Diplomasi hakuna kabisa..
Vitisho havisaidii chochote, ni dalili za kutojiamini au anajiona hatoshi kwenye nafasi Aliopo
demokrasia alikua nayo mkwere mkasema dhaifu,mpole anachekacheka,.Sasa subirini mbatizwe kwa moto[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…