Tua Ngoma
JF-Expert Member
- Apr 14, 2015
- 3,185
- 8,294
Bora mi sijasemaNa wasi wasi na uelewa.wa magufuli..anaelewa tofauti na Mimi... Nahisi mmoja Kati yetu ni kichaa ...kama sio Mimi basi ni yeye...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bora mi sijasemaNa wasi wasi na uelewa.wa magufuli..anaelewa tofauti na Mimi... Nahisi mmoja Kati yetu ni kichaa ...kama sio Mimi basi ni yeye...
View attachment 392484 View attachment 392485
Anaeongea kwa sasa ni Rais John Magufuli baada ya kukaribishwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na anazungumzia amani. Anasema mtu hawezi kuja kuwekeza Pemba wakati watu hawasalimiani, anasema mume na mke wakiwa hawaelewani kwa sababu ya vyama vya siasa hajui usiku wanalalaje. Amesema anajua vijana wengi hawana ajira Pemba, watapata ajira endapo wawekezaji watakuja kujenga sehemu ambayo ina amani.
Magufuli: Uchaguzi umeshakwisha na utakuja tena 2020, huo ndio ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Uchaguzi umekwisha mimi nikachaguliwa kuwa Rais na naitwa John Pome Magufuli na nimefunga Makufuli yote na funguo nimeshatupa.
Nataka niseme Mhe Dk Shein, wewe ndie Rais na inawezekana umekuwa mpole kidogo, huo upole weka pembeni, unasapoti yangu yote, atakaekuchezea chezea niambie hata kwa kuninong'oneza.
Tushirikiane kwa nguvu zote, wanaojaribu kuchezea amani yetu, mimi niliwahi kwenda Libya, mojawapo ya nchi za Afrika zilizokuwa na raha ni mojawapo. Pakajitokeza watu wachache kwa kuahidiwa ahadi za uongo, Libya leo siyo mahali panapokalika, watu wanamwaga damu kila siku, watu walichezea amani, hata amani inalevya.
Rwanda wakati wa genocide walikufa watu wanaokaribia milioni moja, mmenichagua kuwa Rais wenu, nna wajibu wa kuwaeleza ukweli, wanaofanya chokochoko tunawajua wengine, wafatilieni wote wanaochomachoma washughulikiwe wote bila huruma. Mna bahati mna Rais mpole sana na hata sura yake nzuri tu na ni Rais alietoka Pemba, ni kitu gani kinatusumbua.
Mimi nilifanya nae kazi nikiwa naibu waziri na waziri, ninamfajhamu Dk Shein, mpeni ushirikiano. Kuna mtu alijifungia kwenye chumba alafu akasema ametoka Ulaya, msikubali kudanganywa, hivi karibuni alinunua Meli na zinafanya kazi, kuna maeneo mengi yamepelekwa maji na umeme, watu hamtaki kuyaona haya. Palikuwa na Prof Mbarawa hapa mkamkataa jimbo la mkoani(Mkanyageni) mkamkanyagia hukohuko, mimi nnafahamu umuhimu wake na nikachukua wizara tatu nikaziunganisha zote nikampa mtu aliekanyagwa huku.
Mpeni ushirikiano Dk Shein, imebaki miaka minne tu na kitu na kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hiki ndio kipindi chake cha mwisho. Nawaomba wananchi tujenge umoja wetu. Tukienda kwa umoja wetu tutafanikiwa, tunataka tuimarishe uvuvi, mazao na serikali iliongeza hela kununua karafuu japo pato lake limeanza kushuka, tunataka tujenge hii nchi. Katika kipindi kifupi Pemba itakuwa kama Ulaya na wanaoharibu Pemba ni watu wachache sana.
Wengine wanasema uchaguzi utarudiwa, kwa kawaida ndoto huwa ni usiku lakini hizo ni ndoto za usiku, lakini ukimkuta mtu anaota mchana, huyo anatafuta ukichaa. Nampongeza sana nh Jecha kwa kusimamia uchaguzi na umeenda vizruri sana na kama kuna tuzo mheshimiwa Shein utatoa, Jecha umpe hizo tuzo. Napongeza sana vyombo vya ulinzi, mmefanya kazi nzuri sana, mmesimamia amani ya Tanzania kwa uzalendo mkubwa sana.
=====
Rais John Magufuli atua Pemba muda mfupi uliopita akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli baada ya mapokezi yaliyombatana na kikundi cha ngoma, ameenda kuzulu kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Omary Ali Juma. Baadaye saa tisa alasiri atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale, Pemba.
==========
Habari zaidi...
Septemba 2, 2016, Rais John Magufuli amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili visiwani Zanzibar, baada ya kukaribishwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na akazungumzia amani. Amesema mtu hawezi kuja kuwekeza Pemba wakati watu hawasalimiani, anasema mume na mke wakiwa hawaelewani kwa sababu ya vyama vya siasa hajui usiku wanalalaje. Amesema anajua vijana wengi hawana ajira Pemba, watapata ajira endapo wawekezaji watakuja kujenga sehemu ambayo ina amani.
Magufuli: Uchaguzi umeshakwisha na utakuja tena 2020, huo ndio ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Uchaguzi umekwisha mimi nikachaguliwa kuwa Rais na naitwa John Pome Magufuli na nimefunga Makufuli yote na funguo nimeshatupa.
Nataka niseme Mhe Dk Shein, wewe ndie Rais na inawezekana umekuwa mpole kidogo, huo upole weka pembeni, unasapoti yangu yote, atakaekuchezea chezea niambie hata kwa kuninong’oneza.
Tushirikiane kwa nguvu zote, wanaojaribu kuchezea amani yetu, mimi niliwahi kwenda Libya, mojawapo ya nchi za Afrika zilizokuwa na raha ni mojawapo. Pakajitokeza watu wachache kwa kuahidiwa ahadi za uongo, Libya leo siyo mahali panapokalika, watu wanamwaga damu kila siku, watu walichezea amani, hata amani inalevya.
Rwanda wakati wa genocide walikufa watu wanaokaribia milioni moja, mmenichagua kuwa Rais wenu, nna wajibu wa kuwaeleza ukweli, wanaofanya chokochoko tunawajua wengine, wafatilieni wote wanaochomachoma washughulikiwe wote bila huruma. Mna bahati mna Rais mpole sana na hata sura yake nzuri tu na ni Rais alietoka Pemba, ni kitu gani kinatusumbua.
Mimi nilifanya nae kazi nikiwa naibu waziri na waziri, ninamfajhamu Dk Shein, mpeni ushirikiano. Kuna mtu alijifungia kwenye chumba alafu akasema ametoka Ulaya, msikubali kudanganywa, hivi karibuni alinunua Meli na zinafanya kazi, kuna maeneo mengi yamepelekwa maji na umeme, watu hamtaki kuyaona haya. Palikuwa na Prof Mbarawa hapa mkamkataa jimbo la mkoani (Mkanyageni) mkamkanyagia hukohuko, mimi nnafahamu umuhimu wake na nikachukua wizara tatu nikaziunganisha zote nikampa mtu aliekanyagwa huku.
Mpeni ushirikiano Dk Shein, imebaki miaka minne tu na kitu na kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hiki ndio kipindi chake cha mwisho. Nawaomba wananchi tujenge umoja wetu. Tukienda kwa umoja wetu tutafanikiwa, tunataka tuimarishe uvuvi, mazao na serikali iliongeza hela kununua karafuu japo pato lake limeanza kushuka, tunataka tujenge hii nchi. Katika kipindi kifupi Pemba itakuwa kama Ulaya na wanaoharibu Pemba ni watu wachache sana.
Wengine wanasema uchaguzi utarudiwa, kwa kawaida ndoto huwa ni usiku lakini hizo ni ndoto za usiku, lakini ukimkuta mtu anaota mchana, huyo anatafuta ukichaa. Nampongeza sana Mh. Jecha kwa kusimamia uchaguzi na umeenda vizuri sana na kama kuna tuzo mheshimiwa Shein utatoa, Jecha umpe hizo tuzo. Napongeza sana vyombo vya ulinzi, mmefanya kazi nzuri sana, mmesimamia amani ya Tanzania kwa uzalendo mkubwa sana.
“Dokta Shein una support yangu yote, ukiona umemshindwa mtu, nambie mimi uone kama itapita hata dk 5”
“Wakati tukinadi kwenye kampeni mimi na Shein, tulisema tunataka Tanzania yenye viwanda”
“Hawezi mtu kuja kujenga kiwanda kama kuna vurugu, watu hawasalimiani, hamna amani.”
“Vijana wa Pemba hawana ajira kama walivyo vijana wa bara, kwa hiyo vijana lazima tuwe wa mbele kujenga amani.”
“Na mimi nataka nikwambie Dk. Shein, wewe ndiyo Rais, na naona umekuwa mpole sana,
“Upole uweke pembeni, uwe mkali kidogo, usikubali kuchezewa na mtu,
“Libya ilikuwa nchi ya amani, wakatumiwa watu wachache kwa ahadi za uongo, sasa Libya hakukaliki, watu wanakimbia…”
“Libya watu wanamwaga damu kila siku, kwa sababu watu walichezea amani.”
Mna bahati ndugu zangu, mna rais mpole sana , hata sura yake nzuri tu, Lakini pia ametoka Pemba, mnataka nini!? Mnataka malaika aje aongoze!?
Alisema rais Magufuli.
Wasukusuku.Mzee anasema mtu akileta zake amnong'oneze,hivi anawajua wazanzibar vizuri kweli,au wanadhani wale ni wanyakyusa au wapare.
Gharama zimelipwa kwa shirika?au ndio wanaanza kulihujumu shirika kwa matumizi yasiyo ya kibuashara?Itakuwa 'kalazimika' kutumia hii ili kujibu hoja za Kitwanga... Si unajua zile Jet zinahitaji long runway ili ziweze kutua wakati hizi za mapanga boi zinahitaji kiwanja kifupi tuu...
Na kwa wapemba walivyo,mbona kuna mtu kaingia chaka!Naona anapalilia chuki staki kumlaum Bali mola nipe uhai nione matunda ya wanachopanda
Bora wewe mkuuWasukusuku.
Yaani Mimi ndiyo nimeona aibu.
Hapana, Mimi si mtz for 4yrs to come.
Ukawa na wapinzani uchwara.. Wapinzani mara nyingi wanapenda kuongea kauli za uchochezi.. Kumbuka kipindi kile Mbowe Mwaka 2015 alikua anasema nchi itawaka Moto, uchaguzi usipofanyika October.. Lakini wapinzani wenzake hawakukosoa..
Au utasikia mara nyingi oooh wananchi wasipokua huru kukosoa itakua kama Libya, pamoja na kupewa kila Kitu..
Lakini kauli hizi zikitolewa na serikali kua... Amani ni muhimu, tusichezee amani yetu kama watu wa Libya.. Upinzani utasikia, serikali inatisha wananchi
Hotuba ya Magufuli kwa Wazanzibar ilikua inachochea chuki kwa wazanzibari
demokrasia alikua nayo mkwere mkasema dhaifu,mpole anachekacheka,.Sasa subirini mbatizwe kwa moto[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Hii sampuli ya kupiga push up jukwaani tegemea vituko tu
Diplomasi hakuna kabisa..
Vitisho havisaidii chochote, ni dalili za kutojiamini au anajiona hatoshi kwenye nafasi Aliopo