Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Washazoea kulalamika bila kuwa na fikra pevu na yakinifuKwani hiyo ndege nayo si ajira pia kwa watu?
Ebu fikiria kuanzia kwenye hiyo ndege,marubani,mafundi, cabin crew, wabeba mizigo,wasafishaji, waongozaji, walinzi, check in clerks, immigration officials. Baada ya hapo nenda kwenye secondary business: Ground transportation, migahama na mahotel, maduka...
Hivi vyote utavikuta ndani ya aviation industry na vinatoa ajira nyingi sana na msingi ni...Hiyo ndege.
mtukufu mpendwa mheshimiwa Ph.Dkaswali kagumu.
Nazipenda kucha zanguu miee
Mkuu sasa mbona solution ni rahisi tu. Kama kweli demokrasia haitufai...JPM apeleke mswada bungeni wa kufuta mfumo wa vyama vingi..ccm waupitishe...tujue TZ imekua nchi ya chama kimoja rasmi. kwanza itaokoa hela za walipa kodi...maana sasa hivi wapinzani wanapewa mabilioni ya ruzuku na huku wanazuiwa kufanya shughuli zao.Kwa nchi za Afrika demokrasia haiwezi leta maendeleo jaribu kuangalia historia halisi ya uongozi katika dunia
tatizo sio ajira,bali tatizo lilianza pale tulipokubali kurithi na kuuenzi kwa dhati na juhudi zote mfumo wa elimu ya kikoloni(mfumo wa elimu tegemezi)..laiti sote kama taifa kupitia wale tuliowachagua tungekubaliana kuubadili mfumo huu,naimani Tanzania kuna ajira nyingi sana hata pasipo kutegemea ajira toka serikalini.Kwel nineamini ajira sio kipaumbele cha serikali hii, yani ndege zinanunuliwa lakini ajira nooh
Adui zenu ni wakina nani?Muungano wetu ndio umoja wetu. Adui zetu hawaupendi huu muungano. Tutaulinda muungano huu kwa nguvu zetu.
Ningekuwa mimi ningeongea yote,lakini nisingempongeza Jecha.Roho yangu ingenisuta kwa kuwa najua kilichotoka!
Anaeongea kwa sasa ni Rais John Magufuli baada ya kukaribishwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na anazungumzia amani. Anasema mtu hawezi kuja kuwekeza Pemba wakati watu hawasalimiani, anasema mume na mke wakiwa hawaelewani kwa sababu ya vyama vya siasa hajui usiku wanalalaje. Amesema anajua vijana wengi hawana ajira Pemba, watapata ajira endapo wawekezaji watakuja kujenga sehemu ambayo ina amani.
Magufuli: Uchaguzi umeshakwisha na utakuja tena 2020, huo ndio ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Uchaguzi umekwisha mimi nikachaguliwa kuwa Rais na naitwa John Pome Magufuli na nimefunga Makufuli yote na funguo nimeshatupa.
Nataka niseme Mhe Dk Shein, wewe ndie Rais na inawezekana umekuwa mpole kidogo, huo upole weka pembeni, unasapoti yangu yote, atakaekuchezea chezea niambie hata kwa kuninong'oneza.
Tushirikiane kwa nguvu zote, wanaojaribu kuchezea amani yetu, mimi niliwahi kwenda Libya, mojawapo ya nchi za Afrika zilizokuwa na raha ni mojawapo. Pakajitokeza watu wachache kwa kuahidiwa ahadi za uongo, Libya leo siyo mahali panapokalika, watu wanamwaga damu kila siku, watu walichezea amani, hata amani inalevya.
Rwanda wakati wa genocide walikufa watu wanaokaribia milioni moja, mmenichagua kuwa Rais wenu, nna wajibu wa kuwaeleza ukweli, wanaofanya chokochoko tunawajua wengine, wafatilieni wote wanaochomachoma washughulikiwe wote bila huruma. Mna bahati mna Rais mpole sana na hata sura yake nzuri tu na ni Rais alietoka Pemba, ni kitu gani kinatusumbua.
Mimi nilifanya nae kazi nikiwa naibu waziri na waziri, ninamfajhamu Dk Shein, mpeni ushirikiano. Kuna mtu alijifungia kwenye chumba alafu akasema ametoka Ulaya, msikubali kudanganywa, hivi karibuni alinunua Meli na zinafanya kazi, kuna maeneo mengi yamepelekwa maji na umeme, watu hamtaki kuyaona haya. Palikuwa na Prof Mbarawa hapa mkamkataa jimbo la mkoani(Mkanyageni) mkamkanyagia hukohuko, mimi nnafahamu umuhimu wake na nikachukua wizara tatu nikaziunganisha zote nikampa mtu aliekanyagwa huku.
Mpeni ushirikiano Dk Shein, imebaki miaka minne tu na kitu na kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hiki ndio kipindi chake cha mwisho. Nawaomba wananchi tujenge umoja wetu. Tukienda kwa umoja wetu tutafanikiwa, tunataka tuimarishe uvuvi, mazao na serikali iliongeza hela kununua karafuu japo pato lake limeanza kushuka, tunataka tujenge hii nchi. Katika kipindi kifupi Pemba itakuwa kama Ulaya na wanaoharibu Pemba ni watu wachache sana.
Wengine wanasema uchaguzi utarudiwa, kwa kawaida ndoto huwa ni usiku lakini hizo ni ndoto za usiku, lakini ukimkuta mtu anaota mchana, huyo anatafuta ukichaa. Nampongeza sana nh Jecha kwa kusimamia uchaguzi na umeenda vizruri sana na kama kuna tuzo mheshimiwa Shein utatoa, Jecha umpe hizo tuzo. Napongeza sana vyombo vya ulinzi, mmefanya kazi nzuri sana, mmesimamia amani ya Tanzania kwa uzalendo mkubwa sana.
=====
Rais John Magufuli atua Pemba muda mfupi uliopita akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli baada ya mapokezi yaliyombatana na kikundi cha ngoma, ameenda kuzulu kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Omary Ali Juma. Baadaye saa tisa alasiri atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale, Pemba.
==========
Inshallah Mnyazi Mungu amlinde katika shughuli zake zote.
Mkuu nimekupa laiki lakini sijui ni kwanini, by da way wapemba sio kama wale wala sato. Subiri watapata majibuMzee anasema mtu akileta zake amnong'oneze,hivi anawajua wazanzibar vizuri kweli,au wanadhani wale ni wanyakyusa au wapare.
Kwa nchi za Afrika demokrasia haiwezi leta maendeleo jaribu kuangalia historia halisi ya uongozi katika dunia
Naskia Rais hafanyi siasa bali anatembelea wananchi.!!Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usalama wametoa tamko la kuzuia mikutano ya siasa japokuwa ni haki yao kikatiba lakini CCM wanaruhusiwa kufanya mikutano kama huko Pemba kuna mkutano hivi ingekuwa na mkutano wa CUF ungeruhusiwa?
Ushindi wa mwendo kasiNa aruhusu cuf nao wafanye mkutano hapo hapo ili tulinganishe na mkutano wake ili tuone nani kamzika nani, we unashindana peke yako bila rival af mwisho wa siku unakuja kujisifia eti umeshinda?
Nyie wazanzibar kwendeni huko tuachieni Tanganyika yetu..Muungano wetu ndio umoja wetu. Adui zetu hawaupendi huu muungano. Tutaulinda muungano huu kwa nguvu zetu.