Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Raisi kaeleza umuhimu wa watu wote wa Pemba kupendana Karibuni tucheze tuburudike wapemba wote.
Tucheze kidogo na huu wimbo wa amani

 
Kwani hiyo ndege nayo si ajira pia kwa watu?
Ebu fikiria kuanzia kwenye hiyo ndege,marubani,mafundi, cabin crew, wabeba mizigo,wasafishaji, waongozaji, walinzi, check in clerks, immigration officials. Baada ya hapo nenda kwenye secondary business: Ground transportation, migahama na mahotel, maduka...
Hivi vyote utavikuta ndani ya aviation industry na vinatoa ajira nyingi sana na msingi ni...Hiyo ndege.
Washazoea kulalamika bila kuwa na fikra pevu na yakinifu
 
Kwa nchi za Afrika demokrasia haiwezi leta maendeleo jaribu kuangalia historia halisi ya uongozi katika dunia
Mkuu sasa mbona solution ni rahisi tu. Kama kweli demokrasia haitufai...JPM apeleke mswada bungeni wa kufuta mfumo wa vyama vingi..ccm waupitishe...tujue TZ imekua nchi ya chama kimoja rasmi. kwanza itaokoa hela za walipa kodi...maana sasa hivi wapinzani wanapewa mabilioni ya ruzuku na huku wanazuiwa kufanya shughuli zao.
 
Kwel nineamini ajira sio kipaumbele cha serikali hii, yani ndege zinanunuliwa lakini ajira nooh
tatizo sio ajira,bali tatizo lilianza pale tulipokubali kurithi na kuuenzi kwa dhati na juhudi zote mfumo wa elimu ya kikoloni(mfumo wa elimu tegemezi)..laiti sote kama taifa kupitia wale tuliowachagua tungekubaliana kuubadili mfumo huu,naimani Tanzania kuna ajira nyingi sana hata pasipo kutegemea ajira toka serikalini.
 
Ningekuwa mimi ningeongea yote,lakini nisingempongeza Jecha.Roho yangu ingenisuta kwa kuwa najua kilichotoka!​



Anaeongea kwa sasa ni Rais John Magufuli baada ya kukaribishwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na anazungumzia amani. Anasema mtu hawezi kuja kuwekeza Pemba wakati watu hawasalimiani, anasema mume na mke wakiwa hawaelewani kwa sababu ya vyama vya siasa hajui usiku wanalalaje. Amesema anajua vijana wengi hawana ajira Pemba, watapata ajira endapo wawekezaji watakuja kujenga sehemu ambayo ina amani.

Magufuli: Uchaguzi umeshakwisha na utakuja tena 2020, huo ndio ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Uchaguzi umekwisha mimi nikachaguliwa kuwa Rais na naitwa John Pome Magufuli na nimefunga Makufuli yote na funguo nimeshatupa.

Nataka niseme Mhe Dk Shein, wewe ndie Rais na inawezekana umekuwa mpole kidogo, huo upole weka pembeni, unasapoti yangu yote, atakaekuchezea chezea niambie hata kwa kuninong'oneza.

Tushirikiane kwa nguvu zote, wanaojaribu kuchezea amani yetu, mimi niliwahi kwenda Libya, mojawapo ya nchi za Afrika zilizokuwa na raha ni mojawapo. Pakajitokeza watu wachache kwa kuahidiwa ahadi za uongo, Libya leo siyo mahali panapokalika, watu wanamwaga damu kila siku, watu walichezea amani, hata amani inalevya.

Rwanda wakati wa genocide walikufa watu wanaokaribia milioni moja, mmenichagua kuwa Rais wenu, nna wajibu wa kuwaeleza ukweli, wanaofanya chokochoko tunawajua wengine, wafatilieni wote wanaochomachoma washughulikiwe wote bila huruma. Mna bahati mna Rais mpole sana na hata sura yake nzuri tu na ni Rais alietoka Pemba, ni kitu gani kinatusumbua.

Mimi nilifanya nae kazi nikiwa naibu waziri na waziri, ninamfajhamu Dk Shein, mpeni ushirikiano. Kuna mtu alijifungia kwenye chumba alafu akasema ametoka Ulaya, msikubali kudanganywa, hivi karibuni alinunua Meli na zinafanya kazi, kuna maeneo mengi yamepelekwa maji na umeme, watu hamtaki kuyaona haya. Palikuwa na Prof Mbarawa hapa mkamkataa jimbo la mkoani(Mkanyageni) mkamkanyagia hukohuko, mimi nnafahamu umuhimu wake na nikachukua wizara tatu nikaziunganisha zote nikampa mtu aliekanyagwa huku.

Mpeni ushirikiano Dk Shein, imebaki miaka minne tu na kitu na kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hiki ndio kipindi chake cha mwisho. Nawaomba wananchi tujenge umoja wetu. Tukienda kwa umoja wetu tutafanikiwa, tunataka tuimarishe uvuvi, mazao na serikali iliongeza hela kununua karafuu japo pato lake limeanza kushuka, tunataka tujenge hii nchi. Katika kipindi kifupi Pemba itakuwa kama Ulaya na wanaoharibu Pemba ni watu wachache sana.

Wengine wanasema uchaguzi utarudiwa, kwa kawaida ndoto huwa ni usiku lakini hizo ni ndoto za usiku, lakini ukimkuta mtu anaota mchana, huyo anatafuta ukichaa. Nampongeza sana nh Jecha kwa kusimamia uchaguzi na umeenda vizruri sana na kama kuna tuzo mheshimiwa Shein utatoa, Jecha umpe hizo tuzo. Napongeza sana vyombo vya ulinzi, mmefanya kazi nzuri sana, mmesimamia amani ya Tanzania kwa uzalendo mkubwa sana.


=====
Rais John Magufuli atua Pemba muda mfupi uliopita akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli baada ya mapokezi yaliyombatana na kikundi cha ngoma, ameenda kuzulu kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Omary Ali Juma. Baadaye saa tisa alasiri atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale, Pemba.

==========
 
Mzee anasema mtu akileta zake amnong'oneze,hivi anawajua wazanzibar vizuri kweli,au wanadhani wale ni wanyakyusa au wapare.
Mkuu nimekupa laiki lakini sijui ni kwanini, by da way wapemba sio kama wale wala sato. Subiri watapata majibu
 
Kwa nchi za Afrika demokrasia haiwezi leta maendeleo jaribu kuangalia historia halisi ya uongozi katika dunia

Kule Marekani wakati Bush jr alipigiwa kura na baadhi ambao ni marehemu...tehtehtehteh...Na kule Uingereza ile kura ya BREXIT kuna watu wanalia mpaka leo kwamba kulikuwa na kuchakachuliwa..... Kule Ufaransa nako akina Le Pen nao huwa wanalalamika mno....
 
Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usalama wametoa tamko la kuzuia mikutano ya siasa japokuwa ni haki yao kikatiba lakini CCM wanaruhusiwa kufanya mikutano kama huko Pemba kuna mkutano hivi ingekuwa na mkutano wa CUF ungeruhusiwa?
Naskia Rais hafanyi siasa bali anatembelea wananchi.!!
 
Na aruhusu cuf nao wafanye mkutano hapo hapo ili tulinganishe na mkutano wake ili tuone nani kamzika nani, we unashindana peke yako bila rival af mwisho wa siku unakuja kujisifia eti umeshinda?
Ushindi wa mwendo kasi
 
President ni mtu wa matamko tuuuuuu na vitishoooo. Hataki hata kuwatia moyo wananchi wake na hali ilivyo ngumu maisha yamepanda, hela haina thamani hata ,hela haitoki jumlisha na vitisho. Ni hatari hapo hata mwaka bado
 
Dah Magufuli ameonesha kabisa kuwa hakuna mazungumzo wala hatafanya mazungumzo na wapinzani
 
Back
Top Bottom