ZECO yailipa TANESCO 500m/- kila mwezi

ZECO yailipa TANESCO 500m/- kila mwezi

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
picha-no.-2-564x272.jpg

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini na Nishati, Eliakim Maswi

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini na Nishati, Eliakim Maswi, amekanusha tuhuma za Shirika la Umeme (TANESCO) kwamba linaidai Zanzibar kiasi cha shilingi bilioni 47 kutokana na matumizi ya umeme.

Alisema wamekuwa wakipokea shilingi milioni 500 kila mwezi kutoka Shirika la Umeme Zanzibar, ikiwa ni malipo ya umeme unaotumiwa Zanzibar.

Maswi alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwasilisha mada kwa Wahariri na waandishi wa habari kuhusu mikakati inayochukuliwa kuhakikisha kunakuwa na uhakika wa umeme utakaokidhi matakwa ya Mradi wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaotazamiwa kuanza kutekelezwa mapema mwezi ujao hadi mwaka 2033.

"Kwanza niwaambie (waandishi wa habari),deni hili ni la zamani sana ila ,SMZ imekuwa ikilipa kila mwezi na hata hivi sasa tumepokea shilingi milioni 500 za malipo ya umeme kwa Zanzibar tu," alisema.

"Nawaambia mkawaambie wote wanaosema kwamba Zanzibar inadaiwa na TANESCO kuwa huo ni uongo na kama mtu hajafanya utafiti hana haki ya kuzungumza," alisema.

Pia,aliwataka wananchi kutowasikiliza watu aliodai kuwa ni wanafiki kutokana na kuamua kuzungumzia mambo ya TANESCO nje bunge.

Aliwataka wanasisasa wanaosema kuhusu nishati na madini kuhakikisha hawapotoshi ukweli.

Aidha alisema TANESCO na Wizara ya Madini na Nishati, zimekubaliana kutekeleza mipango waliyojipangia ikiwa ni pamoja na kuhakikisha umeme unapatikana kwa uhakika na kwa bei nafuu ili ifikapo 2025 na asilimia 75 ya Watanzania wawe wanatumia nishati hiyo.

Alisema,Juni 30 mwaka huu,wataipatia TANESCO shilingi bililioni 80 ikiwa ni ruzuku kuhakikisha inapata uwezo wa kujiendesha.

Chanzo: Zanzinews
 
Halafu hizo hela wanajilipa kupitia escrow?

SUALA LA WIZI WA FEDHA TSH200BILS NI HATARI KWA TAIFA YAPO MAMBO YA MSINGI KAMA IFUATAVYO:
1. Singh Sethi wa PAP amesajiliwa Kenya Kama raia wa Afrika Kusini mwenye asili ya Asia
2. Singh Sethi wa PAP amesajiliwa Afrika Kusini Kama raia wa Kenya mwenye asili ya Asia
3. Singh Sethi wa PAP amesajiliwa Tanzania Kama raia wa Tanazani Mzaliwa wa Ruvuma
4. Singh Sethi alishirikiana na Geodion Moi mtoto wa Rais Mio kwa wizi wa US$600million na kuangusha serikali ya KANU
5. Singh Sethi ametajwa kushirikinana Riziwan (Albert Marwa) ndungu wa familia ya JK na kusababisha wizi wa Tshs200Bls
6. Mwanamke Mbunge wa UK alipambana sana kwenye Bunge la UK wakati wa wizi wa fedha za Rada ulifanyika na BAYE na hatimaye fedha zikarudi Tanzania. Serious Fraud ilikuja hapa na kuwadaka akina Chenge na wizi ule lakini CCM ikawalinda.
7. Leo UKAWA wanapewa document ya ukweli juu ya Wizi wa akina Werema na wametoka nje kushinikiza akina Eliakimu Maswi wakamatwe. Ukweli ni kwamba Benki ya Standard Chater ya UK imetapeliwa zaidi ya Tsh1770bls na Singh Sett na wenzake. Serious Fraud wapo hapa na kila kitu kinafahamika
8. Kumufukuza balozi wa UK ni sawa na kumufukuza nzi badala ya kuondoa Kinyesi.
9. Prof Muhongo na Lugora wanasema pesa Tshs200Bils sio za serikali ,Je pesa zisizokuwa za serikali zinawapa CCM kuiba??. Mbona Mbunge la UK walijadili pesa zetu na kuwataja akina Chenge hadi zikarejeshwa?? Huu ni upuuzi wa CCM na serikali yake

10. Kule Malawi watendaji wa Malawi wakiongozwa na Rais Joyce Banda waliiba Zaidi ya US$320 sawa na saidi ya Tshs 500bils wizi huo unaitwa CASHGACSANDAL na Ubalozi wa UK umesususia kutoa Misaada Malawi. Rais Mpya Peter Muthariaka ametangaza Kumushughurikia Kwanza Rais Banda na watu wake ndipo aangalie katiba.
Hapa Tanzania kuna wizi wa Escrow Scandal na Kikwete ameamua kuficha wizi huo na kufanya propaganda za msiba wa Mama Zitto kabwe(shida salumu) huku akijificha kwenye ugonjwa wa dengue na Ukawa!
CCM na watawala wachague Kuwatetea Watuhumiwa kwa malengo ya kuangusha serikali nzima au kuwashughurikia watuhumiwa na kuokoa serikali
 
maswi aache porojo. aeleze fedha zetu walizozikwapua kupitia escrow zinarudi lini. mengine hayo ni ni pumba tu anatuambia, na hatuzihitaji muda huu.
 
Maswi tuelezee siri ya huo utajiri wa haraka haraka ulioupata baada ya kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya nishati!
 
"Siku zote ukweli ukidhihiri uongo hujitenga na mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, pia inatakiwa ukweli usemwe hata kama unauma"

Kila siku Wazanzibar wanasimangwa wanatumie umeme bure unaotoka Tanganyika! Leo kiko wapi!!!???

Wachumia tumbo Wa ZNZ nadhani hii habari itawekera sana maana ni moja ya kichaka chao wanachojifichia eti ZNZ INA maslahi na muungano moja wapo ni umeme bure! Jee milioni 500 kwa malipo ya megawat 90 kwa mwezi ni bure!???? Mungu atawalani na kuendelea kupata aibu ya unafiki wao.

Mengi tutayasikia subirini kidogo tu maana MTU anapokuwa basi hutaja maovu yote aliyofanya. Sio mda mrefu utasikia ZNZ wanatoa Bill moja kama mchango Wa Muungano
 
Muungano huu mzuri kuuimbia taarabu. Ila tukiuvunja, tusije chekana...unatusitahi kwenye mambo mengi sana. Naona tumeuchoka tunataka vitu vya kuazima. Cha kuazima hakisitiri mwili
 
Nafikiri amekata mzizi wa fitina wa wale wachache wanaleta ulaghai kuwa ZNZ HAILIPI UMEME au wengine hata kuse TGK INAWALIPIA UMEME ZNZ.

Hongera Maswi
 
maswi aache porojo. aeleze fedha zetu walizozikwapua kupitia escrow zinarudi lini. mengine hayo ni ni pumba tu anatuambia, na hatuzihitaji muda huu.

Tunazihitaji sana tena sana ili yawe majibu kwa wote wanaosena ZNZ inatumia umeme wa bure!

Pia utawaumbua wale wachumia tumbo wa CCM ZNZ wanaosema faida moja ya muungano ni Zanzibar kutumia umeme bure! Leo uongo wao umefika kikomo watafute chaka jengine la kujifichia kutetea huu muungano DHALIM.
 
...Mie jina tu la Tanesco la ni chefua!,utafiti niliofanya ni kuwa watz wengi maskini sb hawana umeme! kamata hilo kama unabisha ingia kwanye study
 
Tunazihitaji sana tena sana ili yawe majibu kwa wote wanaosena ZNZ inatumia umeme wa bure!

Pia utawaumbua wale wachumia tumbo wa CCM ZNZ wanaosema faida moja ya muungano ni Zanzibar kutumia umeme bure! Leo uongo wao umefika kikomo watafute chaka jengine la kujifichia kutetea huu muungano DHALIM.
una point. hao akina vuai shamsi na akina seif khatibu ni viongozi njaa. kaeni nao mbali.
 
Nafikiri amekata mzizi wa fitina wa wale wachache wanaleta ulaghai kuwa ZNZ HAILIPI UMEME au wengine hata kuse TGK INAWALIPIA UMEME ZNZ Hongera Maswi
Nadhani hamjui tatizo hili. Kama mtakumbuka hivi karibuni wakati wa bunge la katiba, SMZ imeamriwa kuanza kulipa umeme wake. Hiyo ni baada ya kubainika kuwa bilioni 20 za TANESCO zimetafunwa. Aliyetoa amri ni JK kwa taarifa yenu. Chanzo kilikuwa ni gharama za tume ya Warioba ambapo wznz walikataa kwa kusema ni jambo la muungano. Hata BMLK wznz wanalipwa na SMZ na ni kuanzia hapo ikaagizwa waanze kulipa deni lao. Si zaidi ya miezi 3. Deni la nyuma lipo na ni zaidi ya 1/8 ya mapato ya znz.

Hiyo haina maana kuwa znz imeshalipa deni lake la umeme. Maswi kasema ni la zamani .
TANESCO wanaidai znz zaidi ya bilioni 67 za malimbikizo kwasababu haikuwahi kulipa huko nyuma.

Kumbuka Maswi wa Escrow si TANESCO,ndipo mgongano ulipo.
Tanesco wanadai pesa zao zaidi ya biloni 67 kwasababu tangu umevushwa znz hawajalipa.
Watawezaje kulipa umeme ukiwa hawawezi kulipa mishahara?

Hizo milioni 500 ni kauli za kisiasa za kuondoa wingu tu lakini ukweli unabaki kuwa hawalipi na hawajawahi kulipa
Waziri wa fedha Omar mzee aseme walianza lini.

Mnadakia habari msizo na ufahamu nazo.

Kwanini iwe flat rate ikiwa matumizi yanabadilika. Hilo hata hamfikirii. Kwanini znz ilipe flat rate kama inalipa kweli.

Hakuna sababu za kulumbana, ombeni mamlaka kamili mlete umeme wa melini kama zamani.
Si mnajua znz ndio nchi ya kwanza kuwa na umeme na TV ya rangi. teh teh teh teh
 
..kukata mzizi wa fitina Tanesco iachane na biashara kichaa ya kuuza umeme Zanzibar.

..Zanzibar wanunue umeme toka Kenya, wa-Tanganyika tumechoka na migogoro isiyokwisha.

cc Nguruvi3, RockSpider
 
Last edited by a moderator:
Bahati mbaya wanalazimishwa kununua umeme wa bei ghali kulipia gharama kubwa za majizi IPTL, AGRECO, SYMBION na SONGAS...
wanalazimishwa na nani? Walete meli kama zamani, au waende kununua kwingine. period.
 
..kukata mzizi wa fitina Tanesco iachane na biashara kichaa ya kuuza umeme Zanzibar.

..Zanzibar wanunue umeme toka Kenya, wa-Tanganyika tumechoka na migogoro isiyokwisha.

cc Nguruvi3, RockSpider
Kumbuka deni la bilioni zaidi ya 40 limekwenda kwa maji. Aliyefidia hasara hiyo ni Mtanganyika. Na inakuwaje wanalipa milioni 500 sasa hivi? Unawezaje kutumia umeme katika rate constant kama hiyo.
Ikiwa umeme uliotumika Pemba uligharimu SMZ milioni 800 kwa mwezi, iweje Pemba na Unguja watumie milioni 500 kwa mwezi?

Hapa ni politics tu za kumtwisha Mtanganyika mzigo zaidi. Naunga mkono, Tanesco haina sababu za kuingia katika malumbano na wazanzibar. Iachane na bishara hiyo, wakanunue wanakotaka.

Haya yote yanaletwa na ukweli kuwa hakuna Tanganyika. Nani atasimamia rasilimali za Tanganyika?
Deni wanalosema limemezwa na JMT ambayo kwa uhalisia limemezwa na Tanganyika.
Tunaendelea kuwakamua watu wetu kwa sababu gani?

Znz ni nchi na kila kitu, wanaweza kufanya maamuzi ya kununu umeme watakako. Mbona mafuta na gesi waliondoa.

Tunapoteza muda sana kulumbana na hawa wznz kila siku. Hakuna tunachopata lakini tupo tu katika malumbano.
Ali Keissy alisema njia nyeupee, hawataki wanasema wanalazmishwa kununu umeme!
 
"Kwanza niwaambie (waandishi wa habari),deni hili ni la zamani sana ila ,SMZ imekuwa ikilipa kila mwezi na hata hivi sasa tumepokea shilingi milioni 500 za malipo ya umeme kwa Zanzibar tu," alisema.

"Nawaambia mkawaambie wote wanaosema kwamba Zanzibar inadaiwa na TANESCO kuwa huo ni uongo na kama mtu hajafanya utafiti hana haki ya kuzungumza," alisema.

Huyu Maswi mbona anakuwa na akili kama za kamanda Kova?! (akili za makengeza) Kwanza anakiri kwamba TANESCO inaidai SMZ, lakini deni lenyewe ni la zamani?! Statement inayofuata anasema kwamba Watu wote wanaosema TANESCO inaidai SMZ ni waogo!! Hivi nyinyi waandishi wa habari huwa mnaweka wapi akili zenu kiongozi anapotoa two contradictory statements at the same time. Bora hata Kamanda Kova ambaye huwa anasubiri hata siku moja ipite kwanza ndio ajichanganye. Halafu mhariri wa gazeti hili anakubali utumbo kama huu kuuchapisha. Kama ningekuwa mimi ndiye mhariri ningemrudisha huyo reporter kwa Maswi akauliza this simple question Je, SMZ inadaiwa na TANESCO, jibu ni NDIYO au HAPANA it can't be both at the same time kama alivyofanya Maswi.
 
Back
Top Bottom