mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Rais Zelensky wa UKraine na mataifa ya magharibi kwa ujumla wanashangilia sana majeshi ya ukraine kuingia kwenye mji wa kherson wakidai wameukomboa. Lakini ukweli ni kwamba hawajaukomboa ila majeshi ya urusi yalitangaza kitambo kuwa yatauachia mji huo. Kwanza Ukraine wal;ikuwa hawaamini kama urusi ni kweli imeamua kuuachia mji huo na walikuwa wanadhani ni mtego wa warusi. Hii ni kwa sababu majeshi ya ukraine yalikuwa yamefanya majaribio mengi ya kuukomboa mji huo bila mafanikio na yaliingia hasara kubwa sana ya kuuliwa askari wake wengi na vifaa vya kijeshi kuharibiwa katika majaribio hayo. Kwa mazingira hayo ilikuwa ni vigumu kwao kuamini kuwa urusi iliyokuwa imefanikiwa kuulinda mji huo usikombolewe leo inaamua kuuachia "bure" bila kufurushwa kwa nguvu za kijeshi.
Urusi iliamua kuuachia kwa kuzingatia hali halisi ya kijiografia na kuzingatia malengo yake ya muda mrefu. Kiasili jimbo la Kherson limegawanywa katika sehemu mbili zilizotenganishwa na mto. Mji wa kherson uko upande wa magharibi wa mto na upande huo una asilimia 30% ya jimbo la kherson. Upande wa mashariki mwa mto huo kuna asilimia 70% ya jimbo la Kherson. Sehemu hizo mbili zinaunganishwa na madaraja. Katika hali ya kivita madaraja hayo yalikuwa yakishambuliwa mara kwa mara na kuharibiwa na kugharimu kutengeneza madaraja ya muda. Kwa malengo ya muda m,refu ni vigumu kujihakikishia usalama kwa walioko upande wa magharibi ikiwa ni pamoja na uhakika wa kuweza kusafirisha silaha kubwa kubwa upande huo. Ndio maana urusi iliwataka raia wahame maeneo hayo na wengi walihama japo kuna wachache walibaki.
Mfano mzuri ni mto Ruvuma unaotenganisha Tanzania na Msumbiji na tunaunganishwa na daraja. Kama (Mungu apishe mbali) ikitokea tukapigana na Msumbiji kisha tukateka sehemu yao, kazi yao ni nyepesi nayo ni kulivunja tu hilo daraja kwa mabomu na hatutaweza kuwahudumia vizuri wanajeshi wetu walioko huko. Mto ni mpaka wa asili na watu hulazimika kuuheshimu, usipouheshimu huko mbeleni unaweza kuadhirika. Ndivyo alivyoamua Urusi kuwa inabidi arudi nyuma na kujiimarisha upande wa mashariki mwa mto. Hali kadharika Ukraine hata akifanyaje hawezi kuvuka mto akakomboa sehemu iliyo mashariki mwa mto huo! Hapo patakuwa hivyo miaka nenda rudi.