Sa
Sababu za Urusi kuitandika Ukraine ziliwekwa wazi:
1. Kuizuia Ukraine isijiunge na NATO. Na hilo limefanikiwa!! Nato wenyewe hawana ubavu wa kukubali ombi hilo la ukraine.
2. Kuinyang'anya silaha Ukraine. Jambo hilo lilishafanikiwa. Silaha zote alizokuwa nazo ukraine karibu zote ziliharibiwa. Ukraine inategemea silaha za kupewa na NATO kila leo. Kama NATO leo wakisema hatupeleki silaha ukraine, ukraine itabaki mikono mitupu.
3. Kukomboa majimbo mawili mashariki mwa ukraine yajulikanayo kama DONBAS. Hilo limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90, na muziki bado unaendelea kumalizia asilimia zilizobaki.
4. Kuangamiza askari wa kinazi, Hili lilifanikiwa maana askari wa kinazi ndio waliokuwa wamejichimbia pale Mariuop. Waliuawa wengi na waliobaki walitekwa!!
MAFANIKIO YA ZIADA:
1. Majimbo mawili kusini mwa ukraine yametekwa na tayari yameshajiunga na urusi. Hii imesababisha kuunganisha Crimea kwa ardhi tokea urusi!! Hii asilimia 30% iliyoachiwa ni mkakati wa kijeshi tu kutokana na mpaka wa asili wa mto!
Hakuna hata moja lililofanikiwa
1. Ukraine ilipeleka tena ombi la kujiunga NATO baada ya Russia kufanya upuuzi wake wa Referendums kwenye ardhi ya watu. Ili ujiunge inahitajika nchi zote 30 zikubali,sio kwamba unajiunga tu kama unajiunga na kikundi cha bongo movies.
2.Demilitarisation
Nayo pia haijafanikiwa maana kwa sasa Russia ndie moja ya wachangiaji wakubwa wa silaha kwa Ukraine wakifatiwa na mabeberu. Kila ambako Russia hua anakimbizwa hua anaacha masilaha kibao ambayo yapo kwenye state nzuri ya kutumika tena mfano vifaru vya kisasa T-90 Ukraine ilividaka kule Kharkiv na sasa wanatumia dhidi ya Urusi wenyewe. Plus Ukraine bado ina stock ya silaha zake za Soviet mfano bado inatumia Grad missiles mpaka Leo,Buk Sam,S-300,Sam,ina Makombora yake ya kuzamisha Meli Neptune.
3. Majimbo ya Donbas nako hakuna hayo mafanikio ya 90%.
Kumbuka mji pekee ambao Russia ilikamata wote ni Kherson ambao ulidakwa mwanzoni mwa Vita. Huko Donbass Russia anashikilia 50% na Ukraine 50% sasa unasemaje ni mafanikio ya 90%?! Tena hiyo 50% hapo kuna maeneo alikua akiyashikilia kabla ya Vita kuanza. Luhansk Ukraine imekomboa baadhi ya vijiji na wiki hii wamekomboa tena 12 settlements,na kazi inaendelea.
Zaporizhzhia pia Russia hajaikamata yote mwezi wa 9 huu tunaelekea wa 10.
4. Moja ya propaganda ya Russia kuvamia Ukraine ni kuondoa Unazi,lakini cha ajabu tumeona kwenye mabadilishano ya wafungwa Russia imeachia hao iliowaita wanazi kibao ambazo wamerejea Ukraine. Sasa unasemaje unaangamiza unazi halafu unawaachia huru wanazi wenyewe?![emoji1745]
5. Hiyo Kura ambao ilipigwa ya maeneo kujiunga Urusi haitambuliki kimataifa ni North Korea na Urusi wenyewe pekee ndo wanatambua hata swahiba wao China na India hawatambui huo upuuzi. Hayo maeneo yamejiunga na Russia kwenye makaratasi ndio maana mpaka Leo bado yanashambuliwa na Ukraine na hakuna kitu Russia anafanya maana hata yeye anajua si sehemu yake halali.