Umeongea na kutoa povu sana., Zelensky anasema hatamuachia Mrusi hata Inch 1 kwenye ardhi yake, ndio mana Ukraine inapigana kupambania taifa lao, halafu inaonyesha hujui chochote kwenye hili sakata, Zelensky akisema akubali masharti ya Putini maana yake eneo kubwa tena la kiuchumi akubali liwe sehemu ya Urusi, mfano kule kwenu Tanzania mulikuwa tayari kupeleka majeshi na kupiga na Malawi kwa sababu Malawi walisema lile ziwa Nyasa ni la kwao kwanini sasa mlitaka kuanzisha vita? kwanini?
Ukrean ni Taifa kama ilivyo Tanzania, wana katiba yao, jeshi lao, na kila kitu chao ni nchi yenye mamlaka yake kamili kwanini walazimishwe masharti kutoka nchi nyengine huru ambayo na wao wana maamuzi yao kule na rais wao., enzi za utumwa zimeisha kama wewe bado ni mtumwa hapo ulipo siyo kila mtu na kila nchi
Wacha wapambane mpaka Mrusi atakapomaliza kufurushwa kabisa kabisa na kurudi kwao kama alivyofurushwa Kyiv na kurudi zake Donbas