Ziara ya Rais Samia nchini China yazaa matunda mapema sana

powercert_Tz

Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
45
Reaction score
44
Baada ya ziara ya Rais Samia nchini China, 98% ya bidhaa kutoka Tanzania kwenda China zitaingia bila kutozwa ushuru. Hii itatoa fursa kubwa kibiashara kwa wakulima, wafugaji na wafanya biashara wetu kulisha soko jipya la China.

China inaidadi kubwa ya watu kuliko nchi zote duniani hivyo hii ni fursa kubwa sana kwa wafanya biashara wa Tanzania. #mamayukokazini
 
Siamini Macho Yangu....!

Maharage Na Yenyewe Yamekuwa mboga ya Anasa?

Eti 'Kilo imepanda Kutoka 'Afutatu' mpaka 'Afunne'...!
 
Kwa hivyo sasa hv wachina watatulisha vitu fake kiulaiiini zaidi eeh
 
Bidhaa zipi hizo?

China ni socialism with capitalism based mode of economy, elewa no free lunch pamoja na mikopo Tunayopata kutoka china, lakini pia wamejihakikishia kandarasi za wahandisi wao kwa kazi nyingi za ujenzi wa miundombinu na vitu mbalimbali ambapo bado nchi yetu inajengwa hivo huko mchina atavuna mabilioni ya pesa hivo kukupa njia ya wewe kuingiza bidhaa hasa za kilimo kwake free sio kesi maana kwanza kajihakikishia uwezo wa kupata chakula na matunda kwa watu wake ambapo watanunua kwa bei nafuu na hiyo ni kutokana na china kua na uhitaji mkubwa sana kwani ana idadi ya watu 1.48 bilioni yeye pekee hawezi kujitosheleza hivo changanya na wingi wa viwanda anahitaji pamba, ufuta, kahawa, chai, tumbaku, mchele, mahindi, maharagwe, nguruwe, na matunda kama parachichi lakini pia Soya, sasa yeye alishapiga hesabu wapi anavuna zaidi kwanza kwenye kandarasi lakini pia wewe ni soko la bidhaa zake, hivo unaongeza ajira kwake, unacheka unadhani umepata soko kumbe mchina anakucheka amekuibia kwa lugha laini kabisa.
 
Hivyo mitazamo ya viongozi wetu wa kiafrika ambayo iko shallow haiwezi kujiongeza kiasi hicho, kufahamu maslahi mapana ya vizazi vyake
 
Ahsante! kikwete aliwai kusema ukitaka kula inabidi nawewe uliwe kidogo je wametula Nini kidogo baada ya sisi kutaka kula??πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Ahsante! kikwete aliwai kusema ukitaka kula inabidi nawewe uliwe kidogo je wametula Nini kidogo baada ya sisi kutaka kula??πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Wachina wanashika kandarasi nyingi sana za kujenga miundo mbinu ya uchukuzi hapa nchini, hivyo kuruhusu bidhaa zetu kuingia free kwenye nchi yao ni faretrade. Tanzania ni tajiri sana katika sekta ya kilimo hivyo wanalenga kupata mazo mengi ya chakula kutoka kwetu of which ni fursa kwa wakulima wetu.
 
Viema mkuu
 
Tangu lini China ilikuwa ikikata kodi kwa pembe za ndovu na nyara zingine za Serikali zinazoingia nchini humo? Tusidanganyane!
 
Naunga hoja mkono. Piga kazi mama tumecheleweshwa mnooo kama taifa zaidi ya miaka 7
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…