Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Vipi wakiifanyia biashara na kuunza kuuza nje ya nchi kupitia mombasa port?...
Ndio utajua Tanzania ni ajabu kama mtu unamuuzia kitu yeye anaeenda kuuza na Mteja anaona bora aende kwake kuliko kuja kwenye source.
Maana kwa sasa ilivyo mfano kwenye nyama, kuchinjia Mbuzi Tanzania ukasafirisha ni ghali kuliko kuwapeleka Kenya ukawachinja na kusafirisha nje

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Hata hizo malighafi zinapozalishwa zinatengeneza ajira nyingi tu. Sio lazima ajira ipatikane katika value addition ya malighafi.

Unapouza malighafi ya zao fulani unatengeneza ajira kwanza katika sub sector hiyo hiyo maana wazalishaji wataongezeka, pili ajira katika sub sectors zingine zitaongezeka pia kwa mfano katika vifaa vya kufungashia kama magunia, kamba, cello tape, maboksi; pia wabebaji, wafungaji mizigo, wasafirishaji, clearing & forwading, gesti zitapata wakaaji kwani wanunuzi wa malighafi watalala humo wakati wakifanya manunuzi, bia na vyakula vitauzwa kwa wingi, malaya watapata soko zaidi, saluni za kuwapamba wanaojiuza kwa wanunuaji wa malighafi zitapata wateja zaidi nk. In short, unaweza kuuza malighafi lakini ukatengeneza ajira zinazotokana na viwanda katika sub sectors zingine kabisa.

Kanada pamoja na kuwa na viwanda lakini wanamuuzia Bakhresa ngano na yeye anaileta na kuichakatia hapa Dar, New zealand na Australia wanauza sana hizo unazoita malighafi nje, hata Sweden wanauza sana mbao laini ikiwa malighafi.

Huwezi ukazalisha kila kitu wewe mwenyewe kwanza huna comparative advantage , nani atanunua bidhaa yako ambayo ni ghali kuliko bidhaa kama hiyo toka nje ambayo ni rahisi? Viwanda vya ndani vinakabiluwa na utitiri wa tozo na kodi kama Osha, zimamoto, kodi ya huduma za jiji nk in addition to traditional taxes plus bei kubwa ya umeme na rushwa wanazodaiwa na wakaguzi wanaopita viwandani kwa kigezo cha kukagua compliance mbali mbali; imagine mkaguzi anathubutu kudai rushwa ya hadi milioni mia mbili! huyo mtu atauzaje hiyo bidhaa?

Unapozuia mkulima asiuze mazao yake kwa kisingizio cha kuyaongezea thamani unamuumiza huyo mkulima. Inachotakiwa huyo anayenunua malighafi na huyo mwenye kiwanda washindane kununua kwa bei na mkulima aachwe amuuzie anayemtaka. Mambo ya kuyaongezea thamani hayamhusu mkulima kwani yeye amelima ili apate bei nzuri. Jiulize hivi kama mtu toka nje anaingia gharama za kuyasafirisha hadi kwao wakati kiwanda hakina gharama za usafiri lakini bado huyo aliyenunua malighafi akaipeleka kwao kisha akatengeneza bidhaa na kuisafirisha kuileta Dar na bado akaiuza rahisi kuliko wewe wa kiwanda cha dar usiye na gharama ya usafiri basi wewe ni highly inefficient producer hivyo kiwanda chako bora ukifunge tu.
 
Hilo liswahili lako limeshapigwa!

Chezea Kenyatta wewe!

He is a business-oriented politician, sio kama huyo kikongwe wa pwani.

Ndio maana wakenya wanamchekea usoni na kumzoza kisogoni maana wanajua wameshapata GOIGOI la kulichuna.
Yaani nyie shombo ya lumumba ni shida kwelikweli.. mnadhani MEKO mshamba wenu atarudi? hata mlieje harudi ng'ooo wacha sasa tucheze wimbo
 
Inaonesha una hofu zaidi. Nategemea utaleta ufumbuzi wa kutatua changamato ulizoona.

Awali ya yote tukumbuke mfumo wa uchumi tulioanza nao mara baada ya kupata uhuru na wenzetu walianzaje.

- Ujenzi wa bomba la mafuta kuwezesha Kenya kuzalisha bidhaa zaidi. Hapa tujiulize kwa nini wataweza kuzalisha na kuuza kwa bei nafuu. Kinachotakiwa kufanya ni kuweka bei ya ges chini kuliko Kenya hivyo wawekezaji wa nje wataamua kuwekeza Tanzania badala ya Kenya kutokana na unafuu huu.

Tena kuna uwezekano mkubwa kwa Kenya kununua gas kutoka Tanzania na kuiuza nchi za nje. Kwa sababu wao wana bandari bora kulinganisha na Mtwara na ni karibu na masoko. Sehemu kubwa ya gas yetu tulitegemea wawekezaji wauze gas hiyo nje kuliko hapa kwetu kwa vile matumizi yetu ya gas yako chini. Na ndio lengo kuu, isipokuwa kuna mahali tumezubaa na wenzetu wanatumia fursa. Na uwezekano wa kuuza gas yetu nje kupitia Kenya upo pia.

- Sera ya viwanda haiwezi kufa kama itasimamiwa kwa ukaribu. Kuna wawekezaji zaidi ya 500 kutoka Kenya. Inaonekana wamevutiwa kwa wingi kuwekeza kwetu. Usiogope, sera yetu ni kuvutia wawekezaji kutoka nje, lakini kwa vile ni Wakenya tunatishika, hatutishiki kwa Wachina, sawa Watanzania waliowekeza Kenya ni wachache, je Watanzania wangapi wamewekeza China?

- Kuhusu Kenya Airways ku dominate soko la Tanzania ni swala la mikakati tu. Waliweza ku dominate soko kwa vile hatukuwa na ndege. Air Tanzania nayo ifanye mikakati kutafuta masoko, mamlaka za viwanja vya ndege na washirika wake watoe huduma nzuri kwa wateja na kutafuta njia mpya. Tujifunze kutoka kwao, shirika lao pia linaendeshwa kwa hasara pamoja na kuwa wabia na KLM.

- Soko la utalii. Tumegundua kwamba tatizo letu ni kujitangaza. Kwa kipindi hiki tumejitangaza sana na tunaendelea kufanya hivyo, hata klabu kama Simba imeona umuhimu huo na kutakuwa na impact. Tuendelea kuimarisha viwanja vya ndege kuwezesha ndege kubwa kutua ili watalii wafike moja kwa moja Tanzania badala ya kushukia Kenya. Kwa mfano upanuzi wa viwanja vya ndege vya Songwe Mbeya na Iringa vitawezesha watalii kufika kwa urahisi katika mbuga za Ruaha, Kitulo, Katavi, Udzungwa nk. Watalii wengine hawapendi kwenda sehemu moja miaka yote, hivyo ni nafasi kubadili kutoka Kenya na Ukanda wa kaskazini na kuhamia Kusini

Nchi kama Dubai haikuanza na viwanda na sidhani kama kuna viwanda vingi, lakini mazingira rafiki yamepafanya kuwe kitovu cha biashara, hivyo kwa bidhaa za Kenya pia tunaweza kuwa kitovu cha biashara kwa bidhaa za Kenya kwenda nchi kama Afrika ya Kati na kusini. . Mbona bidhaa kutoka China zinanoingizwa na Watanzania pale Kariakoo zinanunuliwa na wafanyabiashara kutoka Kongo, Zambia, Burundi n.k? Hakuna kisichowezekana.

Kimsingi tuondoe hofu, tutumie fursa tulizonazo.
 
Mwanamke huongozwa na mwanaume! Eti leo hi mwanamke anaongoza wanaume zaidi ya milion, kadili muda unavyozidi kwenda tutegemee kufeli zaidi.
Kule Ujerumani wanongozwa na nani ?, nyie masalia ya jiwe mnahaha sana nyakati hizi
 
Mkuu Capable God, nimekuelewa juu ya wasiwasi wako, lakini fikiria katika hali ya kawaida ambayo haitaji elimu secondary, ukiwa na ziada (surplus ) ni lazima uuze ili ukidhi mahitaji yako. Kuhusu Kenya kununua na kufanya processing ya ges waliyonunua ni ku-value ili waiuze kwa faida. Sisi nasi inabidi tufanye hivyo hivyo (kui-value) ili tuiuze kwa faida pia. Jiulize, kama Kenya wamenunua ges kutoka TZ na wazaiuzia TZ na WATZ wakanunua ges hiyo na kuacha kununua ya kwao ambayo hawakuinunua bali ni zawadi kutoka kwa God, jua kuwa kuna tatizo mahali. Kodi yetu ya VAT inatufukarisha sana, yaani kila ununuacho. Hivi hiyo 18% ya VAT hawezi kupunguzwa?
 
Waliogundua ni kina nani na waligundua lini?

Rangi ya dhahabu/njano kwenye bendera yetu inawakilisha nini?

Ndio uzuri wa siasa zetu. Hawa wawekezaji watakuja kweli? Mtu awekeze hela zake halafu akipata ndio tunasema cha kwetu. As if yeye hana share
 
Sasa mabo ya ardhi yameingiaje
hapa?

Nani kasema wakenya waje wapewe ardhi yetu? Mbona mnapenda kupotoshapotisha mambo?

Mbona mnakuwa wajuaji wa kupitiliza?

Mama anawashauri wa kutosha kwenye nyanza zote,hivyo maamuzi yake yanakuwa yamezingatia ushauri wa ktaalamu na masilahi ya taifa.
 
Soma, tambua bidhaa & huduma kutoka Tanzania kwenda Kenya au kinyume chake, utaona.
Hapana.
Hakuna hayo unayoelekeza niyasome katika hiyo "competitive advantage" uliyoandika pale. Haipo kabisa.
 
Mwanajamvi....ninapofanya analysis unasema ujua.....hiyo ni analysis

Kwenye uwanja wa siasa one action can lead to many impacts....hii ni siasa

Na hili la ardhi ni mfano...na hii imetokana na alichosema rais wa keny....kauli yake ile inashiria kuwepo free enter out,free access of resources btn zis contries...kitu ambacho hakina afya yote kwa Tz


Unaowaita washauri wataalamu ni binadamu kama wew....na aimaanishi ndo only professional nchi nzima.... ndo mapana kukawepo platform kama hizi......jomba umenipata
 
Nitage ukijibu.. .okeee
 
Nasikia gesi yenyewe sio yetu acha iende.
Maana kwa akili ya kawaida nilitarajia kucover viwanda vya ndani ndio iende nje.
Yajayo yanafurahisha
 
Hata monopolistic competition inaanza baada ya competition ya ndani kuwa kubwa ndo tunatoka nje kutafuta profit
Swali la kujiuliza je "Tanzania kunahiyo competition ya kibiashara mpka kufanya rasilimali kuwa ndogo na kupelekea faida ndogo ili tuanze kuwekeza nje??"
 

Mlizoe kubebwa mkisikia ushindani mnachanganyikiwa. Nchi hii imejaza bidhaa za China madukani, mbona hilo haliwaumi, au tatizo lenu ni wakenya ambao ni waafrika wenzetu?
 
Ndio uzuri wa siasa zetu. Hawa wawekezaji watakuja kweli? Mtu awekeze hela zake halafu akipata ndio tunasema cha kwetu. As if yeye hana share
Haya mavitu yaliyoka ardhini yalishajulikana siku nyingi kabla hata ya 9 Dec 1961 na ndio msingi wa rangi ya njano kwenye bendera. Hawagundui, wana-extract na kutumia mikopo ya kudhaminiwa na serikali yetu wenyewe au kupewa mikopo hiyo na mabenki yetu hapa.

Akope kwao, awekeze hapa, faida tu ndo aruhusiwe kupeleka kwao. Sasa anakopa hapa, uendeshaji wa kampuni unafanyikia kwao, malipo yanafanyikia kwao, mauzo yanafanyikia kwao, ni akili ya wapi hii?

Wanywaji wana uwezo wa kuweka vinywaji ndani ila wa apendelea kufuata vinywaji bar, vivo hivyo kwa bidhaa adimu, unadhani ipo siku mwarabu atazuiwa kuza mafuta soko la dunia? Au sisi tutasubiri mchina alete maronyaronya yake hapa ndo tununue?
 
Mlizoe kubebwa mkisikia ushindani mnachanganyikiwa. Nchi hii imejaza bidhaa za China madukani, mbona hilo haliwaumi, au tatizo lenu ni wakenya ambao ni waafrika wenzetu?
Kisha ni hao hao watakao payuka humu vile wao ni pan -africans.

Kweli 🇹🇿 Imejaa viatu
 
H

Ii project ya kupeleka gesi Kenya ni ya muda mrefu watu walichelewesha kufanya maamuzi. Bora uamue kuliko kukaa kimya na kuchelewesha mambo.
Toka lini Mkuu? Enzi za JK au? I smell Rostam yuko ndani????!@@@!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…