Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Anafungua nchi hata visivyotakiwa kuingia viingie?
Mama fungua nchi tupate maendeleo, Mwendazake alichezea sana hii nchi ilikuwa kama shamba lake anavuna apendavyo au kama zoo yake binafsi anajipigia tu apendavyo... Alituchelewesha sana kupata maendeleo
 
Hoja nyepesi, viwanda si lazima viwe Dar tu, itengenezwe distribution network kwa nchi nzima halafu ndio lije swali la ULIIFANYIA NINI.

Peleka bomba magharibi watu wakatumie chillers kuhifadhi samaki, peleka kaskazini na kusini, weka provision kila mkoa, fanya makadirio ya matumizi yake, kisha tuambie tunao uwezo wa kuuza kwa nchi jirani baada ya kukidhi mahitaji yetu.

Kuna watu walitaka wazalishe umeme, serikali iwajengee transmission line ya kuupeleka umeme huo Kenya kwa mauzo, hiyo ni miaka 8 nyuma, na mwenye akili hiyo ni mtanzania kiongozi.
Wakenya wao wameomba tuwapelekee gesi lakini hii haizuii hiyo gesi sisi kuipeleka huko unakosema..

Mbona mnashindwa kutumia akili japo kidogo tu??

Yaani mimi nina shamba la ekari mia, Ila kwa sasa uwezo wangu ni kulima ekari 10 tu, aje mwenzangu mwenye uhitaji atake nimuuzie ekari 10 ambazo kimsingi zitaniwezesha kupata pesa ya kulima ekari zingine 50 nimkatalie??

Bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Kinyerezi unajua gharama zake?? Sasa unavyosema eti tulipeleke kila kona ya nchi hii unadha ni shughuli ndogo??
 
Mshauri wake wa masuala ya kiuchumi ujue ni mhitimu wa Harvard mkuu.
 
Unaandika vizungu viiingiii ushuzi mtupu!

Monopolistik sijui manini nini!

Uhuru Kenyatta ni mjanja wa mjini yule.

Kashampiga bao Bibi SASHA.
Kwahiyo ulitaka mama aende kwa Kagame ili awe Rais wa maisha? Hivi ule Mpango wa kuongeza miaka ya uongozi umeishia wapi!?
 
Sioni sababu ya kuzua gesi isiuzwe eti kwa ajili ya kulinda viwanda hii roho mbaya
Mambo ya kulinda viwanda vipi...hivi viwanda vya maji?? Rekebisheni productions costs za bidhaa zenu, siku zote zinakuwa juu kuweza kucompete na bidhaa toka nje. Mamake utashangaa pale tutakapowauzia gesi Kenya, lakini baadae wataweza kuproduce bidhaa zenye quality na kutuuzia at a cheaper price than as compared to our products...mambo ni mengi,tusitafute mchawi na ndio global business ilivyo.
 
Hilo la gesi mimi wala sina shida nalo kama gesi tunayo ya kutosha.

Ila nilipoona kuna mikataba ya mambo ya anga na utalii nikasema basiii
 
Nchi imeshawekea umeme wa hydropower ambao utakuwa bei chee na uzalishaji ukianze tunabaki na more than twice the capacity ya matumizi ya nchi.

Ina maana uwekezaji mwingine mpya wa kuzalisha nishati baada ya Nyerere Dam kukamilika ni matumizi mabaya ya hela labda mpaka baada ya 10-15 ijayo nchi itakuwa imefikia matumizi ya megawatt 4000.

Mazingira yote hayo mazuri bado ulalamike Gas kuuzwa nchi jirani, isitoshe Kenya bado inabidi wajenge bomba, wajenge kiwanda cha kuzalisha umeme wa gas, network ya kusambaza Gas Kenya na uwekezaji wote muhimu ili kunufaika na Gas.

By the time wakenya wanafanya uwekezaji wote huo; mfanyabaishara wa Tanzania kama bado ajanufaika na mazingira aliyonayo hilo sio tatizo la Kenya tena.

Gas lazima iuzwe kama kuna njia rahisi ya kufanya hivyo sio mpaka tusubiri mabeberu yatujengee LNG plant yakinyonyaji,.

Besides kwa Kenya kununua Gas yetu kwa matumizi ya uchumi, inatupa regional dominance siku wakitizungua sijui wamezuia mahindi mpakani kuingia Kenya tunafunga tu bomba la Gas, chamoto watakiona uzalishaji wote unaotegemea Gas huko kwao unasimama lazima wapige magoti yaishe.

Issue labda hiyo mikataba mingine.
 
Huyu Mama anatufanya sisi wajingaaaaa... kumbe tunamwangalia tu akili zake zinapofikia

Eti takwimu za uwekezaji wa Kenya hapa kwetu kazitaja kwa dola na idadi ya miradi

Takwimu za uwekezaji wa Tanzania nchini Kenya kazitaja kwa trilioni za shilingi ya Kenya na idadi ya makampuni

Yani vitu vinne tofauti, makusudi kabisa ili kutuchanganya tusiweze kulinganisha...
Hebu tupe takwimu zako..!!
 
Sioni sababu ya kuzua gesi isiuzwe eti kwa ajili ya kulinda viwanda hii roho mbaya
Roho gani mbaya wakati akina Dangote walinyumwa gesi na ni viwanda vya ndani sasa hapo unatengeneza mazingira gani kwa viwanda vyetu.

Yani unamnyima dangote unaenda kumpa mkenya, this is nonsense!
 
Sioni sababu ya kuzua gesi isiuzwe eti kwa ajili ya kulinda viwanda hii roho mbaya
Mtoa Mada naona hajatizama hili jambo kwa upana. Kwanza anasema unauza Gas bidhaa zao zitakuwa rahisi sasa viwanda vyetu wanashindwa nini kutumia hiyo Gas na bidhaa zao ziwe rahisi na pia sisi tunauza Gas sio kutoa msaada. Mambo ya ndege Air Tanzania haishindani na Kenya soko ni kubwa na kila mtu anashindana kama unaona Kenya huiwezi sasa hao kina Qatar, Emirates, Flydubai na Ethiopia ukiondoa Emirates wote wanatua kilimanjaro ila ameona Kenya airways tu, hawa wanaleta watalii kama humtaki Kenya wakatae na wengine. Dubai wana mandege kibao lakini ndege za nchi nyingine zote zinatua kwao sijasikia wakisema tunazo ndege za kutosha hatutaki ndege zingine. Tatizo kubwa sisi tunaogopa sana ushindani dunia hii biashara ni ushindani unadhani Fast jet tungewaacha wakashindana na Air Tanzania na bei zingeshuka kwa faida ya mteja ila wakawaondoa ili bei wa control.
 
Roho mbaya haijengi, kwa hiyo kama watanzania mambo ya viwanda yametushinda si bora kuwauzia huo umeme wa Kenya, hiyo gesi ikaleta faida kwetu sote.

Mrusi anawauzia mpaka mahasimu wake washirika wa NATO gesi, Ukraine mpaka Ujerumani, ni biashara, siasa za east na west anaweka kando. Hawazii ooh watakuwa na umeme wa kulisha mitambo ya kuzalisha makombora. Lakini anakuwa na LEVERAGE, wakizingua anafunga gesi.
Huoni na sisi tutakuwa na LEVERAGE na Kenyans, wakizingua tunakata STIMA?
Fikiria kibiashara, zamani enzi za falme, ilikuwa ili kumaliza shindani na uhasama, basi wana wafalme wa falme 2 tofauti wanaoana. Gharama za vita zinaisha.

Hata sasa kuna bwawa la umeme linajengwa, huko Kagera mitambo kwetu SWITCH zipo kwa Kagame, hii ni katika masuala pia ya kiusalama ya maziwa makuu, na East Africa.

Think of a bigger picture..

Etveryday is Saturday..............................😎
 
CCM hamna lolote huu ni mwaka 60 kutawala kula la maana?
 
Unaandika vizungu viiingiii ushuzi mtupu!

Monopolistik sijui manini nini!

Uhuru Kenyatta ni mjanja wa mjini yule.

Kashampiga bao Bibi SASHA.
Mama ana sign tu na kupitia kuna wataalamu wa kiuchumi na wanasheria wanatengeneza mikataba mama ana ridhia kwa kuangalia faida na hasara ya mkataba.
 
Kinacholalamikiwa ni viwanda vya ndani kunyimwa gesi halafu unaenda kumpa mtu wa nje, kwani ukatumia hata 1% tu ya ubongo wako, utapungukiwa na nini?
Unauza nje unataka $ sio Tsh. Viwanda gani vilinyimwa na kwa sababu zipi lazima tuwe specific sio kuongelea kiujumla tu.
 
Hapo umekosea sana maendeleo yanatokana na sera na sheria za Nchi ktk uwekezaji,kodi na feza, kama Tz inaiuzia kenya gasi na wanazalisha bizaa na kuziuza kwa bei ya chini kuliko za TZ basi tatizo ni la viongozi wa Tz, wanaoweka kodi Kubwa na uzembe.

Utalii TZ ina vivutio vingi na vizuri kuliko kenya tatizo TZ, ni makodi makubwa kwa mfano kenya hakuna VAT kwenye utalii TZ wana 18% kenya wameshusha viingilio,gharama za kutua ndege, wametoa tozo ya kupaki Ndege, kenar wametoa na kusame kodi kwenye makampuni ya utalii sababu ya covid -19, ili makampuni yasife, Wamewekeza kwenye masoko, wameruhusu mashirika mengi ya nje kuleta ndege zao kenya. hapo utalaumu viongozi wa kenya au viongozi TZ.

Kwenye anga TZ ina Ndege 11 inaogopa nini? Kenya Air ways inatua TZ na Air Tanzania inatua Kenya. Watz waache uoga wa kushindana viongozi wa Tz watoke nje wakapambane kam Mama anavyofanya,

Mama sio Muoga amefunga mkanda ametoka nje kupambana, wanaume wako ndani wanapiga wayowe aibu.
 
Back
Top Bottom