Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Hoja zako zote ziko wrong.

Kuhusu gesi.
Hadi sasa hakuna uhaba wa gasi kwa matumizi ya Tanzania. Bomba la kusafirisha gesi toka Mtwara hadi sasa linafanya kazi chini kabisa ya uwezo wake haifikii hata asilimua 50. Hakuna kiwanda cha ndani kinachohitaji gesi ya Mtwara na kinashindwa kupata. Kuuza gesi Kenya kutasaidia bomba la gesi liweze kuwa utilised walau juu ya asilimia 50. Duniani kote walio na gesi nyingi wanaiuza nje ili kupata fedha tena kutokana na gesi kugunduliwa kwa wingi hivi karibuni bei imeanza kushuka rejea eneo la mediteranian. Kosa linaloigharimu Tanzania isinufaike sana na gesi yake ni mikataba mibovu ya uchimbaji na ujenzi wa bomba la Mtwara Dar iliyoingiwa na serikali ya awamu ya nne. Ndio maana umeme wa gesi umekuwa ghali. Hivyo kuiuza Kenya kutaleta unafuu kwa sababu ya economy of scale.

Uwekezaji wa Kenya
Kenya kana zilivyo nchi zote za dunia wana haki pia ya kuwekeza Tanzania kwa kufuata sheria zetu xa uwekezaji. Kwa nini ulalamike Kenya wakiwekeza lakini hulalamiki US au China wakiwekeza nchini? Hata hoja ya kulalamika kuwa Kenya wamewekeza miradi 500 nchini sisi tumewekeza miradi 30 haina mashiko kwani katika uwekezaji sio lazima mlingane , kinachotakiwa ni sisi kama nchi tuwe na sheria nzuri zinazolinda maslahi ya watu wetu wakati uwekezaji unafanyika. Kuna maeneo tunaweza kuzuia kabisa, mfano kumnyang'anya ardhi ya kilimo mkulima mdogo kisha ardhi hiyo hiyo unampa mkulima mkubwa toka nje alime.

Viwanda
Hoja kwamba viwanda vya Kenya vitaua viwanda vyetu haina mantiki. Katika uchumi sio lazima uzalishe kila kitu hata kama huna comparative advantage. Unachotakiwa kufanya ni kuzalisha vitu ambavyo una comparative advantage na kuwauzia wenzako kisha wewe unanunua vile ambavyo huna comparative advantage. Kama gesi imetoka kwetu ikasafirishwa umbali mrefu kwenda Kenya maana yake kuna gharama kubwa ya kuisafirisha kwa mtumiaji wa Kenya kuliko mtumiaji wa Tanzania hivyo kama bado pamoja na ughali wa gesi bado bidhaa toka Kenya ambayo imesafirishwa kuja Tanzania itauzwa kwa bei nafuu kuliko bidhaa kama hiyo iliyozalishwa Tanzania maana yake ni kuwa kiwanda cha Tanzania ni inefficient producer. Sasa wewe uko tayari kununua bidhaa ya ndani tena isiyo bora kwa gharama kubwa kuliko bidhaa rahisi lakini bora toka nje? pia kumbuka bidhaa toka Kenya ikiuzwa nchini serikali inakusanya kodi ya VAT na kodi ya mapato na wananchi wanapata satisfaction kwa kula bidhaa bora. Viwanda vya ndani Tanzania vinaathiriwa na gharama kubwa za uzalishaji zinazotokana kwanza na ughali wa nishati ya umeme au gesi unaitokana na mikataba ya kufisadi iliyofanyika huko nyuma na sio sababu ya kuelewana na Kenya.

Usafiri wa anga
Kuruhusu Kenya airways kuja nchini maana yake pia ATCL inaruhusiwa kwenda Kenya hivyo pande zite mbili zitanufaika. Hata kana ATCL haiwezi kushindana na Kenya airways, bado Tanzania itapata faida za moja kwa moja na zile zisizo za moja kwa moja. Ndege za kenya zikitua katika viwanja vyetu zitalipa kodi mbali mbali, kuweka mafuta, kununua vyakula vya kwenye ndege, makampuni yetu ya kuhandle mizigo yatapata kazi ya kushusha na kupakia, abiria wanaokuja wanatumia pesa kwa huduma wawapo nchini. Urahisi wa connection kuja nchini tokea hub ya Jomo Kenyatta airport utafanya tupate wageni wengi wakiwemo watalii kwa sababu ni rahisi uwanja wao kupokea wasafiri wanaokuja kwetu kutokana na mashirika mengi ya ndege kufua huko. Kiuchumi manufaa ni mengi mno kwa Tanzania tena pengine kuliko hata kenya yenyewe. Kama ATCL ikishindwa kuperform mchawi wetu sio Kenya ni sisi wenyewe mipango yetu mibovu.

Mazao ya wakulima
Wakulima wetu watapata sako la uhakika hivyo kuchochea bei anayolipwa mkulima kuongezeka kutokana na ushindani. Kumbuka hivi karibuni walipozuia mahindi yasiingie kenya bei ya mahindi kwa mkulima ilishuka sana.

NB: Tuache chuki dhidi ya Kenya bali tujifunze na kuiga toka kwao moyo wa kufanya kazi kwa bidii, uzalendo kwa nchi na kuwa aggressive katika kuchangamkia fursa.
 
Unauza nje unataka $ sio Tsh. Viwanda gani vilinyimwa na kwa sababu zipi lazima tuwe specific sio kuongelea kiujumla tu.
Hakuna alienyimwa, hata Dangote alipeww kwa ushirikiano wote, bila vikwazo vyovyote vile 😂😂😂
 
Sisi tuna gesi...wao hawana...kwetu gesi ni bidha...mteja kafika bei...kwa nini usiuze?...kuaogopa kuuza kwa kuogopa ushindani haina maana...wao wananini Cha ziada ambacho sisi hatuwezi kufanya tukashindana... kwanza sisi ndio bidhaa zetu zitazalishwa kwa gharama nafuu kuliko zao kwa sababu gesi ni yetu...hatununui.... mbona dhahabu tunauza.... mbona tanzanite tunauza....mbona korosho tunauza..... ushindani ndio....msingi wa kujifunza zaidi.
 
Wachumi wa Jamiiforums! Una gesi nyingi na uwezo wa kuexport tatizo hujaweza kuitumia ipasavyo nchini, hivi hii no issue ya kuzuia export? Kenya Airways aba monopoly ya soki la Tanzana unatafuta njia ya ATCL kuingia Kenya, then msomi abakwambia utakufa, huyu yuko seriously kweli? Eti labda ubadili uongozi wa ATCL. Sijui kama hayo makubaliano yanahusisha domestic routes. Maana inter States routes ni Kenya Airways pekee ndio ana operate.
 
Jamaa angalia usije kuwa mchawi uzeeni. Kwa nn afungie gas kisa sisi tutumie wenyewe ? Wacha ushindani uwepo ili bidhaa zipatikane kwa bei nafuu, na sisi tujiunze ushindani. Angalia TANESCO wanavyoringa kama pisi kali yenye ta.ko sababu wako wenyewe tu, Angalia mwendokasi huduma mbovuuuu kisa wako wenyewe. Acha ushindani uwepo ili huduma zetu pia ziwe nzuri.
 
Wewe usha wekeza huko? Au uko una implement Idea ya wanaume wenzako then unasema twende tukawekeze kenya
Wewe usha wekeza huko? Au uko una implement Idea ya wanaume wenzako then unasema twende tukawekeze kenya
NIMEWEKAZA GARAGE NAIROBI KARIBUNI KENYA MNAITAJI TOYOTA STOUT?
Nimewekaza kwa kadri ya capital yangu nanyi karibuni sana.
 
3. Soko la utalii hapa Kenyatta amecheza vizuri kama pele.
Tutalajie kuona vijana wetu wakiwa watazamaji kama kipindi cha nyuma na soko la utalii nikirudi mikononi mwa wakenya tena.(hapa kwenye utalii wenye fan zao wanaweza kudadavua kwanini Kenyatta amecheza kama Pela)
👆 👆 👆 👆
HAPA kulikuwa na vita sana, ambayo mwendazake alikuwa ameishinda
  • medereva wetu eti walikuwa hawaruhisiwi kuipick wagen/tourist Jomo Kenyata, ila wao wanaweza ingia Tanzania muda wowote. Sasa ivi tunakutana mpakani au sisi tunaenda mapaka Kenya. Jamaa wakipokea wageni na wakajua wanaenda Tanzania, wanawaspoili ile mbaya.
  • na kwamana nyingine kuna baadhi ya ndege ziliaanza kulazimika kutua Kilimajaro ili kuzuia kubadilisha dereva mara mbili na kupunguza gharama.
  • uyu mama nimemwona mwepesi sana na anachulia poa,
 
Mijitu mingine mizwazwa sana, Nigeria Algeria wanasupply gesi asilia kwnye nchi kadhaa africa lakin mbona wametoboa tu kuliko wewe unaetaka kulalia gesi, i think we jamaa hujui kitu kuhsu biashara za mataifa
 
Thread ya kiwaki kuwahi tokea
Hivi nyie nyumbu mnajua maana ya biashara kimataifa?
Yaani tuwe na gesi halafu tubaki tunaitazama tu na hatuna uwezo wa kuitumia halafu anakuja mtu ana matumizi nayo umuuzie hutaki et kisa atakuzidi uwezo pindi akianza kuitumia aisee huo ni zaidi ya ushamba wa kijinga
 
Tanzania iko mikono salama chini ya SSH. Ila Wasukuma wengi mulimezeshwa propaganda mbovu na mungu wenu Magufuli, hili litawasumbua Sana.

Mbona korosho tunalima Sana lakini tunakula 5% tu na nyingine zote wananunua akina Olam na Mohamed Enterprise s na kwenda kuzichakata na kuziuza Korea.

Kuna nadharia ya Adam Smith kwenye kitabu cha Wealth of Nations ya comparative advantage ndiyo inatawala biashara.
Ndiyo maana nimesema tuna viongozi wasiokuwa na maono.
Umetoa mfano wa Korosho, sasa hebu jiulize, ingekuwaje kama tungekuwa na kiongozi mwenye maono na akili akahakikisha nchi inakuwa na viwanda vya kuchakata Korosho, na kisha Korosho hiyo tukaiuza kutokea Tanzania kwenda kwa walaji moja kwa moja?

Tukija kwenye issue ya Gesi, kwanini viwanda vyetu visipewe kipaumbele kwanza kabla ya kuiuza kwa majirani zetu?
 
Hapa huwezi kupata majibu Wala hoja kujadiliwa vizuri
1) Kuna wale wanaounga mkono gesi kuuzwa, ikatokea Mtu akasema sio sahihi atashambuliwa kwa kuitwa msukuma as if ni Kama ushindani Kati ya Samia na hao wasukuma
2) Kuna wale ambao hawaungi mkono gesi kuuzwa, hawa wanaona Kama mama kaingia chaka. Wanawashambulia wanaokubali gesi iuzwe bila kuwa na point za msingi
Kuna vijana wa kile chama bado wanaishi kwa kivuli Cha Magufuli, akitokea Mtu akasema mama Samia hapa kakosea basi watamshambulia kwa kuhisi alikuwa mfuasi wa Magufuli. Na pia ni Kama hawataki kukubali kuwa hakuna upinzani Kati ya SSH na aliyekuwa JPM
Mimi naunga mkono gesi iuzwe tu,nipo pamoja na mama
 
Mwenendo wa biashara na uchumi wa kimataifa ni jambo linalohitaji umakini na pragmatism. Mataifa yote hasa majirani hutegemeana na kushirikiana.

Leo hii mataifa ya ulaya hasa ujerumani yanategemea gesi na mazao mengi kutoka urusi ingawaje nchi hii iko nyuma yao kimaendeleo. Nchi yetu inayo gesi ya kukidhi mahitaji ya ndani na masoko ya nje kwahiyo kushindwa kwetu kusupply viwanda vya ndani haiwezi kuwa sababu ya kuwakatalia kenya.
Awamu ya sita tumeanza vizuri sana. Keep going our dear Madam President.
 
Thread ya kiwaki kuwahi tokea
Hivi nyie nyumbu mnajua maana ya biashara kimataifa?..
Hakuna mtu anayepinga Gesi kuuzwa nje ya nchi, ila swali tunalojiuliza ni Je, viwanda vyetu vimepewa Gesi hiyo? Na kama havijapewa ni kwanini?

Kuna taarifa kuwa kiwanda cha Dangote kilihitaji sana hiyo Gesi lakini kikanyimwa ,Je, SSH amechukua hatua gani za kutatua migogoro ya ndani kabla ya kukimbilia kuuza Gesi kwa Kenyatta?
 
Back
Top Bottom