Ziara yangu ofisi za JamiiForums

Ziara yangu ofisi za JamiiForums


Wasalaam Wanajukwaa wenzangu.

Mapema tarehe 12 Julai, 2024 nimetembelea Ofisi za Jamii Forums kama mojawapo ya taasisi inayojihusisha na habari za kijamii. Lengo la ziara ni kuweza kufahamu shughuli za taasisi hii na kuona namna ya kushirikiana Ili kupanua wigo wa kuifikia jamii kidigitali.

Kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, tumejadiliana kuhusu umuhimu wa kushirikiana kwenye mada za kuifikia jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa jamii kwa ujumla na hususan, kupambana kutokomeza ukatili wa kijinsia na kwa watoto.

Kama mwanachama hai wa JF na aliyethibitishwa, niko tayari kuendelea kupokea mawazo na changamoto kutoka kwa wananchi kupitia mitandao ya kidigitali ambayo kimsingi inarahisisha sana mawasiliano na wananchi.

Hivyo, nawakaribisha nyote kunitumia mawazo mbalimbali na changamoto kwani, ushirikiano wa jamii ni muhimu kwa maendeleo.

Ahsante sana Mkurugenzi wa JamiiForums Maxence Melo (ninayesalimiana naye) na timu yako yote🤝

Mungu awabariki 🤝🇹🇿 na awabariki wanajukwaa wote🤝

Mheshimiwa Dkt. Gwajima D shikamoo... nimechoka sana baada ya kuona mtaala mpya wa elimu yetu hakuna somo la saikolojia! Hivi Saikolojia watu wanaichukuliaje Kwa mfano!? Hivi kama serikali imeweza kuanzisha michepuo ya masomo ya dini, inashindwa nini kuanzisha na michepuo ya masomo ya Saikolojia!?....

Binafsi naona Somo la Saikolojia liwe la lazima kuanzia kidato Cha kwanza Hadi kidato Cha nne...Saikolojia inatibu akili, dini/Imani inaponya roho na chakula kinatibu mwili ....tusichanganye hivi vitu! Changamoto ya afya ya akili yaweza kumpata Mtu yeyote na hasa asipokuwa na maarifa ya elimu ya Saikolojia na utambuzi.....Dini haiwezi kuchukua nafasi ya Saikolojia na ingekuwa hivyo basi tusingeona vituko Kwa baadhi ya watumishi wa Mungu. Chonde Chonde tunaangamia Kwa kukosa maarifa......
 
Huna baya mama ngoja nimalize kula nikupe kero yangu
 
Sisi kama Taifa, tunachangamoto kubwa sana kimaadili. Sisemei masuala ya ukatili au ushoga maana yanaongelewa sana. Ila nasemea maadili ya mtu mmoja mmoja kwa Taifa lake.

1. Watu wengi si waaminifu.
2. Watu wengi ni waongo waongo wamejaa uswahili uswahili sana.
3. Watu wengi wababaishaji sana
4. Vijana wanawaza kupiga madeal tu, hawataki kufanya kazi na kupata vipato halali
5. Watumishi wengi wa Serikali maadili yao ya kazi yapo ICU.

Najua tumechelewa ila bado tuna nafasi ya kusahihisha. Mwambie Rais afanye maadili ya nchi hii kuanzia ngazi ya familia iwe agenda ya Kitaifa. Kila Viongozi wanapoenda waifanye agenda hii kuwa agenda muhimu zaidi.

Ili tufanikiwe katika hili, viongozi wakubwa wawe vinara wa maadili mema. Endapo wao hawatabadilika na kuonesha njia tutatwanga maji kwenye kinu.

Narudia tena, maadili, maadili, maadili ya watu wa Taifa letu yapo ICU.

Fanyia kazi jambo hili mkuu. Wizara yako inayo nafasi. Tusiwaachie viongozi wa dini peke yao maana watu wa Taifa hili hawana muda na mambo ya Mungu kiviiile. Wao wambie miujiza tu. Bora kidogo mkisema nyie Viongozi wa Serikali mnaweza leta mabadiliko.

Pole kwa kusoma comment ndefu. Nimemaliza.
Uko serious sana mkuu punguza kidogo
 
Maza,
Mh Nawanda kazingua halafu Side akataka kuua soo, naomba simamia haki itendeke kila muhusika apate haki yake.
 
Umekua kiongozi mfano wa kuigwa humu jukwaani jinsi unavyojitahidi kufanyia kazi changamoto za Watanzania wenzetu, Hongera sana Mama.
 
Hongera sana.

Ni jambo jema sana kuwa karibu na Taasisi za kizawa kama jamii forums.

Usiishie kufanya ziara tu kiongozi pia uwe msaada kwa Taasisi hizi ili ziweze kuendelea zaidi na kuiendeleza Tanzania kwa ujumla.

Ishauri serikali wazipatie ruzuku Taasisi za namna hii ili ziweze kusaidia serikali katika kuelimisha na kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii.
Kama haqapati ruzuku,wanajiendeahaje?
 
Boss Melo kaajiri mpaka wazungu , salute kwako Mzee baba
 
Back
Top Bottom