Kombe la dunia 2014 Ureno alikuwa anacheza na Sweden kwenye hatua ya kufuzu.
Sweden walikuwa na ndoto ya kufuzu ugenini lakini Ronaldo alifunga hattrick na kuwatoa Sweden.
Sweden walimchukia Ronaldo kwa jambo hilo.
2016 kwenye Euro Cup, Ureno alikuwa anacheza na Ufaransa ambao ndio walikuwa host of the tournament.
Wafaransa waliona itakuwa ni mechi nyepesi kwao kwakua Ronaldo aliumia mguu wake wa kushoto.
Lakini jamaa akiwa benchi aliendelea kutoa maelekezo kwa team mates wake kama kocha.
Kilichotokea Ureno wakabeba ndoo.
Wafaransa wengi walimchukia jamaa.
2018 UCL Bayern na Madrid ikiwa ni miaka 6 imepita tangu timu yeyote ya Ujerumani kuchukua ubingwa.
Ronaldo aliziba mianya yote ya uwezekano na kisha akatoka na...
Wajerumani wengi walimchukia
Njoo 2017 kwenye fainali ya UCL Madrid na Juventus
Buffon ambaye ni mmoja ya wachezaji bora kwenye eneo la goal keeping ambao wanapewa sapoti na mashabiki pande zote za dunia.
Buffon katika rekodi zake hakuwahi kuchukua kombe la UEFA. Ronaldo aliingia kambani mara 2
Kitu ambacho kiliamsha hisia kwa waitaliani na kumchukia sana jamaa.
Mechi ya Euro waliyocheza dhidi ya Armenia wakati wanafanya warmup, wachezaji wa timu pinzani walikuwa wanapita karibu yake huku wakiimba "Messi Messi Messi"
Jamaa akapiga hattrick afu hivi ndio alivyokua akishangalia
Messi aliwadhihaki mashabiki wa Madrid baada ya kuifunga Madrid ikiwa nyumbani Bernabeu.
Naye Ronaldo akalipiza kisasi kwa kuifunga Barcelona kwake Camp Nou.
Barcelona na nusu ya dunia walimchukia jamaa.
Sababu kubwa jamaa anachukiwa ni mbili, ni eidha ni bora kuliko mchezaji wako pendwa au aliiadhibu vibaya timu yako.
Your love makes me strong, your hate makes me unstoppable” — Cristiano Ronaldo