Zielewe kazi za Usalama wa Taifa (TISS) na mipaka yake

Hahaha sio kweli, mbona hatusikii walioacha? Usichanganye askari kanzu na usalama. Askari kanzu anailinda jamii dhidi ya jinai usalama anailinda dola dhidi ya watu wenye akili za juu
Watu wanaacha,tofauti na taasisi nyingine huko lazima ukaguliwe nini kiko nyuma ya maamuzi yako,kama ni kwa roho safi unahisi kutotaka kuendelea,unaondoka vizuri kabisa.
 
Mkuu mleta mada, mabadiliko ya sheria ya TISS yaliyofanyika last year upo aware nayo? Umesoma mabadiliko hayo? Nimeona kama hujazingatia mabadiliko hayo kwenye bandiko lako.
Sijayasoma, tusaidie kwa kuyaweka hapa kwa faida ya wengine.

Nieleweke kwamba bandiko langu limekusudia kutoa ABCs za usalama wa taifa kwa umma. Sijakusudia kufanya uchambuzi wa ufanisi, kimuundo, wala kimaamuzi.
 
Tunahujumiwa sana na mataifa ya jirani na mbali kidogo kama SA na wengine hapa
Matunda yetu, mboga, kahawa, na hata Korosho na mengi yanatoka kwetu na kuandikwa ni za kwao

Swali je Usalama hawaingii hapo kuchunga mali zetu na majizi?

Na kama ni hivyo kwanini sisi inakuwa ngumu kuuza hata mchicha London?
Hawa sio kazi yao hii?
 
Usikimbie majukumu. Ndiyo kukua huko Eagle girl.

Jibidiishe kujenga Taifa, badala ya kujenga Nchi. Utabarikiwa. 😎

-Kaveli-
😃😃 Wacha nipambane kulijenga taifa kwa kulipa Kodi, hizo nyingine tuwaachie kaunda suti mkuu
Usikimbie majukumu. Ndiyo kukua huko Eagle girl.

Jibidiishe kujenga Taifa, badala ya kujenga Nchi. Utabarikiwa. 😎

-Kaveli-
Wacha nipambane kulijenga taifa kwa kulipa Kodi hizo nyingine tuwaachie kaunda suti mkuu
 
Ila TISS yetu haina ufanisi mkubwa coz haina vichwa vingi vyenye maarifa wengi wamebebwa sana na ndugu zao kupata Kazi.....kutwa kujiona maisha wameyapatia,kulewa ovyo na fujo.
ukitaka watu makini ni LAZIMA uwa target wahitimu waliofanya VIZURI SANA huko mashuleni. Nje ya hapo unakuwa kumbakumba unazoa kila takataka.
 
Nitarudi
 
sijasoma uzi. kwa aliesoma atuambie kama mambo ya kung'oa kucha na kuwapoteza watu yapo aya gani maana uku kitaa tumeambiwa iyo ndo kazi kuu inayofanyika
🤣🤣🤣 Ujuwe kila kazi ina wahuni wanaohasi taratibu za kazi na kufanya yale yasiyotarajiwa (Deviants). Sasa usiufanye uhasi wao ndio taratibu au msingi wa kazi zao.

Changamoto kubwa ya idara za usalama kwenye nchi mbalimbali ni kukabiliana na kitu kinachoitwa DEEP STATE. Kwamba kunakuwa na idara huru na binafsi ndani ya idara ya nchi ambayo inafanya mambo maovu kama utekaji, wizi au kushirikiana na majambazi nk. Ni vigumu sana kugundua uwapo wa Deep State kwasababu wanaotakiwa kugundua ni miongoni mwa hao waliomo kwenye deep state.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…