Zijue aina za utajiri wa kichawi zinazoshika kasi kwa sasa

unaweza hisi ni rahisi ila kugonga kila siku ni mziki mnene

alafu kuna ka nguvu ka kichawi lazima kawepo kukuchosha
 
Mkuu kuna kitu umeficha, ama mwenyewe haukifahamu!

Utajiri wa "kanyoka", "kafara" na"punje", mwisho wake siyo kufirisika tu, huwa na kifo pia.

Mfano huo wa vipunje, jogoo akidonoa vipunje viwili, ndiyo miaka yako ya kutesa na utajiri na ndiyo idadi ya miaka yako ya kuishi.


Tukija kwenye kanyoka hivyo hivyo, ukikiuka masharti kakafa, na wewe ndiyo mwisho wako.
 
Huo wa kuua wafanyakazi naona unakuja kuwa fashion Sana....
Wafanyakazi wana vinasaba Gani...na utajir....
Mm Huwa natamani research zifanyike yaan pale UDSM ianzishwe department ya witchcraft & associates
Najuuliza Nchi kama Norway ni namba Moja kwenye Fishing industry

Nchi ZILIZO undergo Industrial revolution na wenyewe wana amini KATIKA ushirikina....????

Bado tunasafari ndefu sana kama taifa....
 
Utajiri wa nyota za watu - Wanautumia sana manabii, mitume, wachungaji n.k kwa kuiba nyota za watu wenye mafanikio na kuzigeuza kuwa mafanikio yao na familia zao...

Aina hii ya uchawi hufanywa pia na aina ya waganga wa nyota, huiba nyota ya mtu mmoja na kuikabidhi kwa mtu mwingine...

Hawapo mbali pia baadhi ya masheikh na wanazuoni waliobobea katika elimu za nyota...

NB: Hizi sio nyota zile za unajimu
 
Santos06 chuma ulete ni pepo la kimasikini haliwezi kumpa mtu utajiri zaidi ya kula yake ya siku tena chakula duni cha kawaida mno
 
Ukifanikiwa kidogo watu huwa wanaamua kukutengenezea stori ambayo hujawahi kuiishi
Hasa hizi biashara za usafirishaji huwa kuna changamoto nyingi sana unajitahidi uiweke gari kwenye hali nzuri na marekebisho ya mara kwa mara unafunga tairi mpya ila zinapasuka gari inaanguka inaua watu Unaambiwa umetoa kafara.

Unapambana had na madereva wako unawaambia hutaki gari zako zikimbie, zifate utaratibu na Sheria za barabarani hutaki ligi ila unakuja kusikia bus imegongana uso kwa uso na imeua watu 9 na wafanyakazi wote waliokua wamekaa mbele na chanzo Cha ajali ni Lori lililo overtake bila tahadhari ila stori itatengenezwa kuwa mmliki wa bus ndo umetoa kafara
 
Mkuu watu tayari wame generalize mambo, hii ni kutokana na story tunazozisikia tangu tunakua kwenye jamii inayotuzunguka na vingi tunaamini pasi na ushahidi
 
Nakubaliana na wewe ila Kuna ajali za uzembe ila Kuna ajali ni chini ya pazia bisha ama usibishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…