Wewe mbona haujaolewa? hauwezi ukajiweka kwenye mzani sawa na mwanamke ambae ameolewa. Kitendo cha yeye kuolewa maana yake amekuzidi akili. Anajua kwenye mahusiano anatakiwa kukaa wapi na wajibu wake ni nini ndio maana akaolewa. Wewe haujui chochote ndio maana bado u msimbe. Thread ya 11 hakuna mwanamke aloejitokeza kukuunga mkono wewe unafikiri hawapiti humu? Wenzako wanapita hapa na wanakuchora tu uko kwenye mahusiano yao ni watiifu sababu wanajua iyo ndio nguzo kuu ya kuishi na mwanaume. Feminism imewaaribu sana akili imefika hatua wasimbe mnajiweka kwenye mzani wa juu zaidi ya waliolewa.! what the fuvk.!
Wewe bado huwajui wanawake ndio maana unadiriki kusema mwanamke ambaye hajatumika hawezi kuwa na mitazamo kama yangu, mwenzako huko kasema kuna wanawake mabikira wanajitongozesha wenyewe kwa wanaume, ili wakaliwe sababu ya tamaa zao sasa hizo sifa nzuri za mabikira kwa mujibu wenu sijui ziko wapi hapo
Na kwa taarifa yako wanawake waliochezewa ndio huwa hawana ujasiri wa kuwakosoa wanaume sababu wanajua mkiwatukana itawauma, maana mnakuwa mmewaambia ukweli mchungu ila mkiona mwanamke ana ujasiri wa kuwakosoa wanaume, ujue huyo hajachezewa hivyo haogopi hata mkimtukana haimuumi sababu siyo ukweli
Looh eti wanawake kuolewa ndio akili unazungumzia ndoa hizi hizi ambazo waume za watu wana michepuko kibao pamoja na kununua malaya au kuna nyingine, msidhani hatuoni yanayoendelea kwenye hizo ndoa wanawake wengi hawana furaha, pamoja na kutwishwa mzigo wa majukumu huku pesa za waume zao wakifaidi michepuko tu
Yani siku hizi michepuko inatreatiwa vizuri kuliko hata wake za ndoa mume akipata pesa anakula na malaya zake huko, wakishamfilisi ndio anarudi kwa mkewe ili amvumilie na umasikini wake, mimi kuliko kuwa kwenye ndoa ya aina hiyo ni heri nibaki single milele mpaka nakufa sisi wengine kwetu ngono siyo issue kwanza ni uchafu tu mnaoufanya
Mimi siyo kwamba nimewazidi akili wanawake wengi walioko kwenye ndoa tu, bali hata wanaume nao wapo wengi ambao nimewazidi akili ukiwemo wewe ndio maana huwezi kushindana na mimi kwa hoja, bila kutoka nje ya mada na kuleta personal attacks za kipumbavu utadhani unanijua
Kwahivyo wewe huwa unaandika mada ili uungwe mkono na watu yani unaamini ili hoja yako iwe na ukweli basi lazima ipate validation kutoka kwa watu, basi labda nikuambie tu mimi sijali kuhusu kuungwa mkono najiamini na misimamo yangu, uliza wanaonifahamu humu huwa sipindishi maneno nasimamia ninachokiamini hata dunia nzima ingeenda kinyume na mimi
Na hata hivyo nadhani umeongelea uzi huu tu mbona kuna nyuzi nyingi watu huwa wanalike comments zangu, na wengine kucomment kuniunga mkono tena siyo wanawake tu bali hata wanaume wanaojielewa, wapo wengi tu humu wanaonisifia na wanaonipongeza kwa mitazamo yangu na sioni kama ni big deal
Huwa nawaappreciate tu kisha natembea sababu huwa najua naongea ukweli na mtu yeyote mwenye akili timamu na anayependa ukweli na haki ndio atanielewa, huwa siongei ili kuwafurahisha wanaume kama baadhi ya wanawake wanaojifanya kuanzisha mada za kusifia wanaume humu, ili waonekane wife material ilihali nje ya jf ni magold digger tu
Sasa mimi siwezi unafiki na wala msitegemee hizi kauli zenu ndio zitaninyamazisha, nimeanza kuambiwa hizo kauli toka 2019 na waliokuwa wanajifanya manabii feki na wanasaikolojia uchwara, na hayajaniathiri chochote wala kubadili ukweli ndio kwanza maisha yananinyookea huku mkizidi kuteseka na umasikini na misongo ya mawazo