Zijue Mbinu Hizi za Kuwa Tajiri("Milionea")

7. Ukianza kupata utajiri, wafundishe wengine mbinu ulizotumia
Andika vitabu, uza. Wafundishe wengine masuala ya kifedha kwenye semina, warsha, makongamano, kwa malipo.
Bahati Mbaya sana Wanaofundisha kwenye hizo Semina na Warsha na wao hawana hela wanategemea kiingilio unacholipa ndio wale ugali dagaa watoto waende chooni.

Mi nadhani Utajiri una mbinu nyingjne kuliko hizi bla bla za vitabuni

Watu tumesoma Hadi Rich Dady Poor Dady lakini bado
 
Kwani we ni tajiri?!...labda tuanzie hapo...
  1. Kocha wa timu ya mpira si lazima awe mchezaji bora, lakini anaweza kufundisha wachezaji wakawa mabingwa. Hii inaonyesha kuwa mtu anaweza kufundisha mbinu za kupata utajiri hata kama yeye hajaupata utajiri.
  2. Daktari wa afya hajawahi kuugua magonjwa yote anayoyatibu, lakini bado anawasaidia wagonjwa kupona. Hii inadhihirisha kuwa kufundisha hakuhitaji mtu awe na uzoefu wa hali halisi.
  3. Na mimi najifunza ku-apply mbinu hizi. Naamini baada ya muda fulani "nitatoboa".
  4. Utajiri huanza na maarifa. Nimeamua kuwa tajiri wa maarifa kwanza, ili mapesa yafuate baadaye.
Waswahili wanasema: "kizuri kula na mwenzio." Kwakuwa mbinu nilizozieleza zina ukweli kwanini niwe mchoyo nisiwasaidie wengine wanaotamani kuwa matajiri. Nikiwa tajiri peke yangu, watu wengi watakuja kuniomba msaada. Tukiwa matajiri wengi................ jazia...
 
Asante sana kwa maarifa haya.
Hakika watakaoyaamini watavuka,lakini wanaoamini kuwa huwezi kutajirika bila kutokea familia ya kitajiri watayapita tuu.
 
Ukitaka kuwa Tajiri pamoja na yoteee MGANGA

Waganga wa kienyeji ni maajenti wa shetani. Wanapokuambia watakupa utajiri lengo lao ni ili umwabudu shetani. Na ukimwabudu shetani maana yake tayari umejiingiza katika kundi la watakaotupwa katika moto wa milele. Shetani alimwambia pia Yesu amuabudu ili ampe fahari ya ulimwengu.
Mt 4:8-10
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake, akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.” Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa: ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako
na kumtumikia yeye peke yake.’”

cc: Mahondaw Kiranga Mshana Jr Infropreneur Demi FaizaFoxy
 
Unaweza kuthibitisha kuwa shetani yupo kweli na hizo habari za shetani kuwapo si hadithi za ujinga za mapokeo tu?
 
Kwa Afrika, utajiri halali uko shambani na kwenye mifugo
 
Sijakuelewa kabisaaa
Tunazungumzia MOTO au PESA??.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…