Zijue Mbinu Hizi za Kuwa Tajiri("Milionea")

Haya mambo ya Imani na sio kwa nadharia zingine.
Wapo matajiri wengi na pote huko hawapo
Braza ukifanya biashara kuna kuibiwa na vitu vyengine vingiii
Usipo jizatiti LAZIMA WAKUTOE KWENYE RELI.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Kuwa tajiri kunatokana na kudra za mwenyezi Mungu
Mungu hana ujinga huu
Kwamba aliumba yule awe masikini na huyu Tajiri.
Hapana KWA KWELI.
Branch nawoona wapo vizuri kuliko makampuni yote, wao riba yao ni ndogo sana na pia hawana usumbufu ukipenda unaweza ukawatembelea kwa hii link
Ukikop,a hovyo bila mpangilio utakuwa maskini ukikopa kwa malengo utan,ufaika
Hili ni Tangazo Marketing Officer.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Luka 6:38(NEN)
"Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa."
Bila kuwa bahili utoboi
Wakati wa kuanza asilimia kubwa (ikiwezekana hata zaidi ya 80) kiende kwenye biashara zako.
Save then Invest
And Save SO MUCHH.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Eti live below ur means 🤣🤣🤣
huo mshahara wenyewe tuu kwa budget simple ya ugali maharage ikifika tarehee 15 hela kwishney
Unajiuliza below your means itakuwa ugali na maji au? 😂😂😂

Mi nadhani hizi ni mbinu za kuumaintain utajiri baada ya kuupata, na unapatikanaje? That’s a question for another day. (kurithi, kufisadi, kuuza startup kwenye tech au basi kupiga bingo labda lottery)?
 
Unaweza kuthibitisha kuwa shetani yupo kweli na hizo habari za shetani kuwapo si hadithi za ujinga za mapokeo tu?
Ndio, naweza kukuthibitishia kwa mitazamo mitatu pamoja na uzoefu wangu binafsi.

1. Mtazamo wa Kikristo (Kimaandiko)
Katika Biblia, shetani anatajwa mara nyingi kama adui wa Mungu na wanadamu. Baadhi ya mistari inayoeleza uwepo wake ni hii:

1 Petro 5:8 – "Mwe na kiasi na kukesha; kwa sababu adui yenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze."
Katika kitabu cha Ayubu 1:6-7 – Shetani anaelezewa kama mtu halisi anayekuja mbele za Mungu kuleta mashtaka juu ya wanadamu.
Katika kitabu cha Mathayo 4:1-11 – tunasoma kwamba Yesu mwenyewe alijaribiwa na shetani jangwani, jambo linaloonyesha kuwa si hadithi tu, bali ni kiumbe halisi. Kwa mtazamo huu, ikiwa mtu anaiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu, basi anapaswa pia kukubali kuwa shetani yupo kwa kuwa Maandiko yamemueleza waziwazi.

2. Mtazamo wa Kifalsafa
Dhambi na maovu katika ulimwengu huu ni ushahidi wa nguvu hasi zinazopinga mema. Kama tunakubali kuwa kuna Mungu aliye mwema, ni rahisi kuelewa kuwa kuna nguvu za shetani zinazopinga mpango wake. Falsafa nyingi za kidini na hata imani za kale zinakubaliana kuwa kuna nguvu za giza zinazojaribu kuwapotosha wanadamu.

3. Mtazamo wa Kihistoria
Katika historia, matukio mengi yamehusishwa na kazi za shetani, ikiwemo ibada za nguvu za giza, uchawi/ushirikina, na hata roho za uovu zinazowatesa watu. Watu wengi wenye uzoefu wa mapepo (exorcisms) wameeleza uzoefu wao. Kanisa katoliki, kwa mfano, lina kitengo maalum cha kufanya ukombozi wa watu waliopagawa na mapepo. Mapepo ni roho chafu za kishetani. Makanisa ya kipentekoste ndio usiseme. Wainjilisti na Wachungaji wamekuwa wakitoa au kufukuza mapepo katikati ya watu wengi. Uzoefu unaonyesha wazi mtu mwenye mapepo anakuwa na nguvu nyingi zisizo za kawaida. Mwanamke mwenye mapepo, kwa mfano, anaweza kuwararua wanaume wanne. Hizi sio nguvu za kawaida.

Wewe ni shahidi, miaka nenda rudi watu wamekuwa wakienda kwa waganga wa kienyeji/washirikina kutafuta msaada. Ushirikina ni kazi za kishetani.

4. Uzoefu Wangu Binafsi: Mimi mwenyewe kuna siku nilivamiwa na mapepo. Yalikuja usiku yakanikandamiza sana kifuani utafikiri nimeangukiwa na gunia la kilo 100. Nilijua "dawa" ya mapepo ni kuyakemea kwa Jina la Yesu. Niliyakemea dakika ile ile yakaniachia.

Mpaka hapo Chief, nadhani umeamini sasa kwamba shetani yupo.
 
Watu wengi wana ndoto za kuwa matajiri. Wanafanya kazi kwa bidii usiku na mchana ili wawe matajiri. Hata hivyo ni wachache wanaofanikiwa kuupata utajiri. Leo nakutajia baadhi ya mbinu muhimu za kupata utajiri au kuwa milionea/bilionea – sizungumzii utajiri unaopatikana kwa bahati au kwa kurithi.

Utajiri unapatikana kwa kutumia mbinu sahihi, nidhamu, na uthabiti. Kama kweli unataka kuwa tajiri, tumia mbinu hizi:

1. Anza kuwa na mtazamo(mindset) wa utajiri
Utajiri huanzia kwenye mawazo. Watu matajiri huifikiria pesa tofauti na watu wa kawaida. Ili kujenga mtazamo wa utajiri fanya hivi:
  • Matumizi yako ya pesa yawe ya chini kuliko kipato chako(spend less than you earn)
  • Weka malengo ya kifedha ya muda mrefu.
  • Kaa katikati ya watu wenye mafanikio na maarifa ya kifedha.
2. Weka pesa benki na wekeza kwa hekima
Kuweka pesa benki peke yake hakutakufanya uwe tajiri, lakini ukiwekeza utafanikiwa. Kwahiyo badala ya kuweka pesa zako zote benki:
  • Wekeza kwenye hisa, dhamana, au mifuko ya pamoja. Kabla ya kuwekeza fanya utafiti.
  • Anzisha biashara yenye uwezo wa kukua.
  • Wekeza kwenye mali isiyohamishika(real estate) au mali nyingine zenye thamani inayoongezeka.
3. Uwe na vyanzo vingi vya mapato
Chanzo kimoja tu cha mapato hakitoshi sana kama unataka kupata utajiri mkubwa na wa kudumu. Watu matajiri hupata pesa kutoka kwenye vyanzo vingi vya mapato kama vile nyumba za kupangisha, gawio(dividents), au mirahaba(royalties), biashara za mtandaoni nk.

4. Dhibiti fedha zako vizuri
Huwezi kuwa tajiri kama utashindwa kudhibiti au kusimamia fedha zako. Kwahiyo:
  • Uwe na bajeti na ufuatilie(track) matumizi yako.
  • Epuka madeni yasiyo ya lazima na tumia pesa kwa busara.
  • Uwe na akiba ya dharura(emergency fund) ili uweze kuyakabili matukio au hali zisizotarajiwa.
5. Elimu haina mwisho. Jifunze tena na tena masuala ya kifedha
Dunia ya kifedha inabadilika kila wakati. Watu matajiri huendelea kujifunza kwa:
  • Kusoma vitabu kuhusu utajiri na usimamizi wa fedha.
  • Kuhudhuria semina za biashara na uwekezaji.
  • Kujifunza kutoka kwa washauri na wataalamu wa fedha.
6. Uwe mvumilivu (be patient and persistent)
Utajiri hauoti kama uyoga. Wajasiriliamali wengi walichukua miaka kadhaa kuwa matajiri. Hivyo uwe mvumilivu, na usikate tamaa unapokutana na changamoto.

7. Ukianza kupata utajiri, wafundishe wengine mbinu ulizotumia
Andika vitabu, uza. Wafundishe wengine masuala ya kifedha kwenye semina, warsha, makongamano, kwa malipo.

Ukishakuwa tajiri usimsahau Mungu.
Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako... jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake...( Kum 8:10-11).

Ukimsahau Mungu Maandiko haya yanaweza kukuhusu:
“Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. Akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje?

Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanaitaka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu anayejirundikia mali kwa ajili yake mwenyewe, lakini si tajiri mbele ya Mungu.”( Luka 12:15-21)

View attachment 3236711
Points zako zote namba moja hadi saba zipo sahihi.

Swali linakuja hapo ulipoandika "Ukishakuwa tajiri usimsahau Mungu"

Kwanzia pointi namba moja hadi namba saba umepambana mwenyewe, Hakuna Mungu yeyote aliyekusaidia kupata utajiri.

Iweje sasa umeshapata utajiri kwa juhudi na maarifa yako binafsi, Ndio uanze kuleta habari za huyo Mungu?

Wakati ukiwa maskini huyo Mungu alikuwa wapi?

Huyo Mungu alikuwa anasubiri nini asikutajirishe pasipo wewe kuhangaika kumuomba?

Kwa nini huyo Mungu anasubiri wewe uhangaike kutafuta utajiri kwa juhudi na maarifa yako binafsi, Halafu yeye aje baadae kutaka kusifiwa na kushukuriwa?

A God who requires praises when you win, should not shy away from taking blames when you lose.
 
Ndio, naweza kukuthibitishia kwa mitazamo mitatu pamoja na uzoefu wangu binafsi.

1. Mtazamo wa Kikristo (Kimaandiko)
Katika Biblia, shetani anatajwa mara nyingi kama adui wa Mungu na wanadamu. Baadhi ya mistari inayoeleza uwepo wake ni hii:

1 Petro 5:8 – "Mwe na kiasi na kukesha; kwa sababu adui yenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze."
Katika kitabu cha Ayubu 1:6-7 – Shetani anaelezewa kama mtu halisi anayekuja mbele za Mungu kuleta mashtaka juu ya wanadamu.
Katika kitabu cha Mathayo 4:1-11 – tunasoma kwamba Yesu mwenyewe alijaribiwa na shetani jangwani, jambo linaloonyesha kuwa si hadithi tu, bali ni kiumbe halisi. Kwa mtazamo huu, ikiwa mtu anaiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu, basi anapaswa pia kukubali kuwa shetani yupo kwa kuwa Maandiko yamemueleza waziwazi.

2. Mtazamo wa Kifalsafa
Dhambi na maovu katika ulimwengu huu ni ushahidi wa nguvu hasi zinazopinga mema. Kama tunakubali kuwa kuna Mungu aliye mwema, ni rahisi kuelewa kuwa kuna nguvu za shetani zinazopinga mpango wake. Falsafa nyingi za kidini na hata imani za kale zinakubaliana kuwa kuna nguvu za giza zinazojaribu kuwapotosha wanadamu.

3. Mtazamo wa Kihistoria
Katika historia, matukio mengi yamehusishwa na kazi za shetani, ikiwemo ibada za nguvu za giza, uchawi/ushirikina, na hata roho za uovu zinazowatesa watu. Watu wengi wenye uzoefu wa mapepo (exorcisms) wameeleza uzoefu wao. Kanisa katoliki, kwa mfano, lina kitengo maalum cha kufanya ukombozi wa watu waliopagawa na mapepo. Mapepo ni roho chafu za kishetani. Makanisa ya kipentekoste ndio usiseme. Wainjilisti na Wachungaji wamekuwa wakitoa au kufukuza mapepo katikati ya watu wengi. Uzoefu unaonyesha wazi mtu mwenye mapepo anakuwa na nguvu nyingi zisizo za kawaida. Mwanamke mwenye mapepo, kwa mfano, anaweza kuwararua wanaume wanne. Hizi sio nguvu za kawaida.

Wewe ni shahidi, miaka nenda rudi watu wamekuwa wakienda kwa waganga wa kienyeji/washirikina kutafuta msaada. Ushirikina ni kazi za kishetani.

4. Uzoefu Wangu Binafsi: Mimi mwenyewe kuna siku nilivamiwa na mapepo. Yalikuja usiku yakanikandamiza sana kifuani utafikiri nimeangukiwa na gunia la kilo 100. Nilijua "dawa" ya mapepo ni kuyakemea kwa Jina la Yesu. Niliyakemea dakika ile ile yakaniachia.

Mpaka hapo Chief, nadhani umeamini sasa kwamba shetani yupo.
Mtazamo wa Kikristo umejaa kasumba ya mapokeo ya kidini na logical fallacy ya argument from authority. Si kila mtu ni Mkristo na anaukubali, kwa hivyo kuanzia hapo ushashindwa.

Biblia imetaja mambo mengi ambayo hayawezi kuthibitishwa objectively na kimsingi hayatakiwi kukubalika kama ukweli.

Mfano Mungu, mbingu, malaika, shetani, roho mtakatifu na ujinga mwingine mwingi kama huo.

Hivyo kutumia Biblia kutaja kitu kama uthibitisho kwamba kipo ni ujinga tu.

Kwenye mtazamo wako wa kifalsafa, kuwezekana kuwapo kwa maovu popote ni uthibitisho kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote huyo uliyemtaja wa Biblia hayupo. We have been through the Epicurean Paradox/ The Problem of Evil before.

Mungu huyo angekuwapo, isingewezekana kuwepo uovu au dhambi yoyote. Uwepo wa uovu unaonesha Mungu huyo hayupi.

Na kwa mujibu wa maelezo yako ya shetani na Mungu, kama Mungu huyo hayupo, na shetani naye hayupo pia.
 
Unajiuliza below your means itakuwa ugali na maji au? 😂😂😂

Mi nadhani hizi ni mbinu za kuumaintain utajiri baada ya kuupata, na unapatikanaje? That’s a question for another day. (kurithi, kufisadi, kuuza startup kwenye tech au basi kupiga bingo labda lottery)?
Au ugali na chumvi
 
Mungu hana ujinga huu
Kwamba aliumba yule awe masikini na huyu Tajiri.
Hapana KWA KWELI.

Hili ni Tangazo Marketing Officer.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Hapana huwa nakopa sana kwa hawa jamaa nikiwa nashida ndogo ndogo nanikitaji fedha za haraka
 
Kwanzia pointi namba moja hadi namba saba umepambana mwenyewe,
Ukipambana ukawa tajiri, usifikiri umepambana mwenyewe. Bado Mungu anakuwa amehusika kukufanikisha.

Unaweza kupambana sana lakini wachawi wakakuloga ukawa kichaa, akili zako zisiweza tena kuwaza pesa. Unaweza kupambana ukapata mapesa ukaenda kuyaweka benki lakini njiani kabla hujafika benki ukakutana na majambazi wakakuibia pesa zote, au kabla hujafika gari lako likagonga lori na wewe ukafa papo hapo, utakuwa tajiri tena? Macho yako yakipofuka ghafla utaweza kusoma vitabu ili upate ujuzi zaidi wa kupata utajiri?

So, ukiwa mzima, ukisafiri salama, viungo vya mwili wako vikiwa na uzima, msifu Mungu. Ukilala salama ukaamka na nguvu ya kwenda kutoa lecture kuhusu utajiri, mshukuru Mungu. Try to imagine yaliyotokea Los Angeles. Wapambanaji si walikuwa wengi katika huo mji? Moto ulivifanyaje vitega uchumi vyao!!

Nadhani umeona sasa. Ukiupata umilionea, there is still God behind you, making you a millionaire.

So, God requires praises when we win, and when we lose, we should not shy away from thanking Him,
for it is written: 'Give thanks in all circumstances; for this is God’s will for you in Christ Jesus.'
(1 Thessalonians 5:18)
 
Watu wengi wana ndoto za kuwa matajiri. Wanafanya kazi kwa bidii usiku na mchana ili wawe matajiri. Hata hivyo ni wachache wanaofanikiwa kuupata utajiri. Leo nakutajia baadhi ya mbinu muhimu za kupata utajiri au kuwa milionea/bilionea – sizungumzii utajiri unaopatikana kwa bahati au kwa kurithi.

Utajiri unapatikana kwa kutumia mbinu sahihi, nidhamu, na uthabiti. Kama kweli unataka kuwa tajiri, tumia mbinu hizi:

1. Anza kuwa na mtazamo(mindset) wa utajiri
Utajiri huanzia kwenye mawazo. Watu matajiri huifikiria pesa tofauti na watu wa kawaida. Ili kujenga mtazamo wa utajiri fanya hivi:
  • Matumizi yako ya pesa yawe ya chini kuliko kipato chako(spend less than you earn)
  • Weka malengo ya kifedha ya muda mrefu.
  • Kaa katikati ya watu wenye mafanikio na maarifa ya kifedha.
2. Weka pesa benki na wekeza kwa hekima
Kuweka pesa benki peke yake hakutakufanya uwe tajiri, lakini ukiwekeza utafanikiwa. Kwahiyo badala ya kuweka pesa zako zote benki:
  • Wekeza kwenye hisa, dhamana, au mifuko ya pamoja. Kabla ya kuwekeza fanya utafiti.
  • Anzisha biashara yenye uwezo wa kukua.
  • Wekeza kwenye mali isiyohamishika(real estate) au mali nyingine zenye thamani inayoongezeka.
3. Uwe na vyanzo vingi vya mapato
Chanzo kimoja tu cha mapato hakitoshi sana kama unataka kupata utajiri mkubwa na wa kudumu. Watu matajiri hupata pesa kutoka kwenye vyanzo vingi vya mapato kama vile nyumba za kupangisha, gawio(dividents), au mirahaba(royalties), biashara za mtandaoni nk.

4. Dhibiti fedha zako vizuri
Huwezi kuwa tajiri kama utashindwa kudhibiti au kusimamia fedha zako. Kwahiyo:
  • Uwe na bajeti na ufuatilie(track) matumizi yako.
  • Epuka madeni yasiyo ya lazima na tumia pesa kwa busara.
  • Uwe na akiba ya dharura(emergency fund) ili uweze kuyakabili matukio au hali zisizotarajiwa.
5. Elimu haina mwisho. Jifunze tena na tena masuala ya kifedha
Dunia ya kifedha inabadilika kila wakati. Watu matajiri huendelea kujifunza kwa:
  • Kusoma vitabu kuhusu utajiri na usimamizi wa fedha.
  • Kuhudhuria semina za biashara na uwekezaji.
  • Kujifunza kutoka kwa washauri na wataalamu wa fedha.
6. Uwe mvumilivu (be patient and persistent)
Utajiri hauoti kama uyoga. Wajasiriliamali wengi walichukua miaka kadhaa kuwa matajiri. Hivyo uwe mvumilivu, na usikate tamaa unapokutana na changamoto.

7. Ukianza kupata utajiri, wafundishe wengine mbinu ulizotumia
Andika vitabu, uza. Wafundishe wengine masuala ya kifedha kwenye semina, warsha, makongamano, kwa malipo.

Ukishakuwa tajiri usimsahau Mungu.
Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako... jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake...( Kum 8:10-11).

Ukimsahau Mungu Maandiko haya yanaweza kukuhusu:
“Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. Akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje?

Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanaitaka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu anayejirundikia mali kwa ajili yake mwenyewe, lakini si tajiri mbele ya Mungu.”( Luka 12:15-21)

View attachment 3236711
Ww una ngapi?
 
Mungu huyo angekuwapo, isingewezekana kuwepo uovu au dhambi yoyote.
My friend, Yesu anatuandalia makao ambayo ndani yake hakutakuwa na dhambi yoyote. Hii dunia ya sasa inasubiri kuunguzwa. Mungu ni mvumilivu, bado anakusihi uokoke kabla hajaiangamiza dunia na wote wasiomcha Yeye.
 
Kwanza, hujathibitisha Yesu atatuandalia hayo makao na kwamba hizo habari si hadithi za kujazana ujinga tu. Hiyo ni habari ya imani, si fact.

Thibitisha Yesu atatuandakia makao hayo, factually.

Lakini pili, hata kama Yesu atatuandalia makao, hilo haliondoi point ya problem of evil.

Kama una mtoto wako, mko kwenye gari, mnaelekea nyumbani, mtoto analia njaa, una uwezo wa kumpa chakula ale kwenye gari kabla hamjafika nyumbani, kwa nini umwambie mtoto akae na njaa tu kwa sababu atakula akifika nyumbani?

That will be cruel and unreasonable.

Is your God cruel and unreasonable?
 
Watu wengi wana ndoto za kuwa matajiri. Wanafanya kazi kwa bidii usiku na mchana ili wawe matajiri. Hata hivyo ni wachache wanaofanikiwa kuupata utajiri. Leo nakutajia baadhi ya mbinu muhimu za kupata utajiri au kuwa milionea/bilionea – sizungumzii utajiri unaopatikana kwa bahati au kwa kurithi.

Utajiri unapatikana kwa kutumia mbinu sahihi, nidhamu, na uthabiti. Kama kweli unataka kuwa tajiri, tumia mbinu hizi:

1. Anza kuwa na mtazamo(mindset) wa utajiri
Utajiri huanzia kwenye mawazo. Watu matajiri huifikiria pesa tofauti na watu wa kawaida. Ili kujenga mtazamo wa utajiri fanya hivi:
  • Matumizi yako ya pesa yawe ya chini kuliko kipato chako(spend less than you earn)
  • Weka malengo ya kifedha ya muda mrefu.
  • Kaa katikati ya watu wenye mafanikio na maarifa ya kifedha.
2. Weka pesa benki na wekeza kwa hekima
Kuweka pesa benki peke yake hakutakufanya uwe tajiri, lakini ukiwekeza utafanikiwa. Kwahiyo badala ya kuweka pesa zako zote benki:
  • Wekeza kwenye hisa, dhamana, au mifuko ya pamoja. Kabla ya kuwekeza fanya utafiti.
  • Anzisha biashara yenye uwezo wa kukua.
  • Wekeza kwenye mali isiyohamishika(real estate) au mali nyingine zenye thamani inayoongezeka.
3. Uwe na vyanzo vingi vya mapato
Chanzo kimoja tu cha mapato hakitoshi sana kama unataka kupata utajiri mkubwa na wa kudumu. Watu matajiri hupata pesa kutoka kwenye vyanzo vingi vya mapato kama vile nyumba za kupangisha, gawio(dividents), au mirahaba(royalties), biashara za mtandaoni nk.

4. Dhibiti fedha zako vizuri
Huwezi kuwa tajiri kama utashindwa kudhibiti au kusimamia fedha zako. Kwahiyo:
  • Uwe na bajeti na ufuatilie(track) matumizi yako.
  • Epuka madeni yasiyo ya lazima na tumia pesa kwa busara.
  • Uwe na akiba ya dharura(emergency fund) ili uweze kuyakabili matukio au hali zisizotarajiwa.
5. Elimu haina mwisho. Jifunze tena na tena masuala ya kifedha
Dunia ya kifedha inabadilika kila wakati. Watu matajiri huendelea kujifunza kwa:
  • Kusoma vitabu kuhusu utajiri na usimamizi wa fedha.
  • Kuhudhuria semina za biashara na uwekezaji.
  • Kujifunza kutoka kwa washauri na wataalamu wa fedha.
6. Uwe mvumilivu (be patient and persistent)
Utajiri hauoti kama uyoga. Wajasiriliamali wengi walichukua miaka kadhaa kuwa matajiri. Hivyo uwe mvumilivu, na usikate tamaa unapokutana na changamoto.

7. Ukianza kupata utajiri, wafundishe wengine mbinu ulizotumia
Andika vitabu, uza. Wafundishe wengine masuala ya kifedha kwenye semina, warsha, makongamano, kwa malipo.

Ukishakuwa tajiri usimsahau Mungu.
Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako... jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake...( Kum 8:10-11).

Ukimsahau Mungu Maandiko haya yanaweza kukuhusu:
“Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. Akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje?

Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanaitaka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu anayejirundikia mali kwa ajili yake mwenyewe, lakini si tajiri mbele ya Mungu.”( Luka 12:15-21)

View attachment 3236711
Wewe una utajiri (u milionea) kiasi gani kwanza?.
Tuanzie hapo
 
Kwani mbinu hizo zimekuambia ukitaka kuwa tajiri uniulize kwanza utajiri wangu ni kiasi gani?
 
Tunataka kujua hizi mbinu kama unazijua je na wewe unazitumia pia?? Maaana hakuna asiependa kua na pesa.
 
Back
Top Bottom