Zijue Mbinu Hizi za Kuwa Tajiri("Milionea")

Kama unataka facts, plan to visit Israel. Watakuonyesha mambo mengi yaliyoandikwa kwenye Biblia, including kaburi la Yesu linalothibitisha Yesu alikuwepo duniani miaka 2000+ iliyopita. Utauona mto Yordan aliobatizwa Yesu nk. Hizo ni facts kwamba Yesu alikuwepo duniani na kabla hajapaa alisema anaenda kutuandalia makao.

Huo mfano wa mtoto na njaa hauna mashiko. Mimi tangu nimeokoka miaka mingi imepita sijakosa chakula. Yesu alisema tukiutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake tutazidishiwa chakula na mavazi.

So, my God isn't cruel. Ananilisha na anabariki kazi za mikono yangu sawasawa na jinsi alivyoahidi.
 
Tunataka kujua hizi mbinu kama unazijua je na wewe unazitumia pia?? Maaana hakuna asiependa kua na pesa.
Ndio, ninazitumia. Baada ya kuhakikisha kuwa ni mbinu za kweli nikaona niwashirikishe na wengine. Waswahili wanasema: "kizuri kula na mwenzio."
 
Ukipambana ukawa tajiri, usifikiri umepambana mwenyewe. Bado Mungu anakuwa amehusika kukufanikisha.
Mungu gani anashindwa na ameshindwa kuwafanikisha maelfu ya watoto na wanawake wanaoteseka na wanaokufa kwa shida mbalimbali duniani ikiwemo njaa, vita, magonjwa, umaskini na majanga ya asili..👇

Huyo Mungu kama yupo aanze kwanza kuwasaidia maelfu ya watoto na wanawake wanaoteseka duniani, Ndipo nitajua ana uwezo, upendo na huruma.

Unless otherwise huyo Mungu ni muovu, mkatili, muuaji, dikteta, sadist na mjinga.

Mungu huyo hafai kabisa anastahili kufurushwa huko alipo.
Huyo Mungu kama yupo anastahili kufurushwa kabisa.

Maana ni Mungu mjinga na mpumbavu sanaaaa!!!
 
Yesu kuwa kaishi haina uhusiano na hoja ulizojenga, that is a non sequitur logical fallacy.

Kama kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa nini karuhusu ulimwengu unaoweza kuachia baya lolote liweze kufanyika kwa kiumbe chake hata kimoja hata kwa sekunde moja tu?

Hujajibu swali hili.

Unaniambia Yesu anatuandalia makao mbinguni.

Mimi sijauliza kuhusu mbinguni, ambako huwezi hata kuthibitisha kuwa kupo kweli.

Mimi nimekuuliza kuhusu ulimwengu huu ambao upo na tunaujua.

Hujajibu swali uliloulizwa na swali ulilojibu hujaulizwa.
 
Mungu gani anashindwa na ameshindwa kuwafanikisha maelfu ya watoto na wanawake wanaoteseka
Hakuna jambo linalomshinda Mungu. Hujasoma jinsi Yesu alivyowalisha watu elfu tano kwa mikate mitano tu na samaki wawili? Walikula wakashiba na kusaza. Ni ahadi ya Mungu hata leo kwamba tukiutafuta ufaalme wa Mungu na haki yake yote, atatuzidishia chakula na mavazi.
Sikiliza Mfalme Daudi anavyosema katika Zaburi 37:25 BHN
Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu, au watoto wake wakiombaomba chakula.

Shida na matatizo tunayoyaona katika dunia hii yametokana na sisi wenyewe wanadamu. Tusimlaumu Mungu. Mwanadamu wa kwanza alipoumbwa aliambiwa asile matunda ya mti uliokuwa katikati ya bustani akakaidi agizo hilo. Matokeo yake kifo kikaingia na tabu zote tunazoziona leo duniani.

Bado Mungu aliupenda ulimwengu akamtoa Yesu aje duniani, afe msalabani ili kila amwaminiye awe na uzima wa milele. Yesu kabla hajapaa alisema anaenda kutuandalia makao mbinguni. Katika makao hayo hakutakuwa na njaa, wala magonjwa wala vita wala kilio wala kufa. Ni raha ya milele. Wanaokataa kumwamini Yesu ndio watakaotupwa katika moto wa milele.

Ujio wa Yesu umekaribia. Yesu alizitaja dalili za kuja kwake na za mwisho wa dunia. Dalili hizo ni pamoja na njaa, vita na magonjwa. Kwahiyo ndugu, badala ya kumlaumu Mungu, Tubu dhambi zako; mwamini Bwana Yesu na ukiri kuwa Yesu ni Bwana. Ukifanya hivyo Yesu atakaporudi utakuwa miongoni mwao watakaonyakuliwa na kurithi uzima wa milele.
 
Zaburi 53:1 BHN
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu!”
 
mbinguni, ambako huwezi hata kuthibitisha kuwa kupo kweli.
Yesu alipppaa kwenda mbinguni, mashahidi walimuona, na malaika walitokea wakasema:
“Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tena namna hiyohiyo mlivyomwona akienda mbinguni.” (Matendo 1:11)
 
ulimwengu huu ambao upo na tunaujua.
Ulimwengu huujui vizuri. Ungeujua vizuri ungejua ulianzaje na utaishaje. Biblia peke yake ndicho kitabu kinachotuambia asili ya ulimwengu na mwisho wa ulimwengu
Mwa 1:1-25 SUV
"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku..."
2 Petro 3:10:
"Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia na kazi zilizomo ndani yake zitateketea."
 
kwa nini karuhusu ulimwengu unaoweza kuachia baya lolote liweze kufanyika kwa kiumbe chake
Ukimcha Mungu utaona baraka za Mungu.
Zab 91:10 SUV
Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia nyumba yako.

Hiyo ni ahadi kwa wote wanaomcha Mungu. Unamkataa Mungu ndio maana unaishi kwa kulalamika tu
 
Huyo Mungu kama yupo aanze kwanza kuwasaidia maelfu ya watoto
Watoto wadogo wana "free ticket" ya kuingia mbinguni. Wakifa wanaingia uzimani.
Mk 10:14 SUV
"...Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao."

Jililie nafsi yako
 
Asante sana kwa maarifa haya.
Hakika watakaoyaamini watavuka,lakini wanaoamini kuwa huwezi kutajirika bila kutokea familia ya kitajiri watayapita tuu.
Kweli kabisa
 
Huu si uthibitisho, haya ni mahubiri ya injiki.

Mahubiri ya injili si uthibitisho wa facts.
 
Biblia ina contradictions nyingi sana nilishawahi kukuwekea hapa ukakimbia bila kuzipangua.
 
Ukimcha Mungu utaona baraka za Mungu.
Zab 91:10 SUV
Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia nyumba yako.

Hiyo ni ahadi kwa wote wanaomcha Mungu. Unamkataa Mungu ndio maana unaishi kwa kulalamika tu
Haya ni mahubiri ya kidini, mambo ya imani. Imani si lazima iwe jambo la kweli.

Hujathibitisha huyo Mungu yupo factually.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…