Zijue Mbinu Hizi za Kuwa Tajiri("Milionea")

Hizi zote unapiga blah! blah! tu..

Maelfu ya watu hasa wanawake na watoto wanateseka sana hapa duniani na huyo Mungu wako unayehangaika kumuhubiri hapa, Hana msaada wowote kwao.

Maelfu ya watoto wanakufa kwa njaa na vita halafu huyo Mungu wako hana msaada wowote kwao.

Maelfu ya watoto wamekufa kwa vita huko Gaza, Goma DRC Congo. Huyo Mungu hajasaidia chochote.

Maelfu ya watoto wanakufa kwa njaa Huko Tigray Ethiopia, Turkana Kenya, Yemen, Syria, Afghanistan n.k

Halafu wewe unaleta hadithi uchwara za vitabuni eti Yesu aliwalisha watu Elfu 5!!!

Mbona sasa hivi hawalishi hawa watoto wanaoteseka na wanaokufa kwa njaa...👇
 
Zaburi 53:1 BHN
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu!”
Huyo Mungu aliyeumba binadamu ambao wanajisemea moyoni yeye hayupo, Wakati aliweza na anaweza kuumba binadamu wema tu watakao mtii, kumwamini na kusema yeye yupo siku zote lakini akashindwa kufanya hivyo, Yeye ndio MPUMBAVU.
 
Watoto wadogo wana "free ticket" ya kuingia mbinguni. Wakifa wanaingia uzimani.
Mk 10:14 SUV
"...Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao."

Jililie nafsi yako
Ruhusu basi mtoto wako wa kumzaa ateseke ili apate hiyo "free ticket" ya kuingia mbinguni.

Wewe unaona sawa watoto wengine kuteseka kwa kigezo eti wanapata "free- ticket" ya kwenda mbinguni, Halafu hutaki mwanao kuteseka kwa njaa, vita na magonjwa.

Huu ni unafiki.
 
Unaweza kuthibitisha kuwa shetani yupo kweli na hizo habari za shetani kuwapo si hadithi za ujinga za mapokeo tu?
Unaweza kuthibitisha kwamba shetani hayupo? na kwamba mnaoamini hivyo hamna mapokeo ya ujinga?
man,amini unachokiamini na mwingine hali kadhalika ndo maana nchi yetu ikiwaachia wananchi wake uhuru wa kuabudu au kutoabudu ilimradi wasivunje sheria.
 
Unaweza kuthibitisha kwamba shetani hayupo? na kwamba mnaoamini hivyo hamna mapokeo ya ujinga?
man,amini unachokiamini na mwingine hali kadhalika ndo maana nchi yetu ikiwaachia wananchi wake uhuru wa kuabudu au kutoabudu ilimradi wasivunje sheria.
Kwanza kabisa, falsafa ya uthibitisho inamtaka anayedai kitu kipo ndiye awe na nzigo wa kuthibitisha kitu kipo.

Kisichokuwepo hakithibitishiki kutokuwepo kwa sababu hakipo na kama hakipo utakithibitisha vipi kwamba hakipo?

Mwizi ambaye hayupo na hajaiba utapata vipi alama zake za vidole ili uthibitishe hayupo na hajaiba?

Hapo ulichofanya ni kama vile wewe unasema kuna mwizi, mimi nasema hakuna mwizi, halafu badala ya wewe kunipa mimi alama za vidole za huyo mwizi kutoka eneo la tukio, badala ya wewe kunipa video za CCTV zikionesha mwizi anaingia kuiba, badala ya wewe kunipa mashahidi waliomuona huyo mwizi, unaniambia nithibitishe mwizi hayupo.

Kama mwizi hayupo, unanitaka nithibitishe vipi kuwa hayupo?

Nikupe alama za vidole za mwizi ambaye hayupo?

Nikupe CCTV coverage ya kuonesha mwizi ambaye hayupo?

Nikupe mashahidi waliomuona mwizi ambaye hayupo?

Vitu hivyo haviwezekani kufanyika, wewe ndiye unatakiwa kuthibitisha mwizi yupo.

Thibitisha shetani yupo.
 
Uzi ulikuwa na madini mara paap! Umekuwa wa kuhubiri injili na taurati
 
Mbona sasa hivi hawalishi hawa watoto wanaoteseka na wanaokufa kwa njaa
Watu wanataka walishwe tu lakini hawataki kuzingatia vigezo na masharti ya kulishwa.
Soma:
Mt 6:25-34 SUV
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Kigezo ni hicho (in bold letters).


Tatizo ni kwamba watu wanataka walishwe halafu waendelee na uasherati wao. Wanataka walishwe halafu waendelee na ulevi wao. Wanataka walishwe halafu waendelee kuiba na kusema uongo.

Baraka za Mungu zinapatikana kwa kuzingatia vigezo na msharti: "tafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."

Mi nimeishakuambia tangu niutafute ufalme wa Mungu sijalala njaa.

Hao maelfu ya wanawake unaowasema, wote wameutafuta kwanza ufalme wake, wakamuomba Mungu awape chakula wakanyimwa?
 
Kulikuwa na haja gani kuumba binadamu duniani, Halafu tuanze kutafuta ufalme wa Mungu mbinguni?

Kwa nini tusingeumbwa mbinguni?

Kwa nini tuliumbwa duniani, Halafu tuanze kuhangaika kutafuta ufalme wa mbinguni?

Kwa nini hatukuumbwa mbinguni?

Hivi huyo Mungu wako anajielewa kweli?
 
Unamiliki ukwasi wenye thamani kiasi gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…