Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizi zote unapiga blah! blah! tu..Hakuna jambo linalomshinda Mungu. Hujasoma jinsi Yesu alivyowalisha watu elfu tano kwa mikate mitano tu na samaki wawili? Walikula wakashiba na kusaza. Ni ahadi ya Mungu hata leo kwamba tukiutafuta ufaalme wa Mungu na haki yake yote, atatuzidishia chakula na mavazi.
Sikiliza Mfalme Daudi anavyosema katika Zaburi 37:25 BHN
Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu, au watoto wake wakiombaomba chakula.
Shida na matatizo tunayoyaona katika dunia hii yametokana na sisi wenyewe wanadamu. Tusimlaumu Mungu. Mwanadamu wa kwanza alipoumbwa aliambiwa asile matunda ya mti uliokuwa katikati ya bustani akakaidi agizo hilo. Matokeo yake kifo kikaingia na tabu zote tunazoziona leo duniani.
Bado Mungu aliupenda ulimwengu akamtoa Yesu aje duniani, afe msalabani ili kila amwaminiye awe na uzima wa milele. Yesu kabla hajapaa alisema anaenda kutuandalia makao mbinguni. Katika makao hayo hakutakuwa na njaa, wala magonjwa wala vita wala kilio wala kufa. Ni raha ya milele. Wanaokataa kumwamini Yesu ndio watakaotupwa katika moto wa milele.
Ujio wa Yesu umekaribia. Yesu alizitaja dalili za kuja kwake na za mwisho wa dunia. Dalili hizo ni pamoja na njaa, vita na magonjwa. Kwahiyo ndugu, badala ya kumlaumu Mungu, Tubu dhambi zako; mwamini Bwana Yesu na ukiri kuwa Yesu ni Bwana. Ukifanya hivyo Yesu atakaporudi utakuwa miongoni mwao watakaonyakuliwa na kurithi uzima wa milele.
Huyo Mungu aliyeumba binadamu ambao wanajisemea moyoni yeye hayupo, Wakati aliweza na anaweza kuumba binadamu wema tu watakao mtii, kumwamini na kusema yeye yupo siku zote lakini akashindwa kufanya hivyo, Yeye ndio MPUMBAVU.Zaburi 53:1 BHN
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu!”
Ruhusu basi mtoto wako wa kumzaa ateseke ili apate hiyo "free ticket" ya kuingia mbinguni.Watoto wadogo wana "free ticket" ya kuingia mbinguni. Wakifa wanaingia uzimani.
Mk 10:14 SUV
"...Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao."
Jililie nafsi yako
OkAsante kunitabiria u-trilionea 🙂
Unaweza kuthibitisha kwamba shetani hayupo? na kwamba mnaoamini hivyo hamna mapokeo ya ujinga?Unaweza kuthibitisha kuwa shetani yupo kweli na hizo habari za shetani kuwapo si hadithi za ujinga za mapokeo tu?
Kwanza kabisa, falsafa ya uthibitisho inamtaka anayedai kitu kipo ndiye awe na nzigo wa kuthibitisha kitu kipo.Unaweza kuthibitisha kwamba shetani hayupo? na kwamba mnaoamini hivyo hamna mapokeo ya ujinga?
man,amini unachokiamini na mwingine hali kadhalika ndo maana nchi yetu ikiwaachia wananchi wake uhuru wa kuabudu au kutoabudu ilimradi wasivunje sheria.
Watu wanataka walishwe tu lakini hawataki kuzingatia vigezo na masharti ya kulishwa.Mbona sasa hivi hawalishi hawa watoto wanaoteseka na wanaokufa kwa njaa
Kulikuwa na haja gani kuumba binadamu duniani, Halafu tuanze kutafuta ufalme wa Mungu mbinguni?Watu wanataka walishwe tu lakini hawataki kuzingatia vigezo na masharti ya kulishwa.
Soma:
Mt 6:25-34 SUV
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Kigezo ni hicho (in bold letters).
Tatizo ni kwamba watu wanataka walishwe halafu waendelee na uasherati wao. Wanataka walishwe halafu waendelee na ulevi wao. Wanataka walishwe halafu waendelee kuiba na kusema uongo.
Baraka za Mungu zinapatikana kwa kuzingatia vigezo na msharti: "tafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."
Mi nimeishakuambia tangu niutafute ufalme wa Mungu sijalala njaa.
Hao maelfu ya wanawake unaowasema, wote wameutafuta kwanza ufalme wake, wakamuomba Mungu awape chakula wakanyimwa?
Unamiliki ukwasi wenye thamani kiasi ganiWatu wengi wana ndoto za kuwa matajiri. Wanafanya kazi kwa bidii usiku na mchana ili wawe matajiri. Hata hivyo ni wachache wanaofanikiwa kuupata utajiri. Leo nakutajia baadhi ya mbinu muhimu za kupata utajiri au kuwa milionea/bilionea – sizungumzii utajiri unaopatikana kwa bahati au kwa kurithi.
Utajiri unapatikana kwa kutumia mbinu sahihi, nidhamu, na uthabiti. Kama kweli unataka kuwa tajiri, tumia mbinu hizi:
1. Anza kuwa na mtazamo(mindset) wa utajiri
Utajiri huanzia kwenye mawazo. Watu matajiri huifikiria pesa tofauti na watu wa kawaida. Ili kujenga mtazamo wa utajiri fanya hivi:
2. Weka pesa benki na wekeza kwa hekima
- Matumizi yako ya pesa yawe ya chini kuliko kipato chako(spend less than you earn)
- Weka malengo ya kifedha ya muda mrefu.
- Kaa katikati ya watu wenye mafanikio na maarifa ya kifedha.
Kuweka pesa benki peke yake hakutakufanya uwe tajiri, lakini ukiwekeza utafanikiwa. Kwahiyo badala ya kuweka pesa zako zote benki:
3. Uwe na vyanzo vingi vya mapato
- Wekeza kwenye hisa, dhamana, au mifuko ya pamoja. Kabla ya kuwekeza fanya utafiti.
- Anzisha biashara yenye uwezo wa kukua.
- Wekeza kwenye mali isiyohamishika(real estate) au mali nyingine zenye thamani inayoongezeka.
Chanzo kimoja tu cha mapato hakitoshi sana kama unataka kupata utajiri mkubwa na wa kudumu. Watu matajiri hupata pesa kutoka kwenye vyanzo vingi vya mapato kama vile nyumba za kupangisha, gawio(dividents), au mirahaba(royalties), biashara za mtandaoni nk.
4. Dhibiti fedha zako vizuri
Huwezi kuwa tajiri kama utashindwa kudhibiti au kusimamia fedha zako. Kwahiyo:
5. Elimu haina mwisho. Jifunze tena na tena masuala ya kifedha
- Uwe na bajeti na ufuatilie(track) matumizi yako.
- Epuka madeni yasiyo ya lazima na tumia pesa kwa busara.
- Uwe na akiba ya dharura(emergency fund) ili uweze kuyakabili matukio au hali zisizotarajiwa.
Dunia ya kifedha inabadilika kila wakati. Watu matajiri huendelea kujifunza kwa:
6. Uwe mvumilivu (be patient and persistent)
- Kusoma vitabu kuhusu utajiri na usimamizi wa fedha.
- Kuhudhuria semina za biashara na uwekezaji.
- Kujifunza kutoka kwa washauri na wataalamu wa fedha.
Utajiri hauoti kama uyoga. Wajasiriliamali wengi walichukua miaka kadhaa kuwa matajiri. Hivyo uwe mvumilivu, na usikate tamaa unapokutana na changamoto.
7. Ukianza kupata utajiri, wafundishe wengine mbinu ulizotumia
Andika vitabu, uza. Wafundishe wengine masuala ya kifedha kwenye semina, warsha, makongamano, kwa malipo.
Ukishakuwa tajiri usimsahau Mungu.
Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako... jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake...( Kum 8:10-11).
Ukimsahau Mungu Maandiko haya yanaweza kukuhusu:
“Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. Akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje?
Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanaitaka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu anayejirundikia mali kwa ajili yake mwenyewe, lakini si tajiri mbele ya Mungu.”( Luka 12:15-21)
View attachment 3236711
Kiranga kama Kiranga 😂😂Unaweza kuthibitisha kuwa shetani yupo kweli na hizo habari za shetani kuwapo si hadithi za ujinga za mapokeo tu?