Zijue nchi zenye waafrika wengi zaidi nje ya Afrika

ni kwanini ngozi nyeusi inazaraurika sana!!?
Kuna wanaoamini mwonekano wetu ni mbaya. Wengine ni wivu tu kwasababu ya vipaji vyetu na mwonekano wetu pia. Kingine ni tabia zetu za uharibifu na uhalifu.
All in all ukijitambua na kujikubali na kujua thamani yako na nguvu yako hakuna wa kukutisha dunia hii. Never!!!
 
Asikidanganye mtu, hao weusi wa marekani kwa kiasi fulani wanachukia sana kuhusishwa na bara la Africa. Ni kweli wapo very proud kuwa black. Wanaprefer kujiita blacks kuliko african americans. Halafu huwa wanabagua waafrika wanaoishi US.
Hapana wengi zaidi bado wanaipenda Afrika. Hawapendi neno African American sababu linawatenga na kuwabagua wakati wao wameshiriki kuijenga America kama ilivo kwa wazungu ambao hawaitwi kutokana na sehemu zao za Asili. Kuhusu kupatana na waafrika mbona hawana shida nao ndo mana wasanii wao wanafanya sana collabo na waafrika siku hizi ila kinachoweza kuweka kadaraja ni tamaduni tu coz hizi jamii mbili zimetengana muda mrefu sana.
 
Shida mademu wakiafrika ni vizinga na kutudharau sana sisi wanaume wa kiafrika
 
Kwa kweli kupenda rangi nyeupe ni ulimbukeni mkubwa sana wa waafrika unaohitaji kupingwa (siwabagui watu weupe) coz inatokana na saikolojia ya mwafrika kudharau weusi. Ni kweli kila mtu anamapenzi yake ila lazma tutafakari dhamira ya hayo mapenzi. Hata huku afrika watu wanaona wasichana weupe ndo warembo na kudharau wale weusi. Unakuta mtu mama yake mweusi tiii ila hataki kuoa msichana mweusi. Kuna makabila wanatoza mahali kubwa kwa wasichana weupe(wasukuma).

Nikija kwa hawa watu wa pale Andaman ni kweli wapo ila population yao ni ndogo sana now yapata around 450 maximum. Hawa waliondoka afrika yapata miaka 20,000 iliyopita hata dna zao hazifanani na za waafrika ila zinakaribiana na za watu wa asia ya kusini huko karibu na wao wanapoishi. Jamii za watu weusi zipo kadhaa kusini mwa Asia hasa India kusini, Bangladesh, Mynamar, Malaysia, Papua Guinea na Waaboriginal wa Australia, ila hawa walitoka Afrika zamani sana kiasi kwamba kutokana na kutengana nasi wamekua tofauti sana nasi genetically.
 

Nakubaliana na wewe na kuhusu DNA za Andamanese kuwa tofauti na za watu wengine kuna comment ipo chini nilielezea zaidi kwamba kuna kipindi wanasayansi walitaka blood samples zao wakiamini zinaweza kuwa na kitu cha tofauti au profoundly significant ila kwa sababu ya pingamizi la kuwaingilia walishindwa kufanya hivyo.
 
Mkuu Bufa, nimevutiwa mno na bandiko lako. Bravo! Hao jamaa ni nini kinawamaliza? Au ni mkakati wa jamii ya rangi nyingine?
Suala la mkakati hatuwezi kuacha kilitilia maanani. Watu weusi wamemalizwa sana sehemu kadhaa dunia hii. Pale Papua Guinea serikali ya Indonesia imewamaliza sana wapapua wanaodai uhuru wao, waarabu machotara wa sudan wamemaliza sana makabila ya kiafrika pale Darfur.
 

Wea iz e shithole El-Salvador??
 
Shida mademu wakiafrika ni vizinga na kutudharau sana sisi wanaume wa kiafrika

Kwanza wanaume kwa wanawake wote wanatamani wazungu. Kati ya waafrika 10 9 kati yao wanawish waoe/waolewe na wazungu kabla ya kuwaza mambo ya mizinga au dharau.

Pili, huwa nashangaa sana pale amabo muafrika anawasema vibaya waafrika wenzake ila akio mzungu anakubali kila kitu bila pingamizi. Mathalani, unakuta njemba ya kiafrika inasema haiwezi kufua, kupika, kudeki, kushida na mtoto nk ila akioa mzungu anakubali kufanya yote haya bila shurti. Nadhani kila mtu anashuhudia hili.

Ukioa mzungu nini kinachokubadilisha na kuwa mpole ghafla? Unagundua tatizo ni inferiority complex kwamba hawawezi kuendeshwa na mweusi mwenzao ila mzungu akisema wanakubali.
 
Ambacho sijaelewamni kwamba
Waarabu ndio wali Fanya biashara ya utumwa kama tunavyosomeshwa!

Sasa ilikuwaje waafrika hawa wawepo kwenye nchi hizi za masaint kwa idadi kubwa nanmna hii!?

Waliwapataje jamani?

Walikuwa wanawafanyia nini mbali kote huko?
Au ndio walikuwa wanawafundisha usister na upadri ili warudi Afrika kueneza neno la bwana?
 
Mm nimebahatika kuhishi nchi za West Africa Ghana,Nigeria,Senegal,Togo,Mali nk.Hawa jamaa walioko huko America wengi wametokea eneo hili.Kuna kabila la Wafulani.Hawa wanafanana sana na wanyarwanda na kila nikimuangalia mcheza Soka Ronaldinho au Willian wa Chelsea hawa ni pure Fuani people.Mwanamuziki Ashanti for sure ametokea ashanti,Ghana.Senegali ni warefu sana na kila nikiangalia wacheza mpira wa kikapu wa marekani.....Nigeria ni wazuri kwenye muziki na ukiangalia wanamuziki wengi weusi Marekani possibly wametokea hapa.Asante mleta mada.Inafundisha!
 

Sijui umeosoma historia gani kama hujui Triangular Slave Trade, maeneo iliyogusa na athari zake.

Hakika kuna ombwe kwenye elimu yetu.
 
Kweli kabisa ni ulimbukeni uliopitiliza
 

Mkuu hilo lipo wazi, weusi wote wa Amerika ni kutoka W.Africa. Walichukuliwa toka huko kwa sababu kuu mbili, mosi, walitaka watu wakubwa wenye miili mikubwa na nguvu ili wafanye kazi za kutumia nguvu na ukiangalia hadi leo West Africans wana miili mikubwa kuliko watu wengine wote wa Africa, pili ilikua kwa sababu za ukaribu. Ni karibu kutoka nchi kama Nigeria kwenda Amerika kuliko wangekuja kuchukua watu toka nchi kama Malawi(wadogo, wafupi na mbali yani landlocked) hasa ukizingatia usafiri wa wakati huo.
 
India na Pakistani kuna jamii ya Sidi hawa walitoka Afrika Mashariki walichukuliwa kama watumwa na waarabu kwa ajili ya watawala wa India na Pakistani. Wapo hadi leo hii wanafikia 50,000 ila ndo hivo wamemezwa na wahindi maana hata kuna wahindi wengi tu hawajui kama wapo ila bado wana tamaduni za ngoma za kiafrika hadi leo.
Unaweza kuwaona hapa au ukigoogle utapata sources zaidi
 
Fulani ambao wanaongea lugha ya fula wanatrace asili Yao Ethiopia. Wamesambaa Sana west Africa ambapo wengi wao wapo Guinea Na Northern Nigeria. Ni nomads watu wakuhamahama Na mifugo. Pia Ni minorities Ghana, Gambia, Senegal, sieraleone, ivory coast, Liberia. Lakini wengi wao wako Guinea Na nothern Nigeria.

Pia wale anti balaka walikuwa wanawaua central Africa Republic ambao ni Seleka Ni jamii ya Fulani.

Pia Western Sudan wapo Fulani. Karibia Fulani wote Ni waislam.

Ni conservative Na restrictive Na Mila zao. Ni nadra Fulani kuoana Na jamii nyingine. Wote kwa jumla wako milion 20.

Mohamadou Buhari rais Wa Nigeria ametoka jamii ya Fulani.
 
very interesting
 
Halafu hizo nchi za Caribbean zenye weusi wengi kuliko wrupe ndio masikini sana na ushirikina umejaa huko.

Hao jamaa unakuta wana umasikini hata Afrika nafuu.

Hapo ndio unagundua kuwa watu weusi ni matatizo tupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…