Zijue tofauti za kihuduma na Maslahi kati ya Zanzibar na Tanganyika

Zijue tofauti za kihuduma na Maslahi kati ya Zanzibar na Tanganyika

Alafu nilivyo kuwa chuo kikuu, walikuwa ni watu wakijitenga, hawashirikiani na wabara,, sisi wabara tuko bize kupambana na maisha,wao kila siku wanajishuku kuwa wanatengwa ,

Ila sasa wanavyokimbilia kugombania vyeo ilihali uwezo wa kielimu hawana na hata TU kuongea Kwa hoja hawajui,
Sisi wabara tunabaki tunawashangaa mbona hapa bara hatuna ubaguzi wa kumbagua MTU yoyote.
 
Hayo yote yanahusiana nini na uliyaanzishia uzi? Wazanzibari wana kosa gani katika yale uliyayaanzishia uzi? Waliwafuata muungane nao?

Na Waislam wa Zanzibar watabaki kuwa ndugu zetu sisi Waslam wa Bara.

Mengine naona ni maneno meeeeengi umeniandikia.
Undugu wa kunyonyana, au unadhani muislamu peke yako?
Sio kwa mwali, Hadi kwa kungwi kuliwe.
 
Uliposema tu Ocean Road haihusiki na zanzibar ndio nimejua we ni bogus
Ni kweli, kwani huenda neno hili "bogus" lina maana nyingine na ile ya asili. Niliposema Ocean Road na uhusiano wake na Zanzibar ni kwenye sehemu zilipo hizi sehemu mbili; moja iko Bara na nyinine iko visiwani. Hivi kwa kuwa unafundisha na kutibu ocean road ndo unaijua Zanzibar?

Ni majigambo tu na kule kwetu huwa hatuna majigambo. We jidanganye tu!
Nakupa Assignment nenda Hosp ya Mnazi mmoja Zanzibar kawaulize mnahusika vipi na
Ocean Road na kwanini mnaenda ocean Road kwa training?
Hivi hii , kwa ufahamu wako, inahitaji kuuliza kwanini wanakuja ocean road kujifunza? Nikuambietl tu kwamba mtu kuenda kusoma popote, sio ocean road tu, bali pia katika vyuo au taasi nyingine yeyote, ni kupata taaluma. Haina uhusiano wowote na mkufunzi huyo kujua mwanafunzi wake kwao wana nini. Hii ni dalili ile uliyoiita bogus. Hiki ni moja ya kiashiria cha huo ubogus uliousema. Jitafakari, usikurupuke.
Usiache kuja kuqndikq majibu hapa . Kishq urudie ku soma post
Mkuu nadhani hili linajidhihirisha kwa niliyoandika hapo juu. Usisahau kanuni za kuandika. Kabla ya kunyanyua kalamu, fanya rejea kwanza.
 
Ni kweli, kwani huenda neno hili "bogus" lina maana nyingine na ile ya asili. Niliposema Ocean Road na uhusiano wake na Zanzibar ni kwenye sehemu zilipo hizi sehemu mbili; moja iko Bara na nyinine iko visiwani. Hivi kwa kuwa unafundisha na kutibu ocean road ndo unaijua Zanzibar?

Ni majigambo tu na kule kwetu huwa hatuna majigambo. We jidanganye tu!

Hivi hii , kwa ufahamu wako, inahitaji kuuliza kwanini wanakuja ocean road kujifunza? Nikuambietl tu kwamba mtu kuenda kusoma popote, sio ocean road tu, bali pia katika vyuo au taasi nyingine yeyote, ni kupata taaluma. Haina uhusiano wowote na mkufunzi huyo kujua mwanafunzi wake kwao wana nini. Hii ni dalili ile uliyoiita bogus. Hiki ni moja ya kiashiria cha huo ubogus uliousema. Jitafakari, usikurupuke.

Mkuu nadhani hili linajidhihirisha kwa niliyoandika hapo juu. Usisahau kanuni za kuandika. Kabla ya kunyanyua kalamu, fanya rejea kwanza.
Unajichanganya sana dogo kwenye responses zako. Jifunze kusomq kwa ufahamu
 
Megalodon ,Benjamini Netanyahu jaribuni kupunguza chuki coz bandiko lako Megalodon limejaa chuki, hasira, jazba, mhemko,papara na visasi.Mara nyingi ukiwa na vitu hivi huwezi kuwa mkweli.

Kila Mzanzibari ni Mtanzania ila siyo kila Mtanzania ni Mzanzibari.Ukilijua hili hupati tabu.

Kuhusu Nyerere: Alicheza kama pele kuhusu muungano coz of vita vya kimslahi baina ya West vs Mashariki kwa wakati huo.

Historia huwa na mtindo wa kujirudia: Kinachotokea Ukraine ndicho wakubwa wa dunia walitaka kiwe hivyo kwa Zanzibar.

Zanzibar ilitakiwa itumike kama uwanja wa kugombania ufalme baina ya West vs Mashariki.Unafikiri Tanganyika ingepona????? Ungekuwa wewe ungefanyaje??

Kero kuhusu Muungano: Duniani kote hakuna muungano usiokosa kero.Mara nyingi hizi kero hutatuliwa kulingana na nyakati husika.Muungano huu umetatua kero mbalimbali na kero huwa haziishi leo wala kesho!
Upo subjective sana . Nimeweka fact , please , pingana na fact sio mimi
 
Unajichanganya sana dogo kwenye responses zako. Jifunze kusomq kwa ufahamu
Unajitia sana kujua lakini hamuna kitu. Wewe ni debe bovu haliwachi kutika. Karibu sana kwa mazungumzo. Siku zote ukiujua huu, huu huujui. Jitahidi kujua kujadili na sio kutukana na kudharau.
 
Unajitia sana kujua lakini hamuna kitu. Wewe ni debe bovu haliwachi kutika. Karibu sana kwa mazungumzo. Siku zote ukiujua huu, huu huujui. Jitahidi kujua kujadili na sio kutukana na kudharau.
Kujitia ndio nini ?

Najua wewe unatetea maslahi yenu

RELAX .yote niliyoongea ni FACT . Lengo kuu ni kuboresha maana wote sisi ni Tanzania.

Sasa inakuaje some members have high benefits kuliko wengine. ? Nikitoa RAV 4 Dar kodi inaenda Mil 12 while ZNZ kodi mil 5 , but wote ni nchi moja. Mzenji akitoa vitu Dar kule Zanzibar hachajiwi ila mm
Nikitoa mzigo Zenji nachajiwa Zanzibar nq
Dar ; huo ni nini ? And still tunasema ni nchi moja

Hatutaki kuvunja muumgano. Tunatakq Tqngqnyikq nayo iwe na serikali yake kama Zanzibar then tukutane kwenye muungano as independent countries

Sisi ni ndugu tumeoa na kuoleana na tumezaa pia huko, hata Rais wenu ni kijana wetu wa hapo Mkuranga….

Wengine kwa bahati mbaya au nzuri tulizalisha Zanzibar huko tukiwa kwenye majukumu ya kikazi na hatuwezi kukataa viumbe vyetu tuna watoto wetu na tunatumq matumizi kila mwezi kwa mama zao. Sisi ni ndugu but Muungano uwekwe sawa . Tuna option , nchi iwe kama nchi moja , ukitoq mzigo ZNZ gharama ziwe zilezile na ukitoa Dar etc etc

Zanzihar yenyewe pia inamatabaka. Kuna muunguja na mpemba.

Bado muunguja anabqguana na mpemba. Natambua wewe sio mpemba bali ni Muunguja. Natambua changamoto zenu kati ya mpemba na muunguja…

natambua Mpemba anaona anastahili kuliko muunguja.

Natambua pia ubaguzi mkubwa unatoka kwa mmpemba na sio muunguja.

Waunguja wengi wanaelimu na ndio hao wamejaa kwenye serikali

So relax natuma matumizi direct from Canada matumizi kila mwezi kwa mama yake… so muungano utadumu but tuweke mambo sawa
 
Unabishana na mimi mambo ya matibabu. Unaakili kweli wewe ?

Nimefanya kazi na ZNZ miaka mingi and nime wa train sana doctors wa ZNZ nikiwa pale Ocean road . As specialist kwenye Oncology

Health system ya Zanzibar ipo kiganjani kwangu. Matibabu ni BURE ZANZIBAR for as long as wewe ni Mzanzibar
Na mimi nilikaa pale ORCI kwa miaka miwili mkuu. Siku hizi huduma za bure kama zamani hakuna, baadhi wameziwekea malipo kama kumuona Oncologist n.k. sijui Zanzibar kama wamewekewa hii kitu.
 
1. Huduma za kiafya Zanzibar ni bure for as long as unakitambulisho cha mkazi wa Zanzibar. Matibabu na dawa za Figo, Kansa na magonjwa yote ni bure. Gharama yako ni nauli ya kufika Hospital. Kwa Tanganyika hakuna matibabu bure, kama umefanikiwa kuwa na Bima itakuwa ni faida kwako. Kati ya watanganyika takribani 58M , wenye Bima hawazidi asilimia 18…. Hii inamaana zaidi ya 80% ya watanganyika wanapaswa kutumia fedha zao kwenye afya

2. Ushuru wa magari, kwa mfano kuitoa IST zanzibar ni Kati ya 2.5 hadi 3.5 aidha kwa bara kuitoa IST ni takriban 5.7 hadi 6.4M

3. Mzanzibar anaweza kuajiriwa kwenye serikali ya mapinduzi na
serikali ya Jamhuri kwa mfano, mbunge wa makunduchi anao uhuru pia wa kugombani ubunge wa eneo lolote la Tanganyika au mtumishi wa serikali ya mapinduzi anaweza kuingia kwenye serikali kuu ya Jamhuri.Hii ni ngumu Sana Mtangqnyika kuingia Serikali ya mapinduzi na kuhodhi vyeo

3. Umiliki wa Ardhi, Mzanzibar anayohaki ya kumilili ardhi Zanzibar na Tanganyika; kwa Mtangqnyika ni ngumu kuhodhi ardhi ya zanzibar unless ushirikiane na Mzanzibar mwenye kitambulisho cha makqzi ya Zanzibar

4 Mali asili za Tanganyika kama madini na mafuta ni mali za URT, mali za Islands sio mali za URT . Mfano gesi
Iliyogundulika ZNZ sio mali ya URT but gesi ya Mtwara ni mali ya Tanganyika na ZNZ

5. Bandari ya Dar es salaam na Bandari zote Tanganyika ni bandari za URT ila bandari ya Zanzibar sio Bandari ya URT na mapato yake yanainufaisha zanzibar tu . Aidha, Bandari ya DSM imeuzwa kwa waarabu na kupelekea gharama za bidhaa kupanda snaa maana jamaa wanadai wanatumia vifaa vya kisasa hivyo lazima kodi iwe juu. Kwa wale wanaoagiza bidhaa nje watathibitisha hili. However, maumivu haya ya kupanda kwa bei hayahusiani na Zanzibar

6. Deni , fedha zinapokopwa na Serikali ya URT , fedha hizo pia zinaenda kuinufaisha sehemu ya ZNZ ikiwa ni sehemu ya URT. Ila kwenye malipo, Serikali ya URT inatumia resources za Tanganyika kufanya malipo ya deni hilo. Halikadhalika, pesa zinazokopwa na Zanzibar ni kwa ajili ya matumizi ya Zanzibar tu

7. Mkopo wa HELSB. Zanzibar wanapata Mkopo wa HELSB kwa asilimia 100 , lakini pia kuna fungu la serikali ya mapinduzi inawapatia kama gharama za kujikimu. ( study allowance and accommodation) Kadhalika, Mtangqnyika anapata mkopo kwa asilimia, wapo watakaopata 100 na asilimia 80, etc lakini pia hawana access nyingine na hawawezi kuingia kwenye study allowance ya Zanzibar

8. Scholarships, Scholarships za kusoma nje kwa ajili ya URT Mzanzibar ataomba kama atakavyoomba mtangqnyika na wote watagombania, lakini kuna scholarship zinazokujq kwa ajili ya zanzibar tu , hizo haziwi shared tanganyika na mtanganyika huwezi kuzijuq wala kuziomba. Only for Zanzibars chini ya SMZ

Taifa bado linachangamoto nyingi
Mzanzibar akiugua akapewa rufaa kwenda Muhimbili anatibiwa Bure( SMZ inalipa gharama zote) wakati Mluguru wa Matombo akipewa rufaa kwenda Muhimbili , anatakiwa kulipia gharama za matibabu.
 
Na mimi nilikaa pale ORCI kwa miaka miwili mkuu. Siku hizi huduma za bure kama zamani hakuna, baadhi wameziwekea malipo kama kumuona Oncologist n.k. sijui Zanzibar kama wamewekewa hii kitu.
Hakuna mahali nimesema ORCI huduma ni bure. Bali nimesema Mnazi mmoja Znz huduma ni bure ikiwemo za Saratani. Hayo madawa ya mil 3 , kule znz wanapewa bure. Dawa na Huduma ZNZ ni bure as we speak

Tanganyikq ili upate bure ni mchakato mrefu na unaweza kufia njian
 
He was not smart , alifocus kwenye ulinzi tu
Sijaelewa hapa nyerer ameingiaje, kwa sababu wakati wa mwalimu matibabu ilikua ni bure, wanafunzi wa sekondari tulikua tunasafirishwa bure, mwalimu kaingizwaje hapa?
 
Mimi ningeulizwa swali kama ifuatavyo: Je Tanganyika na Zanzibar ziliungana?
Jibu langu ningejibu HAZIKUUNGANA BALI ZINA MASHIRIKIANO KATIKA BAADHI YA MAENEO LKN HAZIJAUNGANA, PERIOD.
Hiyo ni kwa tafsiri/mawazo yangu binafsi. Naomba msinifuate inbox, tumalizane hapa hapa
 
Back
Top Bottom