Zile kelele za Bandari zote zimeuzwa/ kapewa mwarabu zimeishia wapi?

Huo ujumla wa IGA ni kama ujumla wa kwenye mikataba ya economic integration, mathalani East African custom union ina kipengele cha free movement of capital and labour, so nchi wanachama kuwa na haki ya kuwekeza au kuajiriwa nchi husika haimanishi mie nikienda kufungua branch Uganda ntajiendea Tu mzima mzima kama nipo tz, hapana ntaenda huko lzm ntakuja kusaini HGA Ila ntapewa fair Kwa kuwa ni mchama tofauti na atakavyopokelewa mnigeria.
 
Unaandika ujinga, kama DP World wangekuwa wameanza kufanya kazi hapo bandarini ndo ungeleta huu utumbo wako hapa.
 
Hahahahahaha

Wameitoa lini hii? Sijaisikia

Hawa jamaa na vibaraka wao TEC kwa santuri za uongo kweli hawajambo
Wewe ni mpuuzi wa kiwango cha juu sana. Unachekelea nchi yako kupewa watu bure, subiri na ombea mungu akupe uhai mrefu uje ujionee madhila ya kutawaliwa na mwarabu
 
Kwa mujibu wa habari zisizo rasmi, maaskofu uchwara wamekemewa vikali sana kutokea vatikano.

Wameambiwa chezeni na wote msicheze na uwekezaji wa UAE.

Hawa watu walikuwa hawaelewi kama papa ni swahiba mkubwa na Mfalme wa Dubai na wazee wa UAE?

 
Ni kwanini Serikali kupitia Waziri mkuu, Spika wa Bunge, Waziri wa miundo mbinu na uchukuzi, mawakili wa serikali, msemaji wa serikali na wengine walikuwa wakikanusha kwamba huo si mkataba? Walikuwa wanatudanganya waTanganyika?, kwanini watudanganye?

Sasa kwakuwa serikali haijatengua bado kauli yake kwamba hayo ni makubaliano, na si mkataba.., basi tutaendelea kuihoji serikali ituoe tofauti ya Makubaliano na mkataba, hadi pale watapoibuka hadharani nankutuambia kwamba walikuwa wanatudanganya, na watueleze sababu za kutudanganya. Tunasubiri majibu ya hii hoja ya kwanza. Na tuelezwe UKOMO!

Tuendelee na ya pili...
 
Sasa huoni ulichosema wewe ndio kile kile ninachohoji mimi, kwamba kwanini tumesaini mkataba ambao unatuzuia sisi kuingia makubaliano na mwekezaji mwingine kwenye bandari nyingine yeyote ile ndani ya Tanganyika bila ruhusa ya DPW? Huu utumwa tuliojiingiza ni kwa faida ya nani?
 
Acha kulisha maneno watu wewe, hao wote hawajawahi kusema hivyo Bali wamekuwa wakifafanua kuwa, IGA ni mkataba/makubaliano ya awali na kuna mkataba/makubaliano wa HGA ndo utaeleza maeneo mahususi.
 
Njia ya muongo sikuzote huwaga ni Fupi huyo Tundu Lissu mwenyewe sasa hivi yupo na ajenda ya ngorongoro kaona huku kwenye bandari hakuna tena nafasi ya kushika watu masikio
 
Sasa hii ndio inaeleza kile kile tunachohoji, kwamba ni kwanini tuombe ruhusu kabla ya kuingia makubaliano na mwekezaji mwingine juu ya uendelezaji wa bandari nyingine yeyote ndani ya Tanganyika? Yaani sisi tumpe yeye taarifa?! Yeye kama nani ndani ya nchi hii?! Mmmetuingiza kwenye huu utumwa kwa faida ya nani?
 
Katka hoja yako namba 3 nionyeshe Panasema atapewa aridhi na fidia italipa serikali. Naomba usome vizuri kifungu chote cha naneView attachment 2744975
Hujui kusoma au wewe ni hamnazo?! Hicho kipengele sisi kinasema sisi tunatakiwa tuchukue hatua zote zinazohitajika ili DPW apate ardhi kwa uwekezaji wake kwenye mradi wowote ule wa bandari anaotaka kuufanya? Sasa hatua ni zipi?!

Utachukua Ardhi ya mtu bila kulipa fidia? Na anaetakiwa kuchukuwa hatua zote ni sisi, sasa hiyo ya kulipa fidia sio hatua?!

Au kuondoa watu kupisha mradi, hiyo sio hatua? Na si imesemwa hapo kwa hatua zote tutachukua sisi, sivyo?!
 
Sema we ndo unaelewa kinyume kinyume, dpw ni kampuni credible sasa tayari Una mkataba naye wa HGA dar na anachapa kazi vizuri then ukaona kuna uhitaji wa mwekezaji mwanza sasa kuna umuhimu gani wa kwenda kuanza mazungumzo mapya na kampuni ingine wakati Una mdau wako tayari ushalizishwa na kazi yake? Kama dpw ataboronga HGA ya dar then TPA akawa anatafuta mwekezaji bandari ya mwanza, IGA haimbani TPA kutafuta mwekezaji mwingine na ndomana hata sasa anatafuta mwekezaji gati na8 coz hajaingia HGA na dpw katika Hilo eneo hususi Ila tayari Wana IGA.
 
Ndomana nakwambia wewe ni nyumbu umemeza porojo za mbowe hivi serikali ilivyochukua hatua kusimamia wananchi wake kulipwa fidia sehemu linapopita bomba la mafuta kutoka Uganda kwenda bandari ya tanga ni kwamba serikali imemlipia fidia TOTAL? Tatizo mkataba mnautafsiri Kwa mujibu wa matamanio yako Ila si hivyo ulivyo.
 
Mkataba ambao hausemi watatugawia nini, wakija kutugawia 0% tutapinga kwa msingi upi?
Pia hicho kifungu ulichoweka si kinaeleza wazi kwamba msamaha wa kodi utajapohitajika utatolewa kwa mwekezaji (DPW)..., na sheria si zinaruhusu kutoa msamaha wa kodi? Hoja ni kwamba kwanini pamoja na kwamba sisi ndio tuliokuwa tunamiliki hiyo bandari (kabla ya mkataba), na sisi ndio tulikopa matrillion kuiendeleza, na hadi sasa tunakamuliwa kodi za miamala ya simu kulipa mkopo huo, halafu yeye aje apewe bure kabisa..., na bado apewe msamaha wa kodi (sheria inaruhusu kutoa hadi 100%), sasa akija kudai kwa kadri mkataba unavyosema, tutamnyima huo msamaha kwa msingi upi ili hali tumeshakubaliana na kusaini kwenye mkataba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…