Zinatoka wapi pesa zinazotumika kujenga miradi mikubwa na mingi inayofunguliwa kila siku Zanzibar?

Zinatoka wapi pesa zinazotumika kujenga miradi mikubwa na mingi inayofunguliwa kila siku Zanzibar?

Je Nyerere alifanya hivyo kwa makusudi au kukosa utashi wa akili ?
Mwl Nyerere nadhani kulikuwa na msukumo wa nje,ingawa suala la muundo yalikuwa makosa yake mwenyewe.
 
Akili za kimasikini ni kufikiri kila kizuri lazima kitoke serikalini. Zanzibar kuna foreign investors na Private Equity funds kubwa zimeenda kuwekeza, pesa za watu na makampuni binafsi.

Mazingira ya uwekezaji Zanzibar ni mazuri kuliko Bara. Leo hii nenda NEMC kajaribu kufungua kiwanda, EIA watakuzungusha mwaka mzima Tanzania Bara, wakati Zanzibar ndani ya siku kadhaa mambo tayari.

Zanzibar wameunda Special Economic Zones kama Dubai ambazo biashara huweza kuoperate bila kusulubiwa na kodi.

sasa wewe endelea kucheka na sera za akina Mwigulu halafu miaka ya mbele Tanzania Bara tutakuwa tukikopeshwa na Zanzibar
 
Ukiangalia television na kusikiliza redio na hata kusoma magazeti utapata habari za miradi mikubwa mikubwa ikifunguliwa kila siku Zanzibar. Miradi hiyo ni kama vile barabara, shule za ghorofa, viwanjwa vy michezo, masoko ya ghorofa, majengo makubwa, viwanda, miradi ya nishati, flyovers, na kadhalika.

Kwa uchumi mdogo wa Zanzibar huwa najiuliza fedha za kujenga miundombinu mikubwa na mingi hivyo kwa muda mfupi tu wa miaka miwili mitatu zinatoka wapi?

Inaonekana wakati wanachukua fedha ni siri kubwa hufichwa, ila wakati wanafungua miradi siri hizo zinafichuka zote!
jiulize kwanini ni baada ya Samia kuwa rais wa Tanzania, jibu liko wazi pesa za Tanganyika. Muungano kuvunjika hakuepukiki, sema mpaka amalize miaka 5 atakuwa amemaliza rasilimali muhimu na Zanzibar itakuwa mbali sana na hatatakuwa wanahitaji tena muungano. Ukimsikiliza Hussein anavyojiamini utafikiri anaokota hela, eti Pemba yote atajenga lami, kwanini leo hiyo miaka yote 60 iliyopita kwanini hizo lami hazikujengwa? Tumeliwa
 
Watanganyika tuamke!
 
Fedha zote zinatoka Tanganyika.
Rais wa Tanganyika ni Mzanzibar.
Rais wa Zanzibar ni Mzanzibar.

Mwl Nyerere alituachia katiba mbaya kuliko katiba zote Duniani.
Hàmna akili Hadi muendelee kufuàta màtakwa ya hayati Nyerere? Kama katiba ni mbàya kwanini mnaifuata?
 
Tanganyika ndo mnatajirisha zanzibar na mtulie akija kumaliza mingine mitano huku bara basi zanzibar itakuwa Dubai ndogo
 
Back
Top Bottom