Zipi ni njia bora za kumpata mfanyakazi mwaminifu

Zipi ni njia bora za kumpata mfanyakazi mwaminifu

Sina Biashara za maana ila tiali ninaye niliye target kuwa ndio manager/Director wa Biashara zangu kubwa hapo baadae...jamaa ndio anayefanya biashara yangu ya sasahivi na kunilipa kwa week.

Nina mpango wa ku-base kwenye biashara aina moja ziwe kama 5 mjini na yeye ndio atakuwa anazi-manage akisaidizana na mimi.

Sikuzote anasema

“Babu unajua umeweka mzigo wako pesa nakuwa makini sana muda mwengine naumiza kichwa naangalia nini kimepungua”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
manengelo,
This is one of big problem..kwa wajasiriamali na wafanyabiashara...Kupata mtu mwaminifu 💯 Ni ngumu na utabadilisha kila siku Biashara zisizo rasmi kubali kuibiwa kidogo Cha muhimu awe anapiga mzigo kwelikweli..
 
Manengelo mbona watu tumejazana humu , njoo tufanye kazi .... Pima uwezo wa mtu kufanya kazi na sio kuangalia huruma, vyeti, ukabila ,undugu n.k

Hapo lazima utaumia... KINGINE WEKA mkaba mezani ...



Kwa maelezo zaidi njoo pm tufanye kazi manengelo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kama huu mfano utasaidia.

Mabaunsa zamani tulikua tukiitwa kulinda Uwanja wa Taifa tunaambiwa malipo ni 30, na tulikua hatukatai kwakua tulikua tunajua kuna njia za kuiba.

Utakuta unawapitisha watu mlango wa nyuma unapata almost 180. Baadaye ikawa tunalinda na askari, upigaji ukaminywa na tukawa tunakataa kazi.

Point yangu ni kwamba kama maslahi yanaendana na kazi anayofanya mtu uaminifu ni given.
 
1. omba recomendations zaidi from resourceful people other than open source
2. boresha mifumo yako na check and balances ili upunguze necessity ya uaminifu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hiyo Ndio changamoto kubwa katika biashara....cha msingi kabla ya kumuajiri jitahidi umjue hasa alicho kuwa anafanya kabla ya kuja kwako...hobies zake ni nini..kikubwa hata kama una mtu jitahidi sana uwepo mara kwa mara kwenye biashara...na ikiwezekana rekodi kila kinachouzwa...na kuhesabu stock mara kwa mara ili kujue kama mnaenda sawa...la sivyo utavuna mabua.
 
Narubongo,
Kaka samahani kwa kutoka nje ya mada tulikutana kwenye uzi wangu wa biashara ya maziwa na samaki...kwa kweli nimefanyia kazi michango ya wadau...na mchago wako umefanya kazi effective ubarikiwe sana kaka
 
Cleverman324, Asante sana mkuu kwa kunikumbuka, napenda sana kutoa uzoefu wangu chanya ili mwanadamu mwingine afanikiwe na asifanye makosa niliyoyapitia mimi au mwingine. Una spirit ya mafanikio wewe komaa tu na hiyo kazi na mwisho wa mwezi jumlisha faida uliyoiopata kwa mwezi mzima halafu ilinganishe na net salary ya mfanyakazi anayefunga tai kila siku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
manengelo,
Mtu mwaminifu hakuna.....hata nduguyo anaweza kukuibia..hakuna mfanyakazi asiyependa ganji na mapigo (michongo) mahala pa kazi..mimi mwenyewe na mwanangu mmoja tulikuwa tunampiga bosi wetu ili tujazie subsistence wage
 
Back
Top Bottom