Zipi ni njia bora za kumpata mfanyakazi mwaminifu

Zipi ni njia bora za kumpata mfanyakazi mwaminifu

Sijui kama huu mfano utasaidia.

Mabaunsa zamani tulikua tukiitwa kulinda Uwanja wa Taifa tunaambiwa malipo ni 30, na tulikua hatukatai kwakua tulikua tunajua kuna njia za kuiba.

Utakuta unawapitisha watu mlango wa nyuma unapata almost 180. Baadaye ikawa tunalinda na askari, upigaji ukaminywa na tukawa tunakataa kazi.

Point yangu ni kwamba kama maslahi yanaendana na kazi anayofanya mtu uaminifu ni given.
Hakuna mfanyakazi anatosheka na Mshahara
 
Askof tza kaka mambo mengi kaka.
Mimi napenda kumpigia mtu simu kama kuna inshu ya maana, ila kama sina inshu ya maana ya kumueleza, huwa nakuwa mzito sana kupiga na hata kutuma sms!
 
Tanzania hii kila aliyemuaminifu kajiajiri na hawatoshi.

Kwa maana hata hao waliojiajiri wapo wanaojiibia wenyewe.

Sahau.
 
Vijana waaminifu tupo, tatizo hatuna koneksheni.
Mimi nimewahi kushuhudia boss flani kamuajiri kijana ambaye haonyeshi kujali kwa lolote kwa kazi anazopewa na boss wake.
Isitoshe hela analipwa vizuri kabisa, boss akija lazima dogo hakosi 5,000 - 10,000 ya soda.
Nikawa najisemea, "hii nafasi ningeipata mimi"
kwahiyo kwa kifupi vijana waaminifu na wachapa kazi tupo! Ila conection za kukutana na maboss ni inshu. Maana mtu umekulia KASANGEZI KIBONDO hao maboss utakutana nao wapi.
Ndyo maneno yenu hya mkiwa mmepigika ila mkipewa na Chanel mnaanza kuonyesha picha zenu halisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hello!

Kuajiri mtu akufanyie shughuli zako sasa hivi ni kitu kinachosumbua sana watu wengi, nikiwemo. Ukisema uajiri ndugu tegemea maumivu tu yasioelezeka.

Ukisema uajiri rafiki tegemea kabisa urafiki kuvunjika hakawii kukuzunguka. Nyie wenzangu mnatumia njia gani bora za kuajiri mtu MWAMINIFU? Yaani ile kazi unamwachia hela ndefu ukisubiria returns, maana huwezi fanya kila kitu mwenyewe.

Ipi ni njia sahihi ya kumpata mtu atleast mwaminifu. Au ulimpataje mtu mwaminifu?

Nawasilisha.
Tafuta kijana kijijini mleta dsm, by early January 2020, niachie just two weeks then chukua kijana wako akachape kazi.

Serious nitafute I will be there starting 11th January 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbwewe wewe kama huwa unakutana na vimeo wanakuonyesha mapichapicha hao ni watu wako. Ila mimi nijuavyo vijana wachapakazi tupo kabisa!
 
Back
Top Bottom