Kauliza mengi hapo tumejibu kipande hicho cha kufika "rinta", iyakua wewe ndio hujaelewa hilo jibu, kama ambavyo ulikuwa hujayaelewa hapo juu kua swali lilijibiwa mpaka kwa picha, ukaleta "upumbavu". Hakuna janja janaja kweye ufundi bora, majibu yapo straight forward, kama kuna ambacho hujaelewa, uliza tu, usitake kukisia. Yeye hajaulizia kuhusu plaster.
Plasta inakuaje vipi? Sasa wewe swali lako ndilo sijalielewa.
HAkuna jibu la maana ulilotoa!
Lakini ngoja niwashauri wadau!
KWA MTU AMBAYE HANA PESA ZA KUJENGA KWA MKUPUO yaani ( boma, umeme, plumbing n.k) Si mshauri hata kidogo atumie hizo tofali, Kuna fumbo limefichwa hapo ndiyo maana wahusika wakali balaa wakiulizwa mambo ya msingi!
Je; ni wapi tofali hizi zinafaa?
Maeneo ambayo tofali hizi zinaweza kutumika kwasasa kuepukana na changamoto ni kujenga UZIO TU au kumbi ambazo hazihitaji mnyumbuliko wa bomba!
UKISHUPAZA SHINGO Usielewe ushauri wangu ukaamua kujengea nyumba basi jiandae na yafuatayo
1. Lazima wakati wa ujenzi wa tofali hizi mafundi wote wa fani mhimu kama maji na umeme wawepo ili kuweka miundombinu (hii ni gharama ya mpigo)
2 .inatakiwa material ya umeme na mabomba yawepo site ( ujenzi wa mpigo unahitaji bajeti)
3. Lazima saiti kuwe na umeme au jenereta kuwasha grenda ( inaongeza gharama)
4. Mafundi makini zaidi kukujengea (wana bei zaidi)
5. Endapo kukitokea mabadiliko au hitilafu ni ngumu kufanya marekebisho
6. Zinahitaji muda mwingi (labour charge ni kubwa)
7. Kwenye majengo marefu Ufungaji majukwaa kwa ajili ya plaster na finishing ni mgumu kidogo ukitumia mbao, labda kukodo majukwaa spesho
Faida za tofali hizi
1. Nyepesi (kupunguza uzito)
2. Mfuko unapata tofali nyingi kiasi
3. Hazitunzi joto
4. Siyo lazima kufanya plaster
5. Zinafaa sana kujengea uzio na mabanda
MWENYE MASIKIO NA ASIKIE kama una hela ya mawazo usijichanganye kwenye hizo tofali HAINA MAANA NI MBAYA HAPANA BALI Maboresho yanahitajika ili kuongeza mnyumbuliko wa kazi