Mkuu, ni uamuzi wako kutosema bei. Ila nakukumbusha kuwa kuna teknojia nyingine pia zilikuja kwa jina la kupunguza gharama na muda wa ujenzi ambazo ni 1. hydraform bricks, EPS/Megapanel na Moladi lakini walaji wameshindwa kuona maajabu yake na kupelekea kupotea sokoni. Maana kwa watanzania tulio wengi, Muda/Time sio issue kubwa, ndio maana huwa tunajenga course 4 kisha tunapumzika, unajikuta tunamaliza nyumba kwa miaka zaidi ya mi2. Ila hiyo teknolojia yako inataka ukija site upige tofali zote ndio uondoke. Wakati kwa traditional method huwa tunanunua tofali hata 200 fundi anajenga kisha tunasimama.
Lakini pia kwa nini unasema bidhaa zenu zinajiuza zenyewe hakuna haja ya kumshawishi mtu. Ni kweli ????? Ulikuwa na lengo gani kuja huku JF na kuanzisha uzi?
Wish you all the best mkuu. Na ngoja niendelee kunywa mtori kwanza, maana nyama nitazikuta kwa chini
Lengo letu kuu ni kuwezeshana, nimekuwekea hizi link za nyuzi zangu mbili chini, ukizipitia ukazisoma labda utapata kuelewa lengo langu kuu la kutangaza JF. Na baada ya kuzisoma kama utakua na maswali zaidi, usisite kuuliza...
"Social Economic Empowerment Program,." Mpango wa Kijamii wa Kuwezeshana Kiuchumi, Kwa mara ya Kwanza Tanzania. Haujawahi kutokea, duniani. Ni mpango uliobuniwa na Madrassatul Abraar, iliopo mtaa wa Vitendo, Misugusugu, Kibaha, Pwani Tanzania. Mpango ulianzishwa nakuasisiwa na Abdul ghafur kwa...
www.jamiiforums.com
Nikirudi kwenye maeleoz yako ya bidhaa nyingine au za kampuni zingine ulizozitaja, ndio maana juu huko nilikwambia sisi tupo tofauti na wengine. Sisi ujenzi wetu umelenga hilo la Mtanzania kujenga kidogo kidogo, tumeenda mbele zaidi ya kozi nne, ujenzi wetu unaweza jenga nusu kozi au robo kozi au hata block moja ukasimama, ni mwanzo mpaka mwisho wa nyumba namna hiyo. Tunataka kumuelimisha kila Mtanzania kua kila mmoja ana uwezo wa kujenga nyumba yenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu. Si lazima ajenge kwetu, tunakufundisha mbinu na siri za ujenzi zinazofichwa na wajenzi wengi ili nawe uweze kujenga.
Kwa ufuppi, tumedhamiria kufanya mageuzi ya namna ya ujenzi na jinsi Mtanzania anavyoweza kuondoka na fikra za kuwa mpangaji wa wenye nyumba daima. Kila Mtanzania anaeweza kufanya kazi anaweza kujenga, awe kima cha chini cha mshahara au kima cha juu. Ni uelewa tu.
Ujenzi wetu unajenga kwa spidi yako, na tuna vifaa ambavyo humuhitaji hata fundi maiko, unaweza wewe mwenyewe kujenga kila wikiendi mpaka ukamaliza ujenzi kwa spidi yako. Bila hata msaidizi au ukasaidiana na mkeo/mumeo.
Nashukuru kuwa fikra zako zipo tofauti na uhalisia wetu na tulivyo hapa Abraar Education Centre. Nafurahi kuona kuwa unapata kujifunza mapya kwetu. Ukiendelea kufatilia nyuzi zetu hapa JF bado una mengi ya kujifunza, kwa ujuzi wako wa miaka 17 ukiulinganisha na wangu wa zaidi ya miaka 40 kwenye sekta ya ujenzi, kuna gap ya miaka mingi ambayo unaweza kuupata japomachache ya kujifundisha kipya kutoka kwangu, kama si vyote. Nami sikatai, najifunza mengi kutokana na maswali yako. Tuendelee.
Hujaninjibu swali nililokuuliza la kuwa upo upande upi wa ujenzi? Hukuliona swali au umelikwepa?