Zitambue fursa za kiuchumi katika Mkoa wa Njombe

Mheshimiwa Mtaka usitoke hapo kabla ya kuuweka mkoa uwe wa mfano Tanzania.

Wewe ni mmoja wa watu makini sana.

Jaribu sana pia kuhakikisha miundombinu yakamilishwa kwa good landscaping yaani lami kuzunguka, maeneo kama hospitali na shule.

Pia upandaji miti pembezoni mwa barabara husaidia kuleta vivuli na mandhari mazuri, bustani katika maeneo nilitaja hapo juu.

Njombe kijiografia ni mkoa mzuri khasa kwa wawezekaji wa kigeni hivyo upangaji mji khasa katikati ya miji kutawezesha kuleta wawezakezaji katika maeneo mengi kama maduka makubwa, huduma , na mambo mengi sana.

Jaribu kubuni kuweka town centres ambazo zitaleta wawezekaji wa kila aina ambao watakuleteeni kodi za maendeleo.
 
N
Na kaupatia kweli mkoa wa njombe anapiga kazi kweli kweli mkoa unabadilika Sana
 
Kila wilaya ikiwa na town centre italeta msukumo wa wafanyabiashara kuhamia huko.

Ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na kuanzisha zones maalum kwa ajili ya biashara.

Yaani unakuwa na town centre, kisha industrial zones na makazi ya watu..

Pia kuhakikisha mkoa wavutia vijana wenye ujuzi mbalimbali kuhamia huko na kuanzisha makazi na biashara na kuweka mazingira mazuri.
 
Kwa mkoa wa njombe naona Hilo wazo ndo wanatembea nalo maana nimezunguka halmashauri zote zote town centre ni wameboresha street road wamepiga lami ko hili jambo ndo linachochea wawekezaji kuingia mkoa wa njombe na wameteua mji wa makambako kuwa logistic centre wanajenga bandari kavu mizigo itasafirishwa na treni
 
Kwa mkoa wa njombe naona Hilo wazo ndo wanatembea nalo maana nimezunguka halmashauri zote zote town centre ni wameboresha street road wamepiga lami ko hili jambo ndo linachochea wawekezaji kuingia mkoa wa njombe na wameteua mji wa makambako kuwa logistic centre wanajenga bandari kavu mizigo itasafirishwa na tren
 
Balaa la mkoa huo bhana ni hiyo baridi tu! Ila kwa fursa ni kama zote. Tanzania ni paradise ya Duniani, Mungu ibariki Tanzania, wabariki watu wake. 🙏 Amen.
 
Uvuvi ziwa nyasa hasa ludewa hua naweka kambi kila mwezi wa saba hadi wa kumi nanunua dagaa nyasa wa kupeleka Angola na zimbabwe tatizo lenu hamjui hata kama mna hiyo fursa hua nakaa miezi mitatu pale ludewa 7-10.
Watu wanajua fursa za dagaa labda useme soko nje ya nchi
 
Sahihi
 
Kinachotakiwa saizi kwenye huu mkoa ni kuweka barabara njia nne Kipande Cha makambako hadi njombe kutokana na hii Barabara inaunganisha halmashauri zote sita na na kwa Sasa imeanza kuzidiwa kwa kuwa na msongamano hii imepelekea kuwa na trafic light kama nne kipande hicho na msongamano utazidi zaidi utakapo Anza mgodi wa ludewa
 
Kwa kuwa barabara zimejengwa tayari, bado pia njia za watembea kwa miguu zahitajika , mifereji ya maji na taa za barabarani.
 
Hapo iko sawa naona mifereji na njia za watembea kwa miguu.

Hapo zahitajika taa za barabarani na taa za solar zatosha sana.

Picha ya juu ionyeshayo mtaa wa residential watakiwa kufanyiwa kitu chaitwa Residential road improvement yaani barabara za kuingia kwenye makazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…